Kisa cha TUPAC SHAKUR hadi P-DIDDY kuhusishwa na kifo chake

Arnold Kalikawe

Senior Member
Sep 28, 2016
145
335
Ni usiku mkubwa, wa pambano la kati ya Mike Tyson na Sheldon. Ni usiku ambao ulitokea tukio moja kubwa na la kusikitisha sana kwenye ulimwengu wa muziki. Huku pambano likiwa limemalizika na watu kurudi majumbani kwao na wengine kuendelea kula bata katika hoteli kubwa ya MGM, milio ya risasi inasikika mitaani.

Ni kwenye mataa hapo Vegas, mwanaume aliyekuwa na bastola akaamua kummiminia mwana hip hop, Tupac Shakur huku pembeni yake akiwemo Suge. Ni mauaji ya kutisha, yaliyochochea uhasama zaidi baina ya watu wa Mashariki na Magharibi.

Wakati watu wakiwekeana bifu, kutoleana bastola mitaani, hali ilionekana kubadilika na kuamini kwamba sasa ilikuwa ni vita, ule ugomvi wao ukachochewa na mauaji hayo ya Tupac ambaye kwa kipindi hicho alikuwa akifanya vizuri sana, alifanya muziki na kupiga muvi kadhaa.

Kifo chake kilikuwa ni huzuni kwa kila mtu, kijana mpambanaji, msela alikatishwa ndoto zake kama upepo, yaani katika foleni ya mataa barabarani, uhai wake ukachukuliwa hapo. Tupac akaondoka.

Nani amefanya mauaji hayo? Sasa kila mtu akaanza kusema lake, kuna wengine walisema ni Notorious BIG ndiye aliyefanya mauaji hayo. Kumbuka by then BIG na Sean Combs ‘Puff Daddy’ ama P. Diddy kama alivyobadilisha jina tena walikuwa ni washikaji sana, wala bata kishenzi, watu wengi wakasema kwamba masela hao ndiyo waliokatisha uhai wa mwana. Kwa nini?

Walikuwa na bifu zito mno. Akina Ice Cube, Easy E, Dr Dre walijitahidi sana kuufanya muziki wa Hip Hop kuwa juu lakini kupitia muziki huo, kuna madogo Janja wakaja na kuwekeana bifu kali.

Kabla ya kifo cha Tupac, kulikuwa na bifu kali kati yake na BIG kiasi cha kumgongea mpaka mkewe, Faith Evans. Hiyo ilimuuma mno BIG lakini hakusema kitu, wakati bifu likiendelea, Tupac na wenzake wakatoa diss track moja kali sana.

Inasemwa hiyo ni diss track kali kuliko zote zilizowahi kuimbwa duniani. Ngoma ilikuwa kali, iliitwa Hit ‘Em Up. Humo alisema kabisa kwamba ‘Unajifanya playboy lakini nimekugongea mkeo’. Ile ngoma mpaka P diddy aliwahi kukiri kwamba kila alipokuwa akiisikiliza, alihisi kitu chenye ncha kali kikiuchoma moyo wake.

Tupac alijua kuchamba, aliwachamba akina BIG na akawachamba mpaka wale ambao walikuwa wakienda kujiunga na Bad Boys. Hakuishia hapo, kulikuwa na msanii Prodigy wa kundi la Mobb Deep ambaye alikuwa anaumwa ugonjwa wa Sickle Cell, naye akampa makavu yake kupitia ugonjwa huohuo, alimdhiaki mpaka jamaa mwenyewe.

Baada ya kutoa ngoma hiyo, ugomvi ukawa mkubwa zaidi. Faith alimpa Tupac kwa siri lakini jamaa alishindwa kujishika, akaenda kutoa siri kwamba alipewa na akala, yaani wewe pamoja na kuwakula mademu wa watu, mimi nimemkula mkeo, ilikuwa balaa kipindi hicho.

Ngoma ikawa hewani mpaka kupigwa risasi. Ndiyo! Tupac aliuawa kwa sababu ya bifu tu. Nani alimuua Tupac, hakuna anayejua. Watu wengi walikamatwa, wakawekwa vizuizini lakini wakaachiwa.

Miaka ikakatika na kukatika. Majanga yakamuangukia Suge. Kwa nini? Watu wakahoji kwamba kwa sababu gani mchizi alikuwa pembeni ya Pac halafu hata risasi hazikumpata? Inamaana wapigaji walikuwa na huruma sana kiasi cha kumuacha?

Ukiachana na hilo watu wakahoji. Tupac alitaka kujitoa kwenye lebo ya mchizi, alikuwa kwenye harakati za mwisho, halafu ghafla tu, Pac anauawa, watu wakasema mchizi alicheza mchongo, naye akakamatwa.

So kesi ilikwenda. Kwa wenzetu huwa hawafungi faili hata ikiwa imepita miaka mingapi. Mfano nodiebwoy niwe nafuatilia mauaji ya Mhaya , ninafuatilia weee, nitakapostaafu, faili ninamuachia dogo janja mpya naye anaanza kufuatilia kwa undani. So tangu mwaka 1996 mpaka mwaka huu FBI walikuwa wakifuatilia, nani alimuua Pac?

Wiki kadhaa nyuma hapo, kuna mchizi alikamatwa na polisi kwa kuhusika na mauaji ya Pac. Huyu anaitwa Keef D. Watu walimtia hatiani na kuondoka naye, baada ya kufika huko akafanyiwa mahojiano. Kwenye hayo mahojiano si ndiyo voice imevunja kwamba mchizi amemtaja P Diddy kwamba alimtuma kumuua Pac kwa malipo ya dola milioni 1 (Shilingi bilioni mbili hizi na ushee).

Oya! Mambo yamekuwa mabaya sana, kuti kavu limemkalia P Diddy. Mara kadhaa akina Eminem, 50 Cent waliwahi kuimba kuwa jamaa alihusika kwenye mauaji ya Pac lakini hakuna mtu aliyeelewa, wengi walihisi kama wanazingua.

Sasa mahojiano ya Keef D yanajieleza kwamba ni kweli alitumwa na Diddy kwenda kufanya mauaji hayo. Sasa bhana sisi Wabongo tushaanza kuleta porojo kwamba Wazungu wameanza harakati zao kwa watu weusi kutaka kuwafilisi kama ilivyo kwa R. Kelly. Wanaoongea hivyo ni wale vijana waliozaliwa mwaka 1990 kwenda juu, they know nothing kuhusu suala hili.

Wangekuwa wanajua kuhusu bifu kubwa la West na East wasingeongea hilo. Baada ya Tupac kuuawa, masela wanaona siyo kesi, wakaenda kumdedisha BIG kuwa kama kisasi. Sasa bhana kwenye hili napo kuna jambo.

Wengi wanasema ni Diddy ndiye aliyeamua kumdedisha BIG kutokana na umiliki wa pesa aliokuwa akiutamani sana. Alibaki Faith Evans ambaye naye hana mitikasi sana kuhusu pesa za BIG ambazo kimsingi aliwekeza na Diddy.

Vyanzo mbalimbali vilizidi kuelezea kwamba hata Mase (Jamaa nilimfagilia sana) alikuwa ananyonywa sana na Diddy. Unaikumbuka ile ngoma bora miongoni mwa ngoma bora duniani ya More Money More Problem? Mpaka leo hii japokuwa Mase alikamua sana lakini hakupata hata senti moja. Yaani ngoma ilisikilizwa, ikashinda matuzo kibao ila Diddy aliamua tu kuchukua mkwanja wote.

Usione watu matajiri bro! Kuna mambo mengi wanayafanya nyuma ya pazia. Mambo yanazidi kuwa makubwa, ni siku chache tu baada ya Jamie Foxx kusema kwamba Diddy ni mtu wa upinde, akaanza kuumwa sana mpaka kulazwa, alitaka kudedi ila akanusurika.

Ukijenga bifu na Diddy, anakumaliza. Ukiwa kwenye lebo yake na ukatoka, huwezi kusikika tena. Hata pale Marekani ukitaka kushinda tuzo kubwa kama Grammy, bro! Weka ukaribu na Diddy na Jay Z, vinginevyo unaweza kutoka kapa (Hasa kwa sisi Waafrika)

Tunasikilizia kuitwa kwa Diddy naye akatoe maelezo. Mara kadhaa alisema hamjui Keef D ila kuna video nyingi zilionyesha wapo klabu wanakula bata. Nazo zitatumika.

Wanasema kwamba jamaa alihonga FBI miaka ile kuzika ishu ile, sasa kwa nini imeibuka na watu wameivalia njuga? Wengi wanataka Diddy ashikishwe adabu na kufungwa. Unamuuae Tupac? Kipenzi cha watu, mwanamuziki aliyemuimbia mama yake bonge moja la ngoma, mwanamuziki aliyeimba ngoma iliyohusu jimbo la raha la California, huyu mtu unamuuaje? Huyu jamaa mpaka akawa anachukiwa na Michael Jackson, kisa tu kumkula Janeth Jackson bila huruma.

Oyaaa! Tunasubiri kesi.
View attachment 2780792
 
_20231013_114920.JPG
 
Mkubwa umeelezea vizuri sana. Hata mimi niliyekuwa sina clue yoyote juu ya hii issue nimeielewa kinaga ubaga. Big up chief
 
Daah mkuu much thanx apa sasa nimepata mwanga.
 
Maisha ya jasusi huwa hayana thamani dakika yoyote ile tarajia meza kupinduliwa juu chini.
Umeielezea hii issue juu juu sana nataka uchimbe ndani zaidi watu wapate madini ya kushiba hapa nazungumzia uje na nondo za kiintelijensia zaidi shusha posti nyingine mkuu ujazie nyama kwenye huu uzi.
Sitapenda uishie hapo tu najua wewe ni mfukunyuzi mzuri kazi tumekuachia shusha nondo.
 
Back
Top Bottom