Hebu nikukumbushe historia kidogo. Baraza la Nicea lilikaa kupinga uzushi wa mzee mmoja anaitwa Arius, ambaye alikuwa anasema Yesu si Mungu kamili bali ni kiumbe tu, na alikuwa anapigania neno Homoiousios kwamba Yesu anafanana tu asili na Mungu.
Baraza la Nicea likamkataa Arius na likapitisha neno Homoousios kwamba Yesu na Baba wana ASILI MOJA, UUNGU MMOJA, NA UTUKUFU MMOJA WA Milele!
Ukidai Yesu sio Mungu, si unakuwa unashikilia msimamo wa Arius aliyelaaniwa na hilo baraza? Baraza la Nicea lilithibitisha Uungu wa Yesu, wewe unalitaja kama fimbo ya kunipiga mimi? Umesoma vizuri lakini au umegoogle juu juu tu Mkuu?
Kwanza historia ya dini nimeisoma na nakumbuka miaka 30 iliyopita nilifanya reseach kuhusu hiyo historia mpaka israel so ilikuwa ni moja ya my specialtykwahiyo tunaweza kuizungumzia wiki nzima bila kuchoka.. pili Nimeitumia njia yako mwenyewe ya hoja ili kukuonyesha jambo moja muhimu. Umeniletea uamuzi wa Baraza la Nicea ili kuthibitisha uungu wa Yesu, lakini kwa kufanya hivyo umekiri kwamba hoja yako inategemea tafsiri na maamuzi ya wanatheolojia wa karne ya nne, si maandiko.
Kwa mantiki hiyo hiyo, kumbuka kwamba neno
"Utatu" (Trinity) halipo popote katika Biblia. Ni neno lililotungwa baadaye na wanatheolojia ili kuelezea mafundisho fulani. kama tunarudi kwenye mamlaka ya Biblia, basi hoja yetu lazima isimame juu ya maandiko yaliyoandikwa, sio kwenye maamuzi ya mabaraza ya kanisa, ambayo ukitaka tunaweza kudiscuss udhaifu wa mabaraza yote kuanzia baraza la nicea mpaka Council of Trent..
Mimi sitaki tujadili kuhusu liturujia, mapokeo ya kanisa, wala dogma zilizokuja baadaye. Nataka tujadili kile kilichoandikwa katika Biblia.
Kwa mfano, Biblia ina maandiko kama aliyotoa mtoa post wa nyuma hapo na kakupa ila hujajibu ila umeleta porojo kama:
- Yohana 17:3 – Yesu anamwita Baba "Mungu wa pekee wa kweli."
- Marko 12:29 – Yesu ananukuu: "Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja."
- Yohana 20:17 – Yesu anasema: "Ninakwenda kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu."
- 1 Wakorintho 8:6 – "Kwetu sisi yuko Mungu mmoja, Baba... na Bwana mmoja, Yesu Kristo."
- 1 Timotheo 2:5 – "Yuko Mungu mmoja, na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, mwanadamu Kristo Yesu."
Naomba unioneshe andiko linalosema wazi na bila utata
"Yesu ndiye Mungu Mwenyezi," au
"Mungu ni Utatu wa Nafsi Tatu." Kama lipo, tulisome pamoja katika muktadha wake.
Kwa taarifa yako, mimi ni mwanatheolojia na nimejifunza na kufundisha theolojia kwa takribani miaka 39. Kwa hiyo, siogopi mjadala wa kisomi wa kiblia, Lakini ningependa mjadala wetu ujengwe juu ya
Sola Scriptura yaani, kile Biblia inasema ,badala ya maamuzi ya mabaraza ya kanisa, liturujia au dogma zilizotungwa baada ya enzi za mitume.
Tukubaliane jambo moja tuache kunukuu mamlaka za watu, turudi kwenye mamlaka ya Maandiko. Hapo ndipo mjadala utakuwa wa haki na wenye manufaa.
nakuwasilishia