Kwanini Watanzania mnapotoshwa kirahisi na Lowassa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Watanzania mnapotoshwa kirahisi na Lowassa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Synthesizer, Nov 27, 2011.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2011
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,128
  Trophy Points: 280
  Siamini masikio wala macho yangu. Watanzania tuna tatizo gani? Lowasa anawapotosha kirahisi namna hii?!? Jamani, mbona mnasahau kirahisi issue iliyomtoa Lowasa Uwaziri Mkuu ni mazingira ya rushwa kupitisha mradi wa Richmond? Hata kama ni kweli alimpigia simu JK kusema wavunje mkataba wa Richmond, haifuti ukweli kwama alipitisha Richmond kwa nguvu katika mazingira ya kifisadi. Hilo ndio hatia yake, na hilo ndilo kamati ya Mwakyembe ililiona na kulisema. Lowasa si mjinga, nahisi alipiga hiyo simu kumtega JK na kujilinda baadaye mambo yakigeuka, akijua wazi walifanya jambo la ufisadi Richmond! Yaani mnadhani Lowasa hakujua wahusika wa Richmond?

  Lowasa kawatega, amechukua kakipengele kadogo katika suala la Richmond na wote mkakimbilia huko na kusahau lililo kubwa katika mkataba wa Richmond. Jamani, jamani, jamani, be smart!!!

  Hivi kweli kwa kauli moja ya Lowasa basi leo mnaona yale yote yaliyo kwenye taarifa ya Kamati ya Mwakyembe hayafai tena?

  Hivi mnamjua Lowassa nyie? Ulizeni watu waliofanya naye kazi akiwa Waziri Wizara ya Ardhi, hadi ikafikia Mtanzania mhindi kusema Lowasa ananuka rushwa! Mhindi kukutuhumu unanuka rushwa, yaani wewe ndio basi tena, maana ana taarifa zote za rushwa wanazotoa wahindi wenzake! Hivi mmesahau Lowasa alituhumiwa nini na Nyerere katika kugombea uraisi hata akafukuzwa toka ukumbini kama mtoto mdogo?

  Jamani kweli nawasikitikia Watanzania. Wasahaulifu mno!
   
 2. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hili ndilo tatizo la kufikiri kwa masaburi! Yaani wewe ndio unajiona unajua sana kuhusu Richmond? Kuna lipi jipya ambalo halijasemwa kama sio kauli ya EL ya juzi. Sitaki ban TU LAKINI ningekupa vidonge vyako hapa
   
 3. e

  emalau JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2011
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Stop talking about people, talk about issues Jf has already been flooded with Lowasa let's talk something else
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  katika ccm mtu msafi ni mmoja tu nae ni edward ngoyai lowasa.kashfa ya richmond alitolewa kafara tu aliyeiingiza richmond nchini ni samweli sita wakati huo akiwa anaongoza kitengo cha uwekezaji alicho nacho emanuel naiko kwa sasa.
  lowasa alijiuzulu akadai kisa ni uwaziri mkuu,wenye akili tunajua ishu ya makundi ndiyo iliyomhukumu lowasa.kamati yote ya bunge haina ujasiri tena kwa sababu wanajua walizungukwa wakaenda kichwakichwa na wakiambiwa warudie tena watakuja na majibu tofauti.
  mwakyembe alisema kuna mabo waliacha kwa sababu serikali ingevunjika,sasa jiulize kama waziri mkuu ameshajiuzulu ni nani tena yuko juu yake ili serikali ivunjike?
  wenye richmond wanajulikana na lowasa keshawataja.
  ccm 2015 ikmsimamisha lowasa mimi na familia yangu tutakuwa wa kwanza kuipigia ccm kura.
  naomba mwenye ushahidi wa ufisadi wa lowasa auweke hapa tofauti na hapo ni majungu tu.
   
 5. s

  shukia Member

  #5
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inakatisha tamaa kuona watu wanghiribika kirahisi na kusahau hoja za msingi. El, kwa maoni yangu si mtu safi, anajikosha kwa wa TZ kwa kusema kwamba yeye haijui Richmond na alimpigia simu JK. La kupiga simu si hoja ya maana sana. Kama aliona kuna tatizo baada ya kupiga simu kwani kungetokea nini kama angejiuzuru kwa sababu kuwa yeye ni mzalendo na ameona mambo ambayo hakubaliani nayo. Kwa hilo ningempongeza. Kwa ujumla wake, hasa kwa wale wenye kufikiri na kuchambua mambo kisawasawa, El is not a clean person.
   
 6. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  umefanya utafiti kujua ni watz wangapi wamemsamehe lowassa?
   
 7. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2011
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,128
  Trophy Points: 280
  Raia Fulani, tathmini yangu inatokana na jinsi kwa ghafla sana naona maoni mengi kwenye JF ni ya kumuunga mkono EL. Najua wapo Watanzania wengi tu ambao hawawezi kudanganyika kirahisi, kama wewe na mimi na yule. Ukweli naanza kuhizi EL amepandikiza watu wake humu JF ili kupiga propaganda za bei rahisi!
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Nov 27, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280

  mkuu umetumia nguvu nyingi sana,

  huwezi kumtofautisha lowasa na JK kwenye issue ya richmond! labda kama una matatizo ya akili,,,kwa nini anatamkwa EL peke yake..wakati CCM yako wote ni wezi???

  Kingine Nyerere sio standard acha kujiaibisha....Nyerere ndiye aliyesema Mkapa Mr. Clean unajua Mkapa kafanya nini ikulu?

  wezi wote waende jela...ama sivyo ni jirani na ndugu zetu, ukifikiri sana utagundua tatizo sio hao wezi..ila wanaotakiwa kuwachukulia hatua hao wezi......hili lingekuwepo hakuna ambaye angepona

  in other words stop talking about EL....talk about how we can punish mafisadi!!!
   
 9. twatwatwa

  twatwatwa JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 2,036
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  wewe ni wakupimwa akili
   
 10. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,993
  Likes Received: 1,001
  Trophy Points: 280
  You are deluded...Ndio maana unakuja na hoja za kuzalimisha, hata uletewe ushahidi wa aina gani bado hauwezi kukubadilisha msimamo wako dhidi ya Lowassa, maybe after psychiatric help
   
 11. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2011
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
   
 12. J

  Joseph Peter Member

  #12
  Nov 27, 2011
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna kijana mmoja aliwahi kusema kumsafisha LOWASA ni sawa na kupiga rangi upepo.
   
 13. J

  Joseph Peter Member

  #13
  Nov 27, 2011
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali watu wana fanya kazi kwa maandishi kama yeye FISADI Lowasa alivyo fanya kwa vi-memo vya ufisadi wa Rich Monduli. Alimpigia simu JK kwani bwana yake? Si angeandika document aka-scan na kumtumia? Aache utaahira huyu Mr. Zero.
   
 14. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #14
  Nov 27, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  ukimhukumu lowassa then wahukumu ccm wote, ukimuacha lowassa then waache wote, yeye ni kingpin yuko kwenye system anaelewa move zote cha kumfanya ni ku mkolimba tuu otherwise let him be!
   
 15. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #15
  Nov 27, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  du EL kawajaza si mchezo. wakati wa kampeni 2015 maneno machache yatasemwa. NYERERE ALIMKATAA EL HAFAI KATU
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Nov 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Usiwalaumu bure ndugu zako - NJAA.. Kama Bush aliyekuwa akilaaniwa dunia nzima alipokelewa Tanzania kwa shangwe ambazo hajawahi kuzipata mahala popote duniani ktk utawala wake WOTE.. Unafikiri hawa watu wazima kweli? Mwenye njaa mpe kipande cha samaki ashibe leo ya kesho yatajulikana - Mungu akipenda..
   
 17. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #17
  Nov 27, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa ndipo ninaposhindwa kuwaelewa ndugu zangu wa Nchi hii pale unapokosa namna ya kujenga hoja halafu unaanza kuwalaumu Watanzania inashangaza sana pale unaposema eti Watanzania wanapotoshwa kirahisi halafu wewe unajitoa humo kwamba wewe ni zaidi ya hao Watanzania ni kwa nini nawe pia usifikiri kuwa kwa hilo unaloliamini nawe pia umepotoka ni kwa nini utake kuonekana kwamba wewe ndiye uliye sawa kuliko Mtanzania mwingine yeyote awaye!

  Mi nadhani busara ni kutumia nafasi yako kujenga hoja yako ni si kuwashawishi Watanzania au kuwalazimisha kuwa hawaki sawa ila wewe ndiye uliye sawa hii ni dharau ya ajabu. Wapo wanao amino na watazidi kuamini kuwa Liwassa is of no problem na wengine hawataamini hivyo sasa usiwe kama Litmus paper acha fikra zitofautiane wewe huwezi kuwa bora mpaka kufikia hatua ya kudhani kuwa Watanzania wote wanapotoka eti kisa wanamtetea Lowassa nenda mbele zaidi wapo waliodhani yale ya Richmond yalikuwa ya kweli per se ila juzi wamethibitishiwa ukweli pasipo shaka sasa sababu ni ipi wao wasibadili mitizamo yao!!!!! Tujaribu kupunguza UDIKTETA wa fikra na mawazo tuishi tukijua hata wengine wana uhuru wa kufikiria kama watu wengine......
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Nov 27, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,465
  Trophy Points: 280
  Sisi sote ni binadamu, kwenye ubinadamu, hakuna mkamilifu. No one is perfect!.

  Lowasa kamtubia Mungu dhambi zake, kasamehewa na sasa yeye ndie Chaguo la Mungu kwa mwaka 2015 ili litimie lile neno yasemavyo maandiko
  "rais wa 2015 atatoka Kaskazini!.
   
 19. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #19
  Nov 27, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hivi ni kwanini mti wenye matunda ndio hurushiwa mawe????
   
 20. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #20
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Mungu ni Mwema.
   
Loading...