Kwanini Watanzania wengi hawapendi kucheza na kuwajali wanyama wanaowafuga?

1. Tz watu wengi hawana disposable income(kipato-kodi) kubwa, tunasikia watu wengi wanaishi chini ya dola 5, dola 1 moja kwa siku. Kutunza mnyama ni jukumu na lina gharama zake, wenzetu mambele wana disposable income kubwa kwahiyo wana uwezo wa kutunza mifugo vizuri.... sio kuwalisha makombo.

2. Tuna tamaduni ya kuhusisha mifugo na uchafu, unakuta mtu hataki kugusa mbwa anaona kinyaa, hii ipo kwa watu wengi.... yaani pets na livestock sisi tunaona ni kama pests

3. Tusichokijua ni kwamba ukiishi na mnyama yeyote kuanzia akiwa kachanga, kuna biological process inaitwa imprinting, yaani anabond na wewe anakuona kama kiongozi/mzazi.... mahusiano kati ya binadamu na wanyama yanawezekana.

4. Kulingana na point ya 3, wabongo tushazoea kila mnyama ana kazi yake, ukiachana na wanaoliwa, mbwa ni wa ulinzi, paka wa kufukuza panya.... mambele kuna livestock, wanafugwa ili waliwe... na kuna pets, wanafugwa ilimradi tu kama company
Namba 3 ni very true na ushahidi ninao miaka fulani mbwa wangu alishawahi kuniokoa kwenye issue ya hatari sana kwa kuja kunishtua kwa hali ya kitofauti ambayo sikuizoea kabla.

Pia nimefuga mbuzi na ng'ombe hawa nilicheza nao kiasi hata nilipokuwa nikiingia nyumbani nikifungua geti shingo zote kama wanataka kutoka bandani kunikimbilia mbuzi na ng'ombe wote japo hawakuwa wengi niliwapa majina na walikua wanayajua nikiwaita unaona response burudani kubwa niliipata kwa mbuzi kwa michezo michezo ya kukimbizana pale nikiwa free na kuruka wanavyoruka.

Hadi leo mtu nikiona anapiga mnyama sifurahii kabisa.
 
Tanzania wanyama tunaoishi nao wanateseka sana kwakweli, ni kama vile waliumbwa na shetani wakati tumeumbwa nao na Muumba wetu alietupa mamlaka tumsaidie kuwatunza, Watanzania tunasali sana na kuomba dua ila ya nini hivi vyote kama hatupo tayari kuukubali uumbaji wa viumbe vingine vilivyoumbwa na Baba wa mbinguni / Allah?

Ni mwaka unaisha sasa paka wako hujawahi hata kumpa zawadi ya samaki mzima.

Ni mwaka unaisha sasa mbwa wako hujawahi kwenda buchani umnunulie kilo ya nyama umchomee ama umchemshie.

Mbuzi ama kuku umemnunua wa kumchinja, yafaa umtendee haki walau kwenye safari yake ya mwisho umuandali malazi safi, chakula na maji viwepo, kisha kesho yake umchinje, si sawa apigwe na mvua ama upepo wa el nino, chakula umbanie na maji anywe kwenye vyombo vichafu kisha kwa unafki eti umuombe Mungu kabla ya kumchinja.

Paka ama mbwa kakuzoea hujawahi hata kukaa nae sehemu kumpeti peti, akija unamwambia tokaa, yupo kwao tayari aende wapi?

Mbwa wako kakuzoea hujawahi hata kucheza nae michezo ya kukimbizana ama mpira

Mbwa yumo kwenye banda kila siku, hujawai kutembea nae hata siku moja jioni
Duh
Ana hoja, asikilizwe
 
Nchi yetu ingekuwa serious na sheria, watu wengi sana wangefungwa jela kwakuwa ipo,animal welfare act inayosimamia yote aliyoandika mdau ikiwemo chakula na malazi ya wanyama.
 
Kuna ile kauli "lete jiwe...lete jiwe"

Binafsi napenda pets, hasa mbwa, ni company nzuri lakini pia ni mlinzi mzuri wa nyumba na master wake pia.
 
Jana tu nlikuwa nmekaa sehemu,ghafla mbws akapita zake,jamaa akaokota bonge la jiwe anataka kumrushia,hadi nikamzuia..Its so sad,na hali hii ni kubwa sana mitaani kwetu. Wanyama hasa mbwa na paka wanateseka sana aisee!
 
Tanzania wanyama tunaoishi nao wanateseka sana kwakweli, ni kama vile waliumbwa na shetani wakati tumeumbwa nao na Muumba wetu alietupa mamlaka tumsaidie kuwatunza, Watanzania tunasali sana na kuomba dua ila ya nini hivi vyote kama hatupo tayari kuukubali uumbaji wa viumbe vingine vilivyoumbwa na Baba wa mbinguni / Allah?

Ni mwaka unaisha sasa paka wako hujawahi hata kumpa zawadi ya samaki mzima.

Ni mwaka unaisha sasa mbwa wako hujawahi kwenda buchani umnunulie kilo ya nyama umchomee ama umchemshie.

Mbuzi ama kuku umemnunua wa kumchinja, yafaa umtendee haki walau kwenye safari yake ya mwisho umuandali malazi safi, chakula na maji viwepo, kisha kesho yake umchinje, si sawa apigwe na mvua ama upepo wa el nino, chakula umbanie na maji anywe kwenye vyombo vichafu kisha kwa unafki eti umuombe Mungu kabla ya kumchinja.

Paka ama mbwa kakuzoea hujawahi hata kukaa nae sehemu kumpeti peti, akija unamwambia tokaa, yupo kwao tayari aende wapi?

Mbwa wako kakuzoea hujawahi hata kucheza nae michezo ya kukimbizana ama mpira

Mbwa yumo kwenye banda kila siku, hujawai kutembea nae hata siku moja jioni
Maskini tangu lini akawa na upendo yeye mwenyewe hajipendi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom