future lawyer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2020
- 404
- 388
Habari za siku wanajamvi,
Natumai nyote wazima wa afya. Niende moja kwa moja kwenye mada.
Kumekuwa na chuki inayosambaa kwa spidi ya 5G baina ya tabaka lenye elimu "waliosoma" na tabaka wasio na elimu "darasa la 7 " . Kwenye haya matabaka kila moja linajinasibu kuwa bora kuliko lenzie katika nyanja za kimaisha.
Mimi ni kijana nimebahatika kupata degree, baada ya kumaliza chuo Kama mjuavyo Kuna uhaba wa ajira "hakuna kabisa " nimesota kitaa bila matumaini nikachukua maamuzi ya kuendesha bodaboda. Tangu niingie kwenye hii fani nimekuwa nikisemwa vibaya na watu wa Std vii .
Nilichogundua ni kwamba watu "std vii" wanatuchukia sana tulio na elimu zetu wanajifariji kwa maneno yao Kama vile: Elimu yako imekufikisha wapi, una_degree unafanya bodaboda n.k. Kingine wao ndio wanajiona wajanja wanajua kila kitu kuliko wenye degree "sisi washamba hatujui bata wala maisha". Niliona uzi wa mdau humu akilalamika jamaa yake anamsema vibaya kwa watu kuwa ana degree lakini bodaboda.
Nataka nitoe rai kuwa na degree sio dhambi na sio kipimo cha mafanikio Bali ni kipimo cha elimu tu .
ACHENI WIVU ATA HUMU MPO NA NINAWAJUA