Kwanini watu wanavaa saa mbovu/zisizo na majira?

Kwanini watu wanavaa saa mbovu/zisizo na majira?

Raimundo

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2009
Posts
13,415
Reaction score
12,627
Kuna kitu kwa muda sasa nimekuwa nakiona ila nadhani ni kama hali inaongezeka, at least kila watu 3 waliovaa saa, mmoja anakuwa amevaa saa mbovu.

Takwimu inaweza isiwe sahihi lakini nimejikuta niko interested na hii kitu kwa sababu ukiwa kwenye daladala au mwendokasi, kuna vile unaweza kuona jirani yako ana saa ukasema utazame ni saa ngapi badala ya kutoa simu mfukoni, sasa kila ukiangalia unakuta mtu kavaa saa imepozi kabisa na yuko tu sawa.

Sasa najiuliza kwa nini mtu anavaa saa wakati ni mbovu?
 
Ugonjwa wa wengi huu. Nina Seiko yangu ya dhahabu huu mwaka wa nne haifanyi kazi lakini kila siku iko mkononi na kwa mwaka lazima niipeleke kusafishwa kwa sonara. Hata sijui ni kwa nini bado naivaa japo inang'ara kweli kweli na "nice watch" za hapa na pale huwa naambulia [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Saa kwa sasa ni pambo la mkono tu.. wengi hawavai kwa ajili ya kuangalia muda..!
 
Na hii nadhani imekuja baada ya kuwa na hizi simu.
 
Simu INA onesha mda; Ubungo kuna SAA, feri kuna SAA, nyumbani kuna SAA, ofisini kuna SAA ,Posta kuna SAA, kooote ukipita utaona SAA, GARI inasaa, daladala inasaa!....YA MKONONI INATIA UVIVU SANA ndio maana mafundi SAA wengi wamegeuka SHOE SHINER TU
 
Hahaaaa mkuu ni maajabu kudhani saa ya sh 150 ni kwabajiri ya muda.
 
Timepiece yangu bila kufanya kazi siwezi kuivaa naienjoy zaidi inavyofanya kazi ina vimadoido fulani hivi ndani
 
Naona umetumia ile takwimu ya 4:1

Mkuu sijawa exactly, lakini nimejikuta tu nikiona mtu kavaa saa naangalia ni nzima au siyo nzima?

Na unakuta wengi zimesimama.
 
Back
Top Bottom