Kwanini watu wanaogopa kufa?

Bonge moja la somo hili. Kumbe sasa kinachotusumbua ni hofu ya future lakini kiuhalisia kama tungeishi the moment hakuna cha kuogopesha si ndio?
Very interested, kumbe hofu ni kuogopa yajayo ambapo si kweli.
Hofu, hasira , upendo na nk hizi ni njia za asili tu za mwili kupata taarifa kuweza kujilinda na kukabiliana na mazingira tu
 
Hofu, hasira , upendo na nk hizi ni njia za asili tu za mwili kupata taarifa kuweza kujilinda na kukabiliana na mazingira tu
Kuna jamaa wanadai haya yote ni jambo lilelile moja ila mawanda tofauti "dichotomy of the same continuum"
Chuki ni upendo katika mawanda ya chini
Kifo ni uhai katika mawanda ya chini.
 
Kuna jamaa wanadai haya yote ni jambo lilelile moja ila mawanda tofauti "dichotomy of the same continuum"
Chuki ni upendo katika mawanda ya chini
Kifo ni uhai katika mawanda ya chini.
Yeah wana make sense mno bwashee😅
 
terminal rally ipo na inajulikana , kuomba maji ipo kitabibu kabisa kwa baadhi ya watu , pia baadhi ya watu huwa wanajua wanakaribia kufa, hivyo huweza kuwaomba wapendwa wao ,wakalete kitu ili wa siwaone kwenye hiyo hali.
Unayosema ni sahihi, terminal rally hutokea kwa watu wachache zaidi wanaofariki ila ndio story kubwa zaidi kuliko ya wale wengi ambao huwa wanakufa bila terminal rally yoyote.

Hiyo pia ya baadhi ya watu kutotaka kuonwa saa wanakufa ni kawaida duniani kote, cultures nyingine mtu kama hataki kuonwa huwa anaambia watu wazi kabisa wampishe kidogo saa imefika ila sisi nafikiri ni tofauti ndio mtu anatafuta namna ya kuwaondoa watu kwa kutuma vitu.
 
Yeah
 
Mimi nimeshuhudia mtu akitapatapa akaitwa jamaa mtu mzima akashauri apewe maji baada hapo alikufa Sasa nilijiuliza huyo aliyeshauri apewe maji alikuwa anajua au hajui alichokifanya mpaka Leo sijapata jibu.
Huenda hata asingempa bado angekufa tu. Ni vile kwa kuwa hamku-experience upande wa kutokupewa maji ungekuaje ndio maana washauri wa kumpa maji wanakuwa blamed
 
Hii ni stoicism, mawazo waliyokuwa nayo akina Zeno of Citium na kuendelezwa na akina Markus Aurelius na wengine Stoicism (Stanford Encyclopedia of Philosophy).

Ndio tutakufa kama tulivyozaliwa lakini that's not all about life. Na ukipenda kujua maisha yana maana gani, basi yape maana wewe mwenyewe. Bila hivyo utafikiri maisha ni kuzaliwa na kufa basi.
 
Kuna dini zinaambia watu wakifa usiku wa kwanza kaburini watawekwa mtu kati.😀

Nani haogopi kipigo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…