Kwanini watumishi wa Mungu hawamuelewi Goodluck Gozbert?

Praise the lord..
Hivi kwanini watu wamejaribu kumuandama Goodluck Gozbert mara nyingi watumishi wa Mungu wamekuwa wakimuona wa dunia na sababu zao kubwa ni uvaaji wake.

Uimbaji wake hapa wanapenda kuzungumzia suala la kutungia baadhi ya wasanii nyimbo kama baraka prince.

Suala lingine ya kuwa uimbaji wake hajawahi taja jina la Yesu

Nyie mnamuelewaje kwani???

New-song shukrani
huyu dogo amekaa kishoga shoga
 
naona watu wa dini za wazungu na waarabu mnanena kwa lugha mnazoelewana...hakunihusu mimi nisiyemuamini yehova
 
Mbona wimbo wake mpya japo hakumtaja YESU lakini kamtaja MUNGU, nanukuu "Ninakushukuru MUNGU sababu ya mengi/ hata uhai huu sikustahili/ Ninakushukuru MUNGU tena sababu ya vingi/ hata nikiwa nasali ujue namaanisha...
 
Mungu haangalii mavazi,mwili,umbo au uzuri yy anaangalia moyo afu Mungu aonavyo ni tofauti na ss binadamu tuonavyo kumtumikia Mungu si lazima uvae suruali ya kitambaa na shati la thatini na tai usikariri badilika

Sent using Jamii Forums mobile app
very unfortunately, Mungu anaangalia hata mavazi unayovaa,ndio maana kuna aina ya mavazi anaruhusu, menigne haruhusu, wala msifuatishe namna ya dunia hii.....usiishi kwa kubadilika kadiri dunia inavyotaka bali kadiri Neno la Mungu linavyotaka. usijevaa vibaya, mfano mwanamke kavaa mavazi ya kikahaba akasema Mungu anaangalia moyo sio mavazi, usije kaa pamoja na watu wenye mizaha wanaomdhihaki Mungu, chagua marafiki wa kuwa nao kondoo wa Bwana wanaijua sauti yake na humfuata, hakuna ukristo tofauti na ukristo wa watu wengine, kama kweli unaongozwa na Roho yule yule wa Kristo ambaye na wenzio wanaye lazima mtakuwa na tabia zinazoendana. binafsi huwa simwelewi kuanzia mapozi, nyimbo zake, kutunga nyimbo ya kidunia isiyokuwa ya kimungu, unajua bongoflava ni nyimbo za kishetani/hazihamasishi watu kumtumikia Mungu, zinahamasisha tu uzinzi, ugomvi na takataka za dunia hii, ukiona mtumishi anawatungia watu wa dunia nyimbo jua hana Mungu, anahitaji msaada.
 
Hamtaji YESU lakini anamtaja MUNGU. Wimbo wake mpya wa SHUKRANI kafanya hivyo akimshukuru MUNGU.
jamaa target yake ni watu wote wenye imani tofauti ndomana hamtaji Yesu pia msanii mwengine ambaye hamtaji yesu kwenye nyimbo zake na anakiki ni Angel Benard. kiukweli wamefanikiwa kwa hili maana comments za nyimbo zao zina watu wa imani tofauti tofauti
 
"Umeugua tumaini la kupona hakuna. Usimtizame mwanaadamu, siku zako zimekaribia".
Ni mashairi katika ule wimbo wake wa "Ipo siku", sasa me nahisi hapo ndipo shida inapoanzia na hao wakuu.
 
Praise the lord..
Hivi kwanini watu wamejaribu kumuandama Goodluck Gozbert mara nyingi watumishi wa Mungu wamekuwa wakimuona wa dunia na sababu zao kubwa ni uvaaji wake.

Uimbaji wake hapa wanapenda kuzungumzia suala la kutungia baadhi ya wasanii nyimbo kama baraka prince.

Suala lingine ya kuwa uimbaji wake hajawahi taja jina la Yesu

Nyie mnamuelewaje kwani???

New-song shukrani
Ungeweka na kapicha mkuu!
 
Anakuchapia mkuu
Hahaah huku karatu sidhan kama alishawah kuja huyo jamaa sema basi ule utoto wa kuhusudu wasanii ukizingatia ndio kamemaliza form 4

Ila huyu jamaa alivyo mlaini laini hata nimfungie chumbani wakiwa uchi na demu wangu hawezi fanya lolote
 
Binafsi, jamaa namkubali sana tu.. anajua pia hasa nyimbo zake za sasa kama shukrani na hauwezi kushindana naona kabadilika halambi sana midomo na swaga za ajabu ajabu, zaidi pengine labda waTZ hatuna exposure tu kama unafatilia Gospel za wenzetu hasa wazungu ndio utashangaa kabisa!! the way walivyo mtu mpk anavaa earnings...
 
Back
Top Bottom