Kwanini Watanzania wengi ni wabishi?

MFALME WETU

JF-Expert Member
Feb 1, 2021
2,586
6,168
Hello,

Zamani nilikua najua watu wafupi au ndugu zetu wa upareni, Tanga, Morogoro na Kigoma ndo wabishi tu kumbe nilijidanganya.

Sasa nimekuja kugundua wabongo wengi tuna hulka ya ubishi, sio wanaume sio wanawake, sio vijana sio wazee, sio warefu sio wafupi, sio mtandaoni sio kwenye maisha halisi yani ni patashika!!

Leo hapa kuna mteja nimetoka kumfanyia delivery ya simu nikamwambia ni waterproof kama haamini alete maji tutest ikiharibika ntamfanyia return akagoma katakata!

Huyo ni mfano tu maana wabongo wengi wanaomiliki izi simu za waterproof kama iPhones, Samsung, Sony n.k kuliko kutumia izo simu kwenye maji mfano beach au swimming pool bora uwauwe 😅

Jobless ni kawaida sana kuwakuta wanabishana ila sikuizi tabia imeambukizwa hadi kwa baadhi ya waajiriwa na wafanyabiashara. imefikia hatua watumishi wanabishana mpaka muda wa kazi bila wasiwasi wowote.

Juzi kuna duka nilienda kununua maji nikakuta muuzaji hayupo kwa vile ninamjua nikajaribu kuangaza kumbe yupo kwenye magazeti wanabishana kuhusu Simba na Yanga.

Sasa ukifuatilia ubishani wao utabaki tu unashangaa, vitu vya ajabu.

Kuna wengine unajitolea kuwapa connection au fursa ya kazi sehemu wanahisi ni scam mwishowe unaamua kuachana nao.

Nilikua napenda kujua kwanini % kubwa ya sisi wabongo ni wabishi sana kitu kinachopeleka mpaka wengine kupigana, ndio asili yetu au Kuna shida Mahala?
 
Jaribu pia kufanya kautafiti na Marekani na nchi zingine, huenda ukaja na hitimisho zuri kuhusu hulka ya mwanadamu.
 
Utafiti wangu hauitaji gharama
Ni kweli. Mtanzania kwa ubishi ndiyo mwenyewe. Ni ulimbukeni na elimu ndogo. Msomi mzuri hupenda kusikiliza. Sasa taizp letu ni kwa watu wanamaliza chuo kikuu na kichwani hakuna kitu hivyo hujaribu kuonyesha kuwa anajua kwa kubisha.
 
Wanakuja wanaotafuta connection na fursa za kazi!
Sema tangazo lako limekaa kitaalam sana!
ubishi wenyewe naozungumzia ndo huu

Mimi nimetoa mfano kulingana na thread yangu, wewe mbongo na ubishi wako ushafikiria kwingine? huoni ata pm yangu imefungwa?

Hopeless
 
CCM ndio sababu.

Tumetengenezewa mfumo wa kuwa kama "Nyumbu".

Yaani imefika mahali wema sepetu anaweza kubadili upepo wa nchi kwa scendo,mambo ya msingi hayana wachangiaji,mambo ya kipuuzi ndio wengi wanapelekwa na mafuriko.

Mimi nadhani sio wabishi,tumekuwa wajinga,na hatujui kama ni wajinga.

Nchi iliokosa utawala bora,umeme wa uhakika,maji ya uhakika,miundombinu ya kueleweka na mengine mengi.

Yule aliesema mwenge wa Uhuru unapumbaza akili zetu inawezekana
 
sababu ni ufinyu wa maarifa na taarifa na exposure

watanzania wengi tunajua vitu kwa juu juu sana yani tunapewa headlines tu ya mambo kuanzia kielimu mpaka kifamilia.
 
Back
Top Bottom