Kwanini watu wanaogopa kufa?

Dah! hii nayo changamoto yaani Mzee wa miaka 70 anaogopa kufa haya ni maajabu.
Miaka 70 mbona Bado sana,tuliokaa na wazee wa 85+,

Kuna bibi jirani hakai ndani peke yake ata kama ni mchana anatoka nje😁
 
Maisha ni matam, ukishayapata ukaelewa maana yake lazima utaogopa kuyapoteza. Utotoni hujui maisha ni nini mpaka uzaliwe ujenge ufahamu.
 
Kwa sababu wanaogopa kufa. Bata wahed!
 
Mkuu heshima yako inaonekana umekula chumvi nyingi inasemekana mtu mzima akikaribia kufa anajua Lakini kwanini uogope wakati unajua lazima urudi ulipotoka me nadhani inabidi kujiandaa maana hakikwepeki.
Kifo kinaogopesha mjomba! Pia kifo kinauma! Fikiria unakufa halafu hutawaona tena wapendwa wako. Fikiria hapo ulipo hujui utakufa kifo cha aina gani! Ni wachache ndiyo wamebahatika kufa kifo cha starehe mfano wakiwa usingizini, nk. Waliobakia ndiyo hawa wamekufa vifo vya mateso mfano kwa kuzama majini, kutekwa na kuuwawa kikatili na wasiojulikana, kufa kwa ajali ya moto, kulipuliwa na mabomu, kuchinjwa na magaidi, nk.
 
hii ya kulipuliwa na bomu mbona kama tamu sana bwashee
 
Issue si kuogopa Kifo, tatizo kubwa ni madhara ya Kifo chako kwa utakaowaacha wakiwa bado wanakitegemea. Mateso yatakayo wapata ndiyo kizungu Mkuti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…