Saa nazipenda sana na nimezoea kuvaa; huwa ni jambo la mwisho kabla sijatoka chumbani kabla ya kustafutahi na kuelekea kwenye misele. Tangu simu zimeingia, hasa zenye auto update, SINA TENA SAA INAYOFANYA KAZI IPASAVYO. Navaa kama
pambo tu na siwezi kutoka bila kuivaa! Kila zama zina kitabu chake; ni mambo mengi tu yamebadilika kutokana na maendeleo ya teknolojia. Lini mara ya mwisho ulikwenda posta kuchukua au kutuma barua binafsi nje ya zile za kiofisi? Lini ulituma au kupokea TMO? Au lini uliandika au kupokea telegram ya taarifa ya dharula? Labda tuweke uzi wa kukumbushana mitindo mbalimbali ya maisha ambayo sasa imekufa yenyewe tu bila kuzuiliwa. Wenzetu kule kwa wazungu ambako teknolojia nyingi ndiko zinatokea kuna makubwa zaidi; ni wewe uchague likufaalo ulichukue au uliache; yapo magari yasiyo na dereva, unaita taxi kwa mfumo maalumu inakuja inakupeleka utakako; kama wewe ni msela hutaki dada poa, unanunua mdoli full size wa shape unayotaka, anakupapasa, ana joto la binaadamu, ana sauti, atakupa kwa staili zote utakazo. Na kwa wadada hivyohivyo; zipo zana loose, ziko mashine zinapeleka mapigo kwa kasi atakayo mdada n.k; all is about technology; wewe tu!!