Kwanini Watanzania wengi wanataka IGP Sirro aondolewe? Utendaji wake haufai?

Kosa kubwa ni hili mnalolifanya la kuunganisha kila kitu na siasa za vyama. Naomba muongeze upeo ili mjadili vitu kwa weledi. Kuping akila kitu kunaubaya gani kama vitu ni vibaya?

Mfano:- Tozo za simu, tunajua zinaumiza wananchi, wapige makofi kwa sababu ni wanaccm? Je wanaopinga tozo in wana ccm tu?

Mfano:- Kuhalalisha ufisadi na kudidimiza maisha ya raia wengi kwa kukosa huduma, mikitaba ya ovyo na, kukosa uwajibikaji wa srikali. watu wasipinge kwa sababu gani? Inahitaji chama cha siasa kuona maumivu ya ukosefu wa ajira nchini na mazingira ovyo ya uwekezaji? , ubadhilifu wa mali ya umma kama wale wezi wa wizara ya fedha waliokamatwa halafu kesi ikayeyuka, bila mwendelezo. Watu wkaubaliane na lipi? Kukamatwa ama kupotezewa kwa tuhuma? Au kwa utashi wako wawe wanayumba tu wasiojiamini? Washangilie kukamatwa kwa wezi hao kwa vile serikali iliwakamata na halafu tena washangilie kupotezewa kwa tuhuma kwa vile ni seriklai imepotezea?

Unasema Chanjo hii ni hatari na inahitaji udhibiti wa kitaalam ili kuhakikisha kwamba haitakwa na madhara kwa watumiaji, na kwa kuwa haijapitia michakaoto yote, tusubiri kwanza, na watu wanakuelewa wanakuung amkono, halafu baada ya miezi kadhaa , wewe huyo huyo serikali inasema chanjo chanjweni kwa kuwa nawegine wanachanjwa. Unasema haya bila rejea rekebishi ama rejea samihi, kwamba tulikosea, halafu unataka watu wakuelewe na wakuunge mkono. Hivi hawa watu ni binadamu ama misukule na maroboti?

Ningekuelewa kwamba, wanaopinga ni walisoma shule na wajasiri wa kutaka kuelewa, wasiotaka kufanywa misukule kifkira, hapo ungeeleweka. Lakini ukisema CHADEMA, unapwaya sana. Inaonekana wewe pia una tatizo la uelewa.
UKILETA PUMBA, WENYE AKILI WATAKUPINGA TU, UKILETA MEMA WENYE AKILI WATAKUPONGEZA NA KUKUNG AMKONO HUKU WAKIKUONGEZEA MAARIFA MAPYA.

Hiyo ya kusema kila mtu akiping ajambo la serikali basi ni adui wa ccm, ni upumbavu.
Kusema watanzania wengi siyo kweli sema wanachadema wengi walio mitandaoni wengi wanapinga Kila kitu kinachofanywa na serikali ndo wanapinga uwepo wa police ambao wanawaita policcm.
Wanasahau IGP siyo cheo Cha kisiasa ambacho hata lissu angeweza kugombe
 
Huyo Kaganda mwenyewe mnamharibia maana hicho cheo sio cha kisiasa , na Polisi sio lazima apendwe ,
 
Watanzania wengi? Hao watanzania wengi umewatoa wapi? Nyie chadema vichaa kweli. Sirro ni kati ya ma IGP bora kabisa kuwahi kushika hiyo nafasi Nchini.
 
Anatokea Wapi Ama Yule Aliyepandishwa Vyeo Viwili Haraka Haraka

20210819_093511.jpg
 
Mkuu wa jeshi la polisi ndio msimamzi mkuu wa shughuli za Jeshi hilo kwa kila namna, kuanzia utendaji, nidhamu na hata kufanya kazi kwa misingi ya haki.

Kila kona sasa hivi inaonekana wananchi hawana imani na IGP Sirro.

Je, ameshindwa kusimamia polisi kutenda haki?

Huyu mama Suzan Kaganda ndio atatenda haki?

Malalamiko kwa Sirro ni mengi juu ya kutetea uovu wa askari. Wanasiasa, wakulima na hata wananachi wa kawaida wanalalamika mitaani. Je, ni kweli hafai?

Umepita mitaa mingapi kupata maoni ya Watanzania na kufikia hiyo conclusion yako?
 
Mimi kwa mawazo yangu nashauri Mfumo mzima wa Jeshi la Polisi ufumuliwe na kuundwa upya.
Kutaka Siro aondoke wakati mfumo wa Polisi ni ule ule naona haiwezi kusaidia hata aje IGP yupi!
lakini zaidi ya yote ni mpaka tutakapopata Katiba Mpya.
Jeshi letu la Polisi linafanyakazi vizuri isipokuwa linatumika zaidi kwa maslahi ya Chama tawala badala ya Maslahi ya wananchi hapo ndipo linapoonekana halina weledi katika kufanyakazi zake.
 
Questionnaire dunia ya leo inafanyika kidigital siku hizi. Acha kukariri. Nchi nzima inafikiwa na dodoso kwa dk mbili tu.
Rudi darasani upya. umeshafeli. even in digital way bado sana. even serikali haitumii njia hiyo kupata actual number ya ishu za kijamii.

try again man. umeshafeli
 
Mkuu wa jeshi la polisi ndio msimamzi mkuu wa shughuli za Jeshi hilo kwa kila namna, kuanzia utendaji, nidhamu na hata kufanya kazi kwa misingi ya haki.

Kila kona sasa hivi inaonekana wananchi hawana imani na IGP Sirro.

Je, ameshindwa kusimamia polisi kutenda haki?

Huyu mama Suzan Kaganda ndio atatenda haki?

Malalamiko kwa Sirro ni mengi juu ya kutetea uovu wa askari. Wanasiasa, wakulima na hata wananachi wa kawaida wanalalamika mitaani. Je, ni kweli hafai?
Amehamisha Jeshi la Polisi lote kushughulikia siasa kuwakandamiza CHADEMA kwa kuwabambikizia kesi na kuwatupa mahabusu bila kosa lolote akiacha uhalifu ukiongezeka kwa kasi ya ajabu ikiwa ni pamoja na mauaji ya kutisha. Intelligentsia ya Polisi aliyokuwa anajigamba kuwa na uwezo wa kuwabaini Wapinzani waliokuwa wanafikiria kuandamana ilikuwa wapi "Gaidi" akafanikiwa kuuwa Polisi 4 na wengine kujeruhiwa Mita chache tu toka Kituo cha Polisi mchana kweupe? Polisi wenyewe wamekiri mauaji yameongezeka sana Awamu hii wakisingizia Ushirikina. Jeshi chini ya uongozi wake limepoteza kabisa Imani ya wananchi linatakiwa kufumuliwa kabisa kulipa nguvu na imani mpya.
 
Mimi kwa mawazo yangu nashauri Mfumo mzima wa Jeshi la Polisi ufumuliwe na kuundwa upya.
Kutaka Siro aondoke wakati mfumo wa Polisi ni ule ule naona haiwezi kusaidia hata aje IGP yupi!
lakini zaidi ya yote ni mpaka tutakapopata Katiba Mpya.
Jeshi letu la Polisi linafanyakazi vizuri isipokuwa linatumika zaidi kwa maslahi ya Chama tawala badala ya Maslahi ya wananchi hapo ndipo linapoonekana halina weledi katika kufanyakazi zake.
hilo suala lilishawahi kuongelewa enzi za jpm. kuwa police tz inatakiwa ibadilike kutoka police force to police service. lakin sababu ya siasa muhusika akaonekana ni adui.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom