Marcostilone
JF-Expert Member
- Jun 25, 2023
- 7,019
- 17,839
Nimeisoma mistari yote uliyotoa mkuu, na kama mwanatheolojia nadhani unajua kitu kinaitwa contextual hermeneutics.Unapotaja Yohana 17:3 au Yohana 20:17 ambapo Yesu anamwita Baba Mungu wangu hiyo inaakisi kabisa hali yake ya unyenyekevu katika mwili wa nyama yani Kenosis kama inavyofafanuliwa kwenye Wafilipi 2:5-8).Kwanza historia ya dini nimeisoma na nakumbuka miaka 30 iliyopita nilifanya reseach kuhusu hiyo historia mpaka israel so ilikuwa ni moja ya my specialtykwahiyo tunaweza kuizungumzia wiki nzima bila kuchoka.. pili Nimeitumia njia yako mwenyewe ya hoja ili kukuonyesha jambo moja muhimu. Umeniletea uamuzi wa Baraza la Nicea ili kuthibitisha uungu wa Yesu, lakini kwa kufanya hivyo umekiri kwamba hoja yako inategemea tafsiri na maamuzi ya wanatheolojia wa karne ya nne, si maandiko.
Kwa mantiki hiyo hiyo, kumbuka kwamba neno "Utatu" (Trinity) halipo popote katika Biblia. Ni neno lililotungwa baadaye na wanatheolojia ili kuelezea mafundisho fulani. kama tunarudi kwenye mamlaka ya Biblia, basi hoja yetu lazima isimame juu ya maandiko yaliyoandikwa, sio kwenye maamuzi ya mabaraza ya kanisa, ambayo ukitaka tunaweza kudiscuss udhaifu wa mabaraza yote kuanzia baraza la nicea mpaka Council of Trent..
Mimi sitaki tujadili kuhusu liturujia, mapokeo ya kanisa, wala dogma zilizokuja baadaye. Nataka tujadili kile kilichoandikwa katika Biblia.
Kwa mfano, Biblia ina maandiko kama aliyotoa mtoa post wa nyuma hapo na kakupa ila hujajibu ila umeleta porojo kama:
Naomba unioneshe andiko linalosema wazi na bila utata "Yesu ndiye Mungu Mwenyezi," au "Mungu ni Utatu wa Nafsi Tatu." Kama lipo, tulisome pamoja katika muktadha wake.
- Yohana 17:3 – Yesu anamwita Baba "Mungu wa pekee wa kweli."
- Marko 12:29 – Yesu ananukuu: "Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja."
- Yohana 20:17 – Yesu anasema: "Ninakwenda kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu."
- 1 Wakorintho 8:6 – "Kwetu sisi yuko Mungu mmoja, Baba... na Bwana mmoja, Yesu Kristo."
- 1 Timotheo 2:5 – "Yuko Mungu mmoja, na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, mwanadamu Kristo Yesu."
Kwa taarifa yako, mimi ni mwanatheolojia na nimejifunza na kufundisha theolojia kwa takribani miaka 39. Kwa hiyo, siogopi mjadala wa kisomi wa kiblia, Lakini ningependa mjadala wetu ujengwe juu ya Sola Scriptura yaani, kile Biblia inasema ,badala ya maamuzi ya mabaraza ya kanisa, liturujia au dogma zilizotungwa baada ya enzi za mitume.
Tukubaliane jambo moja tuache kunukuu mamlaka za watu, turudi kwenye mamlaka ya Maandiko. Hapo ndipo mjadala utakuwa wa haki na wenye manufaa.
nakuwasilishia
Yesu alitwaa namna ya mtumwa, akawa mwanadamu kikamilifu, hivyo kisheria na kiutu alikuwa chini ya Mungu.Lakini huyo huyo Yohana aliyeandika hiyo injili anaanza sura ya kwanza mstari wa kwanza kwa kusema: Hapo mwanzo kulikuwako Neno... nalo Neno alikuwa Mungu. Na mstari wa 14 anasema Neno akawa mwili.
Kama tunasimama kwenye Sola Scriptura, hatuwezi kuchukua mistari ya utu wake tukafuta mistari inayotaja Uungu wake. Yohana alimaliza kwa kumwonyesha Tomaso akimwambia Yesu: Bwana wangu na Mungu wangu! Ukisoma Yohana 20 utaelewa na Yesu alikubali. Kama Yesu hakuwa Mungu, hayo yaliyowekwa kwenye maandiko yangekuwa ni kufuru.
Tukiacha mapokeo na mabaraza ya karne ya nne, unabii wa Agano la Kale unamtajaje huyu Kristo anayekuja?