Kwanini Zanzibar inakuwa mbele kutoa taarifa za Corona kuliko Tanzania bara?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,125
142,223
Ukiwa mfuatiliaji wa habari utagundua mara zote waziri wa afya Zanzibar mh Hamad Rashid amekuwa akimtangulia Ummy Mwalimu kwenye kutoa taarifa za Corona.

Mfano kuwaweka abiria wanaoingia nchini katika karantini alianza Hamad then Ummy akafuatia.
Jana Hamad Rashid katangaza ongezeko la mgonjwa mmoja leo Ummy karudia kitu hivho hicho.

Lakini nimeangalia kwenye taarifa za WHO kule sijaiona Zanzibar kuna Tanzania

Labda Hamad Rashid na Ummy Mwalimu wakubaliane namna ya kutoa taarifa kwa pamoja kwani sisi ni nchi moja mbele ya Dunia.

Nawasilisha

Maendeleo hayana vyama!
 
... kwanza corona yaani afya sio suala la muungano. pili eneo dogo sana lile, wakificha taarifa watakwisha wale.

... by the way, idadi ya wagonjwa wa Tanzania inajumuisha ile ya Zanzibar? Namaanisha jumuiya za kimataifa kama WHO wanachukua taarifa za Ummy au wanachukua za Ummy na kuongeza zile za Zanzibar kama statistics za Tanzania?
 
Kwasababu wao wana VIONGOZI sisi tuna WATAWALA.
Wakitangazwa mnasema mambo ya familia, kwanini familia zingine zinatangazwa, ikitangazwa ya Mbowe kunakuwa na NONGWA au ni special?

Corona haina CHAMA
 
... kwanza corona yaani afya sio suala la muungano.
... pili eneo dogo sana lile, wakificha taarifa watakwisha wale.
... by the way, idadi ya wagonjwa wa Tanzania inajumuisha ile ya Zanzibar? Namaanisha jumuiya za kimataifa kama WHO wanachukua taarifa za Ummy au wanachukua za Ummy na kuongeza zile za Zanzibar kama statistics za Tanzania?
Nadhani Hamad hatambuliki WHO!
 
Back
Top Bottom