The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,355
- 17,321
Leo Baraza la mitihani limetangaza matokeo ya kidato cha 2,4 na mitihani ya ufahamu kwa wanafunzi wote waliofanya hiyo mitihani mwaka 2021.
Mwezi june 2022 itatutangazia matokeo ya form 6 pia kama kawaida ya miaka yote, kila mwaka ni matokeo ya ulinganifu wa nani kafanya vizuri na nani kafanya vibaya.
Kinachonisikitisha ni kwamba pamoja na udhaifu mkubwa sana wa huu mfumo wa elimu tulionao ambao bado unawaandaa wanafunzi kua waajiriwa, bado wazazi wengi kama sio wote wako na tamaa ya kuona watoto wao wanapata A ama B au Div 1 au 2.
Wote tunakubaliana kwamba huu mfumo wa kupima watu uelewa ama ufahamu wa kukabiliana na changamoto zinazowazunguka ni wa hovyo lakini bado wazazi wako very much obsessed na As. Pamoja na kwamba huu mfumo wa mitihani ni mbovu, unaua ubunifu, ugunduzi, uvumbuzi na uchambuzi wa masuala muhimu kwenye jamii lakini bado Tanzania yunaikumbatia na kuushadadia kwa kila hali.
Tujiulize, hao top 10 wa kitaifa wa kila mwaka, yaani Tanzania kila mwaka tunapata watu wenye akili kuliko wote 20, je hao ma genius hua wanasaidia nini taifa? Je wanakua na mchango gani kwa nchi? Utashangaa hao brainy ama geniuses 20 wa kila mwaka huishia kupewa kazi serikalini, kuajiriwa eitha kua waalimu vyuo vikuu ama maafisa wa kawaida wa serikali.
Dhana ya elimu ni kumpa mtu ufahamu, uelewa na ujuzi wa kukabiliana na changamoto na mazingira yanayomzunguka. Sasa hnajiuliza toka lini kupata elimu ikawa mashindano? Kwamba hata kutatua changamoto zinazotuzunguka tunazitatua kwa mashindano? Ama mtu akipata A basi yeye atatatua changamoto haraka zaidi na kwa ufanisi kuliko aliepata D? Mbona hatuoni faida za A ama Div 1 kwenye jamii?
Hivi 1 zilivyo nyingi kila mwaka sitegemei Tanzania bado tungekua na changamoto yoyote inayotuzunguka maana tuna geniuses wa kutosha.
Hii mada inaendelea.