IGP Simon Sirro apumzishwe

EKILOZO

Member
Jul 16, 2021
23
75
Japo havijaanza leo lakini vitendo vya rushwa, kubambikia kesi na uonevu kwa raia chini ya IGP sirro vimekithiri ukilinganisha na miaka ya nyuma

Kukithiri kwa vitendo hivi ni kiashiria kwamba IGP sirro ameshindwa kudhibiti nidhamu ndani ya jeshi la polisi na hivyo kupelekea utendaji mbovu wa jeshi hilo.

Nje ya kuonea na kumbambikia watu kesi, ndani ya kipindi kifupi, sirro amegeuza jeshi la polisi kutoka kuwa usalama wa raia kuwa adui wa raia ndio maana polisi wakipatwa matatizo ya kifo au kudhurika watu wanashangilia.

Actually, IGP sirro ametengeneza uhasama kati ya polisi na raia kwa sababu ya kufumbia macho vitendo viovu vinavyofanywa na askari wake.

Kama uhasama huu na chuki vitazidi kuenea kwa raia na kufikia kiwango cha juu tutarajie siku zijazo kama kutatokea kikundi au mtu wa aina ya HAMZA anayelenga kutekeleza vitendo vya kigaidi kwa polisi wetu kuungwa mkono na raia na hivyo kuhatarisha usalama na amani ya nchi yetu

Kabla haya hayajatokea maana hatujui huko mbele itakavyokuwa, tunaziomba mamlaka za uteuzi zimpumzishe kamanda sirro ili kutoa nafasi kwa mtu mpya mwenye mawazo mapya atakayeweza kuboresha utendaji wa jeshi letu la polisi kuanzia nidhamu, mafunzo, kudhibiti vitendo vya rushwa na ubambikaji kesi na atakayeweza kuunganisha jeshi la polisi na raia wake kuliko ilivyo sasa.
 
Gerald .M Magembe

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
2,432
2,000
Ukisikia jambazi, gaidi, mwizi, tapeli, na kundi lolote linalo lalamika na linachukia polisi au vyombo vya usalama.

LAZIMA UFAHAMU VYOMBO VYA USALAMA VINAFANYA KAZI VIZURI.

SIRRO SHIKILIA HAPO HAPO, YANAPUMULIA JUU JUU.
 
peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
5,185
2,000
Ukisikia jambazi, gaidi, mwizi, tapeli, na kundi lolote linalo lalamika na linachukia polisi au vyombo vya usalama.

LAZIMA UFAHAMU VYOMBO VYA USALAMA VINAFANYA KAZI VIZURI.

SIRRO SHIKILIA HAPO HAPO, YANAPUMULIA JUU JUU.
 
Attachments

  • File size
    980.3 KB
    Views
    0

Uswiss

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
834
1,000
Kazi yetu ni ngumu sana.. Ngoja siku tususe/tugome ndo mtajua na kuheshimu kazi yetu.. Police wengi ni watu wazuri tu ila wapo wachache wanaofanya wengi waonekane wabaya. Asante
 
MADAXWEYNE

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
1,219
2,000
Kazi yetu ni ngumu sana.. Ngoja siku tususe/tugome ndo mtajua na kuheshimu kazi yetu.. Police wengi ni watu wazuri tu ila wapo wachache wanaofanya wengi waonekane wabaya. Asante
Ni kweli ni ngumu sana ila kwa sasa hivi wengi ni wabaya kuliko wazuri. kwa zama hizi Inapotokea ukamuona polisi ana roho nzuri inabidi ushangae sana yaani ni jambo la kushangaza sana
 
Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
8,568
2,000
Pamoja na watu sampuli ya Sirro kuondolewa pia ni muhimu sana tena sana kwa jeshi la polisi kubadilishwa kutoka kuwa jeshi na kuwa (Huduma ya Polisi Tanzania). (Tanzania Police Services) badala ya Tanzania Police Force.

Polisi inafanya huduma za kijamii hivyo haipaswi kuwa jeshi la kutembea na silaha masaa yote utafikiri nchi iko vitani.

Pia polisi wawe na Public Relations Department ambayo itakuwa inashughulikia mahusiano na jamii pia kitengo hichi kiongozwe na watu wenye weledi na maswala ya sheria na haki za binadamu.

Kwa sasa polisi wa Tanzania wanaweza wakashikilia namba moja duniani kwa kuwaonea raia wao kwa kuwabambikia vyesi feki ili wapate kuhongwa fedha nyingi kabla ya kuachiliwa.

Polisi ktk nchi hii wamekuwa ni kero kiasi kwamba wakipatwa na zahama yoyote kama ya juzi wananchi wengi hushangilia.
 
kirengased

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
4,773
2,000
Igp alikuwaga Said Mermaid, polisi na raia wakaelewana. Huyu sijui anasimamia nini has kiufupi hanaalama yamaana anayoiacha.
 
Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
29,541
2,000
Samahani mkuu....
Hivi ulikuepo enzi za utawala wa Omari Mahita..??
 
EKILOZO

Member
Jul 16, 2021
23
75
Pamoja na watu sampuli ya Sirro kuondolewa pia ni muhimu sana tena sana kwa jeshi la polisi kubadilishwa kutoka kuwa jeshi na kuwa (Huduma ya Polisi Tanzania). (Tanzania Police Services) badala ya Tanzania Police Force.

Polisi inafanya huduma za kijamii hivyo haipaswi kuwa jeshi la kutembea na silaha masaa yote utafikiri nchi iko vitani.

Pia polisi wawe na Public Relations Department ambayo itakuwa inashughulikia mahusiano na jamii pia kitengo hichi kiongozwe na watu wenye weledi na maswala ya sheria na haki za binadamu.

Kwa sasa polisi wa Tanzania wanaweza wakashikilia namba moja duniani kwa kuwaonea raia wao kwa kuwabambikia vyesi feki ili wapate kuhongwa fedha nyingi kabla ya kuachiliwa.

Polisi ktk nchi hii wamekuwa ni kero kiasi kwamba wakipatwa na zahama yoyote kama ya juzi wananchi wengi hushangilia.
Mkuu wangu nakupa kongole kwa hoja yako mujarabu. Natamani wahusika wangeichukua na kuifanyia kazi ili kuboresha utendutendaji kazi wa jeshi letu la polisi. Shukrani sana mkuu
 
Niza doyi

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
2,336
2,000
Usisahau pia kuwa huyu ndo alidhibiti utekwaji magari,
Alidhibiti mauaji ya albino,
Alidhibiti ujambazi ,wakati wa utawala wake Mwendazake.

Alidhibiti jiji kuchomwa Moto akiwa RPC Mwanza,pale CHADEMA walioona kulikuwa na dalili za kuchakachuliwa matokeo.

Mtoeni tu wekeni wa kwenu.
 
Isakhamisi

Senior Member
Sep 5, 2019
132
250
Japo havijaanza leo lakini vitendo vya rushwa, kubambikia kesi na uonevu kwa raia chini ya IGP sirro vimekithiri ukilinganisha na miaka ya nyuma

Kukithiri kwa vitendo hivi ni kiashiria kwamba IGP sirro ameshindwa kudhibiti nidhamu ndani ya jeshi la polisi na hivyo kupelekea utendaji mbovu wa jeshi hilo.

Nje ya kuonea na kumbambikia watu kesi, ndani ya kipindi kifupi, sirro amegeuza jeshi la polisi kutoka kuwa usalama wa raia kuwa adui wa raia ndio maana polisi wakipatwa matatizo ya kifo au kudhurika watu wanashangilia.

Actually, IGP sirro ametengeneza uhasama kati ya polisi na raia kwa sababu ya kufumbia macho vitendo viovu vinavyofanywa na askari wake.

Kama uhasama huu na chuki vitazidi kuenea kwa raia na kufikia kiwango cha juu tutarajie siku zijazo kama kutatokea kikundi au mtu wa aina ya HAMZA anayelenga kutekeleza vitendo vya kigaidi kwa polisi wetu kuungwa mkono na raia na hivyo kuhatarisha usalama na amani ya nchi yetu

Kabla haya hayajatokea maana hatujui huko mbele itakavyokuwa, tunaziomba mamlaka za uteuzi zimpumzishe kamanda sirro ili kutoa nafasi kwa mtu mpya mwenye mawazo mapya atakayeweza kuboresha utendaji wa jeshi letu la polisi kuanzia nidhamu, mafunzo, kudhibiti vitendo vya rushwa na ubambikaji kesi na atakayeweza kuunganisha jeshi la polisi na raia wake kuliko ilivyo sasa.
Sirro lazima apumzishwe kachoka mfano baada ya mauwaji ya mapolisi wetu kabla hata uchunguzi haujaanza sirro moja kwa moja alimuuhusisha muuwaji hamza na kuweko kwa askari wetu msumbiji ni kosa kubwa sana kitaalamu.
 
EKILOZO

Member
Jul 16, 2021
23
75
Samahani mkuu....
Hivi ulikuepo enzi za utawala wa Omari Mahita..??
Nilikuwepo mkuu...

Lakini ubovu wa mahita sio kilele cha kuhalilisha utendaji kazi mbovu wa jeshi letu la polisi

ndio maana tuna shauri sirro aliyeamua kufuata nyendo za mahita naye apumzishwe awekwe mtu mwingine atakayeenda kuziba makando kando yote yanayolichafua jeshi letu kwa sasa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom