Kosa kubwa ni hili mnalolifanya la kuunganisha kila kitu na siasa za vyama. Naomba muongeze upeo ili mjadili vitu kwa weledi. Kuping akila kitu kunaubaya gani kama vitu ni vibaya?
Mfano:- Tozo za simu, tunajua zinaumiza wananchi, wapige makofi kwa sababu ni wanaccm? Je wanaopinga tozo in wana ccm tu?
Mfano:- Kuhalalisha ufisadi na kudidimiza maisha ya raia wengi kwa kukosa huduma, mikitaba ya ovyo na, kukosa uwajibikaji wa srikali. watu wasipinge kwa sababu gani? Inahitaji chama cha siasa kuona maumivu ya ukosefu wa ajira nchini na mazingira ovyo ya uwekezaji? , ubadhilifu wa mali ya umma kama wale wezi wa wizara ya fedha waliokamatwa halafu kesi ikayeyuka, bila mwendelezo. Watu wkaubaliane na lipi? Kukamatwa ama kupotezewa kwa tuhuma? Au kwa utashi wako wawe wanayumba tu wasiojiamini? Washangilie kukamatwa kwa wezi hao kwa vile serikali iliwakamata na halafu tena washangilie kupotezewa kwa tuhuma kwa vile ni seriklai imepotezea?
Unasema Chanjo hii ni hatari na inahitaji udhibiti wa kitaalam ili kuhakikisha kwamba haitakwa na madhara kwa watumiaji, na kwa kuwa haijapitia michakaoto yote, tusubiri kwanza, na watu wanakuelewa wanakuung amkono, halafu baada ya miezi kadhaa , wewe huyo huyo serikali inasema chanjo chanjweni kwa kuwa nawegine wanachanjwa. Unasema haya bila rejea rekebishi ama rejea samihi, kwamba tulikosea, halafu unataka watu wakuelewe na wakuunge mkono. Hivi hawa watu ni binadamu ama misukule na maroboti?
Ningekuelewa kwamba, wanaopinga ni walisoma shule na wajasiri wa kutaka kuelewa, wasiotaka kufanywa misukule kifkira, hapo ungeeleweka. Lakini ukisema CHADEMA, unapwaya sana. Inaonekana wewe pia una tatizo la uelewa.
UKILETA PUMBA, WENYE AKILI WATAKUPINGA TU, UKILETA MEMA WENYE AKILI WATAKUPONGEZA NA KUKUNG AMKONO HUKU WAKIKUONGEZEA MAARIFA MAPYA.
Hiyo ya kusema kila mtu akiping ajambo la serikali basi ni adui wa ccm, ni upumbavu.
Kusema watanzania wengi siyo kweli sema wanachadema wengi walio mitandaoni wengi wanapinga Kila kitu kinachofanywa na serikali ndo wanapinga uwepo wa police ambao wanawaita policcm.
Wanasahau IGP siyo cheo Cha kisiasa ambacho hata lissu angeweza kugombe