Hukumuzuku
JF-Expert Member
- Aug 29, 2008
- 6,691
- 5,041
Wazungu wana matabaka aka social classes. Waliomaliza vyuo au elimu ya juu kiujumla wanakuwa wapo makini na afya zao na aina ya vyakula wanavyokula, hawa wana kipato kikubwa na kwa Marekani wanapenda kwenda grocery stores kama Whole Foods, Costco, Trader Joe's, etc. Wale wenye elimu duni wanapenda sana kula vyakula vya bei rahisi, vyenye sukari, chumvi, mafuta na kemikali nyingi vilivyotengenezwa viwandani au processed foods vikijumlisha fast foods kama pizza, burgers, fries, ice cream, fried chicken, soda, candy, smoothies, fish & chips, kebab, canned food, frozen microwave ready meals, etc. za restaurants na supermarkets za bei rahisi kama Walmart, Spar, Lidl, Aldi, etc. Kundi la mwisho huwa hawapendi kupika au kutengeneza chakula from zero. Hawa ndiyo utawakuta ni overweight sana.