Kwanini Watu wa Kaskazini (Kusini na Magharibi kidogo) Wanataka Mabadiliko?

peoples awareness always should have a starting point, then it spreads allover the country!. GOOD idea starts to one person then....
 
mikoa ya pwani mdebwedo wao ilimradi apate ka kikombe ka kahawa na kashata kisha huyooo anaenda kucheza bao mpaka muda wa kula unadhani atataka haki yake kweli? Viongozi waibe wasiibe kwake ni kazi bure.
 
nchi yoyote duniani huwa inahijidi mabadiliko.hata marekani walimwondoa bush kwa kumchagua obama.tanzania ina rasilimali zote za kuwa nchi tayari.shida ni ulafi , kukosa viongozi,ufisadi, na wizi, ubinafsi.wananchi wamechoka na umaskini.viongozi kazi yao ni kuuza mali zetu na kujinufisha wenyewe.
 
mikoa ya pwani mdebwedo wao ilimradi apate ka kikombe ka kahawa na kashata kisha huyooo anaenda kucheza bao mpaka muda wa kula unadhani atataka haki yake kweli? Viongozi waibe wasiibe kwake ni kazi bure.

Haswaaah! Lakini kiukweli jibu la swali hili lina dimension kadhaa za ziada na michezo miwili mitatu yakisiasa chini kwa chini.
 
Nyongeza ya hapo nimaeneo ambayo kuna wasomi kibao hii ina maanisha kuna awareness kwa watu they can reason na kuchukua hatua yenye maana tofauti na huku pwani ambako kuna wacheza viduku kama mkuu wa nchi
 
kusini magharibi siyo kusini Ntwara na Lindi lakini! Mikoa ya wanaotaka mabadiliko ndiyo kwenye lower temperature compared to other places! kwenye baridi watu bongo zao zinachaji zaidi! tazama hata duniani kote, kwenye joto watu wanarelax tu hawafikirii sana mabadiliko zaidi
 
Mikoa yenye kutaka mabadiliko ni Mara, Mwanza, Kagera, Shinyanga, Kigoma, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, na miji kama Iringa, Ruvuma, na Dar. Kote huko kuna wakazi wenye sifa ya elimu. Iwe ni elimu rasmi (formal education) au isiyo rasmi (informal education). Pale ambapo wakazi wake wana-access na vyombo vya habari, au wengi wao wamekwenda shule, au wamejaliwa kufikiwa kwa wingi na waelimishaji utaona wana mwamko kisiasa. Angalia Zanzibar kwa mfano. Tangu kabla ya uhuru wazanzibar wamekuwa wakijadili mambo ya siasa. Kitendo cha mapinduzi kiliwa-sensitize kisiasa. Matokeo yake unayaona. Hawana mchezo na siasa, wanajua inavyohusikana na maisha yao.

Lakini huku bara mikoa mingi ikifanyiwa brainwashing na TANU na baadaye CCM. Wengi wamepokea dogmatically (bila kuhoji) kila kitu walichosikia toka kwa ccm na serikali yake. Enzi za "zidumu fikra za mwenekiti", na "kidumu cdm" na "chama kushika hatamu (au utamu?)" ziliwalemaza wengi wasifikiri critically. Ziliwajengea utamaduni kuwa siasa ni ccm na kila isemacho. Ujinga huu ndio mtaji mkubwa wa ccm. Hivi sasa yaweza kusemwa kuwa kura za ccm (ukiacha mambo ya uchakachuaji) hutokana na makundi mawili ya wapiga kura: Kundi moja ni la WANUFAIKA WACHACHE ambalo ndio kwa mtazamo wangu ccm yenyewe (nafikiri mnakumbuka ule usemi kwamba ccm ina wenyewe). Hawa ndio WALANCHI.

Kundi la pili ni WAFUATA MKUMBO WASIOFAHAMU KINACHOENDELEA, hawa ndio "the brainwashed mass." Ndio WANANCHI wanaoangamia kwa kukosa maarifa, waimbao nambari wani ni ccm bila kujua kuwa wenzao walishahama kwenye unambari wani wa uzalendo wakaingia kwenye unambari wani wa ULAJI. Ndio mikoa nisiyoitaja. Kazi ya kuelimisha ni kubwa. Laikini lipo tumaini, joto la awareness linapanda kwa kasi.
 
mkuu kwa hili sikuungi hata kucha achilia mbali mkono, unaposema wameenda Shule kwa maana ya elimu Elimu ipi ?, ya Darasani(vitabu), Mazingira yanayomzunguka Mhusika, Ya kuzaliwa nayo (ya kujua Baya na jema), au ya kusikia, kuona kama hii iliyopo hapa JF? Maana Elimu ni uwanja mpana Fafanua
 
ndio maana akasema formal na informal education yaani elimu ya darasani na ile isiyokuwa ya darasani
 
mkuu kwa hili sikuungi hata kucha achilia mbali mkono, unaposema wameenda Shule kwa maana ya elimu Elimu ipi ?, ya Darasani(vitabu), Mazingira yanayomzunguka Mhusika, Ya kuzaliwa nayo (ya kujua Baya na jema), au ya kusikia, kuona kama hii iliyopo hapa JF? Maana Elimu ni uwanja mpana Fafanua

Mkuu angalia tena nikilichoandika, nimeandika pia elimu rasmi na isiyo rasmi (formal education na informal edu) pia nimetaja elimu ya kutokana na kufikiwa na waelimishaji na kuwa na access na vyombo vya habari yaani kuwa na "exposure" ya kutosha. Haya yote ni elimu mkuu.
 
Back
Top Bottom