Mkuu kuna kitu ambacho naona bado waafrika tunakosea hapo kwenye elimu, mfumo wetu wa elimu umekaa kama script ya movie yaani una muandaa mtu ku digest kile anachofundishwa darasani kwanzia ngazi ya awali mpaka ana maliza chuo na hatimae kwenda kufanya kazi inayohusiana na kile alichofundishwa huko, na sio kumuandaa mtu kutumia kile alichofundishwa darasani kwa ajiri ya kupanua wigo wake kifikra hili kufanya vitu ambavyo ni exptional.
Na ndio maana tunaona nchi kama nigeria,egypt,south africa pamoja na kuwa na idadi kubwa ya wasomi lakini hatuoni innovators wakitoka katika nchi hizo kwa sababu mifumo yetu ya kielimu ina limitations ambazo zina mfanya mtu aconcetrate zaidi na kile anachosomea na ina kuwa ngumu kuwaza beyond ya kile anachosomea.