Kwanini Zitto nisikuite msaliti?

Kwanini Zitto nisikuite msaliti?

Kwa wale wanaopinga kwamba ZZK hakuwa msaliti kwa Chadema lazima sasa waamini alikuwa msaliti, na hii ni kutokana na yeye mwenyewe kukiri.

Gazeti la MAWIO limemnukuu Zito katika kujitetea kwake kwamba alikuwa anakutana na JK mara kwa mara kuzungumzia 'masuala ya kitaifa.' Lakini alikuwa hawajulishi viongozi wenzake katika Chadema kabla au hata baada ya hiyo mikutano yake na JK

Sasa tuamini walikuwa wakiongelea masuala ya taifa? Ikumbukwe kuwa kipindi cha vikao vyao mpaka kupelekana Ethiopia,Zito alikuwa ni kiongozi CHADEMA.
 
Mkuu, ni wachache sana wanaobisha kwa kusema zito hakuwa msaliti kwa moyo wa dhati ukiasisiwa na kukosa taarifa. Wengi wanaobisha humu ni wanufaika ama mawakala wa wanufaika wa usaliti huo ambao wanaufunika makusudi. Kufunika huko ni ama kuendelea kumwacha zito kwenye green circles ili wazidi kunufaika ama kutaka kuonyesha kwamba CHADEMA wamekuwa unfair na zito ili kupaka matope chama kwa lengo lile lile alilokuwa akilitimiza zito kwa usaliti.

Ukwlei unajulikana. Zito ni msaliti na haaminiki. CHADEMA bila Zitto inazidi kuimarika maradufu na kuenea kwa kasi ya mwanga. Si Ukawa wala CHADEMA vitaathrika na propaganda za makusudi kutoka kwa washindwa ccm.

Wale wasiokuwa na taarifa sahihi, ulizeni mtaelezwa lakini kutetea kwamba zito hajasaliti chadema ni kujidhalilisha.
 
Zitto ataisumbua sana Bavicha. Pateni viroba mkalale. Msaliti ni yule aliyemkana Yesu na kuukacha upadre. Kisha kumsaliti mkewe na kutwaa mwanamke wa watu.
 
huyu jamaa bila mods asingeweza jibu sifa zake humu ndani
 
Sidhani kama kulikua na tatizo zitto kukutana na Rais wa nchi yake. Na kukutana na Rais haimaanishi kua alikua nafanya hujuma dhidi ya chama chake.

Huu ni uzushi na unafiki usio na mashiko.
 
Kwa wale wanaopinga kwamba ZZK hakuwa msaliti kwa Chadema lazima sasa waamini alikuwa msaliti, na hii ni kutokana na yeye mwenyewe kukiri.

Gazeti la MAWIO limemnukuu Zito katika kujitetea kwake kwamba alikuwa anakutana na JK mara kwa mara kuzungumzia 'masuala ya kitaifa.' Lakini alikuwa hawajulishi viongozi wenzake katika Chadema kabla au hata baada ya hiyo mikutano yake na JK

Sasa tuamini walikuwa wakiongelea masuala ya taifa? Ikumbukwe kuwa kipindi cha vikao vyao mpaka kupelekana Ethiopia,Zito alikuwa ni kiongozi CHADEMA.

Hii nayo ni thread kweli!? Mods, tupa kureee!
 
Zitto ataisumbua sana Bavicha. Pateni viroba mkalale. Msaliti ni yule aliyemkana Yesu na kuukacha upadre. Kisha kumsaliti mkewe na kutwaa mwanamke wa watu.

This time next year I will remind you about this reply
 
.Tuliaminishwa tukaamini kua Tanzania kuna upinzani imara sijui kama bado tuna imani hiyo
.Tukaaminishwa tukaamini kuwa uzaledo ni kufunga mikanda tukaifunga sawasawa wenzetu wakailegeza wakanenepa
.Tuliaminishwa kua wazungu ndio wabaguzi peke yao, baada ya kuchomwa moto na weusi wenzetu huku tukiokolewa na wazungu hatuamini hivyo tenaq
.Tuliaminishwa tukaamini eti Nduli alipata kula nyama za watu, mpaka sasa sijui ni wa gapi bado wanamini hivyo
.Tuliaminishwa tukaamini kuwa kutoa na kupokea rushwa ni kosa kubwa ,, bado tunaamini hivyo ila mhhhh mbona wale watoaji wa..... wako huru
.Tuliaminishwa tukapinga kuwa daraja la Kigamboni ni possible,, leo tunaona aibu daraja limekamilika
Tuliaminishwa tukaamini kua kuna mchungaji anatoa misukule,, sijui kama bado tuna amini katika hili
Tuliaminishwa tukaamini eti ZZK ni msaliti nadhani tumebaki wachache tunao amini katika hili
.Tuliaminishwa tukaamini kua Tanzania ni kisiwa cha amani, tulipoanza uwa ndugu zetu albino sidhani kama tunaweza amini dhihaka hii
.Tuliaminishwa kua Mtwara na Kigoma kuhamishiwa kule kikazi ni kama adhabu,,sasa tunagombania kwenda huko

JE WEWE NDUGU YANGU ULIAMINISHWA NINI NA SASA HALI NITOFAUTI?
 
Wewe ZZK atakupoteza kama sio njaa yako. Baada ya miaka 20 ya vyama vingi hatukuhitaji wala kumtuma mtu kuanzisha chama kipya, huyo mtu lazima akili yake ni fupi mno na wala sio mwanaukombozi hata kidogo
 
Tuliaminihwa kusoma sana ndio kufanikiwa maisha kumbe wapi unaweza soma nausifanikiwe maisha na unaweza usisome naukafanikiwa maisha maana kuna ujasiliamali
 
kama zzk hutaki madaraka kwanini hukujiunga na chama kingine ambacho kina uongozi tayari.Utakao wandanganya hawazidi % 0.002 ya watz.Utawandanganya watz lakini huwezi kuwandanganya watz wakati wote unajisumbua bure.
 
Mimi mpaka sasa bado naamini Zitto kabwe ni msaliti na sikuaminishwa nimejionea mwenyewe usaliti wake.
 
.Tuliaminishwa tukaamini kua Tanzania kuna upinzani imara sijui kama bado tuna imani hiyo
.Tukaaminishwa tukaamini kuwa uzaledo ni kufunga mikanda tukaifunga sawasawa wenzetu wakailegeza wakanenepa
.Tuliaminishwa kua wazungu ndio wabaguzi peke yao, baada ya kuchomwa moto na weusi wenzetu huku tukiokolewa na wazungu hatuamini hivyo tenaq
.Tuliaminishwa tukaamini eti Nduli alipata kula nyama za watu, mpaka sasa sijui ni wa gapi bado wanamini hivyo
.Tuliaminishwa tukaamini kuwa kutoa na kupokea rushwa ni kosa kubwa ,, bado tunaamini hivyo ila mhhhh mbona wale watoaji wa..... wako huru
.Tuliaminishwa tukapinga kuwa daraja la Kigamboni ni possible,, leo tunaona aibu daraja limekamilika
Tuliaminishwa tukaamini kua kuna mchungaji anatoa misukule,, sijui kama bado tuna amini katika hili
Tuliaminishwa tukaamini eti ZZK ni msaliti nadhani tumebaki wachache tunao amini katika hili
.Tuliaminishwa tukaamini kua Tanzania ni kisiwa cha amani, tulipoanza uwa ndugu zetu albino sidhani kama tunaweza amini dhihaka hii
.Tuliaminishwa kua Mtwara na Kigoma kuhamishiwa kule kikazi ni kama adhabu,,sasa tunagombania kwenda huko

JE WEWE NDUGU YANGU ULIAMINISHWA NINI NA SASA HALI NITOFAUTI?

Tuliaminishwa tukaamini, kuwa aliyepost thread hii ni mkweli sijui kama bado tunaamini
tuliaminishwa tukaamini kuwa huyu jamaa si mmoja wawale wanaolipya buku saba sasa kwa thread hii sijui kama bado 2naamini.
 
Back
Top Bottom