Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,172
Naomba majibu ya kina nipate somo.
mikoa ya pwani mdebwedo wao ilimradi apate ka kikombe ka kahawa na kashata kisha huyooo anaenda kucheza bao mpaka muda wa kula unadhani atataka haki yake kweli? Viongozi waibe wasiibe kwake ni kazi bure.
Mikoa yenye kutaka mabadiliko ni Mara, Mwanza, Kagera, Shinyanga, Kigoma, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, na miji kama Iringa, Ruvuma, na Dar. Kote huko kuna wakazi wenye sifa ya elimu. Iwe ni elimu rasmi (formal education) au isiyo rasmi (informal education). Pale ambapo wakazi wake wana-access na vyombo vya habari, au wengi wao wamekwenda shule, au wamejaliwa kufikiwa kwa wingi na waelimishaji utaona wana mwamko kisiasa. Angalia Zanzibar kwa mfano. Tangu kabla ya uhuru wazanzibar wamekuwa wakijadili mambo ya siasa. Kitendo cha mapinduzi kiliwa-sensitize kisiasa. Matokeo yake unayaona. Hawana mchezo na siasa, wanajua inavyohusikana na maisha yao.
Lakini huku bara mikoa mingi ikifanyiwa brainwashing na TANU na baadaye CCM. Wengi wamepokea dogmatically (bila kuhoji) kila kitu walichosikia toka kwa ccm na serikali yake. Enzi za "zidumu fikra za mwenekiti", na "kidumu cdm" na "chama kushika hatamu (au utamu?)" ziliwalemaza wengi wasifikiri critically. Ziliwajengea utamaduni kuwa siasa ni ccm na kila isemacho. Ujinga huu ndio mtaji mkubwa wa ccm. Hivi sasa yaweza kusemwa kuwa kura za ccm (ukiacha mambo ya uchakachuaji) hutokana na makundi mawili ya wapiga kura: Kundi moja ni la WANUFAIKA WACHACHE ambalo ndio kwa mtazamo wangu ccm yenyewe (nafikiri mnakumbuka ule usemi kwamba ccm ina wenyewe). Hawa ndio WALANCHI.
Kundi la pili ni WAFUATA MKUMBO WASIOFAHAMU KINACHOENDELEA, hawa ndio "the brainwashed mass." Ndio WANANCHI wanaoangamia kwa kukosa maarifa, waimbao nambari wani ni ccm bila kujua kuwa wenzao walishahama kwenye unambari wani wa uzalendo wakaingia kwenye unambari wani wa ULAJI. Ndio mikoa nisiyoitaja. Kazi ya kuelimisha ni kubwa. Laikini lipo tumaini, joto la awareness linapanda kwa kasi.
mkuu kwa hili sikuungi hata kucha achilia mbali mkono, unaposema wameenda Shule kwa maana ya elimu Elimu ipi ?, ya Darasani(vitabu), Mazingira yanayomzunguka Mhusika, Ya kuzaliwa nayo (ya kujua Baya na jema), au ya kusikia, kuona kama hii iliyopo hapa JF? Maana Elimu ni uwanja mpana Fafanua
mkuu kwa hili sikuungi hata kucha achilia mbali mkono, unaposema wameenda Shule kwa maana ya elimu Elimu ipi ?, ya Darasani(vitabu), Mazingira yanayomzunguka Mhusika, Ya kuzaliwa nayo (ya kujua Baya na jema), au ya kusikia, kuona kama hii iliyopo hapa JF? Maana Elimu ni uwanja mpana Fafanua
Nafikiri mkuu hapa vidole viliteleza!Wengi wamepokea dogmatically (bila kuhoji) kila kitu walichosikia toka kwa ccm na serikali yake. Enzi za "zidumu fikra za mwenekiti", na "kidumu cdm" na...
Nafikiri mkuu hapa vidole viliteleza!