Kwa hali na Changamoto za dunia ya Sasa katika ajira, Kuna umuhimu mkubwa sana kupata elimu katika vyuo vya nje

Parabora

JF-Expert Member
Jul 6, 2019
1,504
2,180
Huku bado lock-down inaendelea wakuu japo Cha kushukuru ni maambukizi mapya yamepungua sana na huenda masharti yakalegezwa siku za hivi karibuni, lakini kipindi hiki ambacho hatuna ratiba nyingine nimeamua tuwe tunajadili mambo muhimu na yenye afya kwa vijana wenzangu.

Leo tujadili hasa umuhimu wa kupata elimu ya chuo nje ya nchi. Hapa naomba niweke wazi sina uzoefu na elimu inayotolewa na vyuo vya huko nyumbani na hivyo sijui ubora wake kabisa japokuwa nina marafiki wengi niliosoma nao ambao wamesoma huko, lakini kwa kutumia tu elimu ile ya O'level na Advance ambayo practical tulifanya miezi ya karibu kabisa na mitihani na kupitia marafiki zangu ambao tumesoma kozi sawa inanifanya niamini kabisa hata elimu ya chuo kutakuwa na tatzo .

Katika dunia hii ya changamoto za ajira elimu inayotakiwa ni ya maarifa zaidi kuliko theory, kwa mzazi aliye na uwezo na anahitaji kuandaa future nzuri ya mwanae basi elimu ya nje haiepukiki hasa kwa ngazi ya degree kuliko masters na hata kwa wasio na uwezo nadhani taasisi mbalimbali bado zinatoa ufadhiri changamoto ni ufaulu na wengi hawana taarifa muhimu kuhusu fadhiri hizi na kiukweli hizi taarifa zingetakiwa ziwe zinatolewa mashuleni hasa kwa form5 & 6.

Elimu ya nje haswa kwenye vyuo bora (tuelewane hapa sizungumzii vyuo vya uchochoroni) degree tu inakutosha kufanya mambo makubwa na itakufanya kuwa comfortable kujitegemea na sio kutegemeana support ya familia baada ya kuhitimu.

Mazingira ya vyuo vya nje ni bora sana, Vifaa vya kujifunzia vipo vya kutosha, unapata elimu haswa na mkienda field mnakutana na wanafunzi wengine wa vyuo tofauti kwenye taasisi mliyoenda na chuo kinasubiri majibu kutoka uongozi wa hiyo taasisi kuhusu ufanisi wa wanafunzi wake, mkifanya vibaya mnashusha hadhi ya chuo kwenye masoko ya ajira na hili linapelekea wanafunzi husika msizingatiwe katika fursa mbalimbali na uongozi wa chuo baada ya kupata majibu otherwise muoneshe ku-improve zaidi na hapa hamna ujanja ujanja report inatumwa chuo kulingana na uwezo ulioonesha

Kabla sijaeleza kwa nini unatakiwa usome nje degree ya kwanza hebu tuangalie huu mfano halisi, Kuna rafiki yangu amesoma udsm Telecommunication Engineering na mwingine kasoma mbeya sijui chuo gani kozi ya computer engineering hizi ni moja kati ya fani muhimu sana katika ulimwengu wa leo, hawa ni rafiki zangu kabisa wa tangu utotoni na mpaka Sasa Wana miaka 6 hawana ajira tangu wamalize, tuko karibu sana kimawasiliano na kila nikiongea nao pamoja na kwamba hawana ajira na umri uko 30+ malengo yao ni watafte pesa wakasome masters hukohuko nchini, hapa nilishangaa inakuaje mtu elimu yako ya mwanzo hujaitumia hata robo then utake kuongeza nyingine huku mataifa ya wenzetu ni vigumu kukuta mtu anasoma mfululizo Kama hana mpango wa kuwa mhadhiri au professor na hufika kwenye level hizo za uprofesor wakiwa na umri wa miaka (28-35), Elimu ya degrees ndio walizo nazo ma-professional wengi kwenye makampuni makubwa ya kimataifa ambayo nimebahatika kuyafahamu ama kufanyia kazi na wanafanya makubwa sana kazini pia huwa wanaongezea vikozi vidogovidogo vinavyohusu fani yao tu.

Jana usiku nimeongea nao tena Hawa rafiki zangu wananiambia wamepata temple miezi miwili iliyopita taasisi ya umma na wanalipwa Tsh 150,000/= kwa mwezi, wakuu hapa nikashindwa kuelewa kabisa inakuaje mtu aliye na computer engineering tena degree akajitolee tena baada ya kukaa 6yrs bila ajira, nini vyuo vya huko wanafundisha hasa kwenye hizi kozi mpaka Hawa vijana washindwe kabisa kutumia fani yao katika teknolojia vizuri?

Na hapa ndio unaona umuhimu wa kusoma katika vyuo bora vya nje, Kama ni ajira zinakufata kipindi wewe huna mda nazo, ukisoma nje unajiunganisha na Dunia waajiri wengi wa kimataifa huajiri vijana wenye elimu nzuri na zisizo na mashaka kutoka vyuo bora vya kimataifa nilipokuwa Ghent University kila msimu wa kumaliza kwenye notice board unakuta zimebandikwa nafasi za kazi mbalimbali kutoka kampuni nyingi za kimataifa zinataka vijana wanaotoka hapo chuoni wakafanye kazi kwenye kampuni zao ama zinapitia kwenye uongozi wa chuo direct ambao kazi yao inakuwa ni kuchagua vijana mahiri kwenye fani husika baada ya kumaliza wanapewa barua za ajira tu wanaenda kuanza kazi.

Pia ukisoma vyuo bora vya nje utaweza kumudu changamoto mpya za maisha za nchi zingine ambazo zitakufanya uijue dunia vizuri, kupata fursa kimataifa, kujifunza lugha za kimataifa, kutengeneza mtandao wa urafiki duniani na hapa vijana wengi wa Ghana, Nigeria na Kenya wametuzidi sana wako wengi huku nje wanasoma, wamewekeza ama wanafanya kazi.

Ukipata elimu bora haijalishi umesomea nini utatoka na maarifa bora kabisa na uwanja mpana wa kujiajiri ama kuajiriwa kimataifa

wewe mzazi Kama una uwezo peleka mwanao akasome chuo nje na hakikisha ameenda chuo kizuri na aende asome haswa na wadogo zangu form5 na 6 huu ndio mda wa kutafuta taarifa za ufadhiri sio kutumia mda mwingi kuwaza MAPENZI .

Karibuni kwenye mjadala
Parabora
Geneva -Switzerland

Chukua hatua stahiki, Corona ipo na ni hitari
 
Hili unalosema ni kweli elimu yetu inampumbaza mtoto zaidi kuliko kumtengeneza ajiamini katika kupambana na maisha.
Kijana akishakosa ajira za ndani anakuawa hana plan nyingine na kibaya zaidi hana uwezo wa kushindania ajira za kimataifa, ni muoga, hajiamini hata kujieleza tu anashindwa

Mimi najichanga pensheni yangu nimsomeshe mwanagu ng'ambo kwa kweli
 
Nina wasiwasi kama kweli umesoma, tatizo ni ajira au aina ya elimu? Suluhisho lako naona halitoi jawabu ila ni jibu
 
  • Thanks
Reactions: o_2
Mkuu ungetupa na connection yakupata ufadhili ili uwe umetoa na solution ya tatizo.
Hapa nchini elimu ni kichefu chefu tu unakuta mtu kaaoma coz tofauti na anaenda ajiriwa kwenye fani ya mtu mwingine
 
Nilipomaliza Form Six nikaenda kuchukua degee south africa niliporudi nyumbani nikaanzisha shamba la miti wakaanza kunishangaa ndugu na wazazi badae nikaanzisha kilimo cha ndizi, na Parachichi wakazidi kunishangaa nikachimba bwawa la samaki na leo kila mtu anaelewa nilichokuwa nakifanya.

Mwaka 2018 nilivuna miti na kupata mil 200+ navuna ndizi kwa wiki fuso moja, na parachichi fuso moja. samaki navuna samaki elf50 kwa miezi 3 nashukuru wazazi wameshaelewa na mambo yanaenda kama nalivyo panga.

Nilichokigundua unapnsoma nje unakuwa na uwezo mkubwa wa kujiamini na kuchukua hatua na ku-face changamoto nimesoma na wanaigeria na wagana jamaa wako vizuri kwenye kijiamini na kuchukua hatua. Mfumo wetu wa elimu ni wa hovyo sana lazima tukubali kwanza. Tunapopiga kelele tunajua kabisa nini kinaendelea kwenye mfumo wetu wa elimu.
 
Nina wasiwasi kama kweli umesoma, tatizo ni ajira au aina ya elimu? Suluhisho lako naona halitoi jawabu ila ni jibu
Mkuu ndio sijasoma, basi eleza wapi panaonesha mapungufu yangu na nini kifanyike?
 
Nilipomaliza Form Six nikaenda kuchukua degee south africa niliporudi nyumbani nikaanzisha shamba la miti wakaanza kunishangaa ndugu na wazazi badae nikaanzisha kilimo cha ndizi, na avokado wakazidi kunishangaa nikachimba bwawa la samaki na leo kila mtu anaelewa nilichokuwa nakifanya
Big up, haya ndio maarifa tunayosema
 
Mkuu ungetupa na connection yakupata ufadhili ili uwe umetoa na solution ya tatizo.
Hapa nchini elimu ni kichefu chefu tu unakuta mtu kaaoma coz tofauti na anaenda ajiriwa kwenye fani ya mtu mwingine
Nitafanya hivo mkuu nikiziona
 
Hili unalosema ni kweli elimu yetu inampumbaza mtoto zaidi kuliko kumtengeneza ajiamini katika kupambana na maisha.
Kijana akishakosa ajira za ndani anakuawa hana plan nyingine na kibaya zaidi hana uwezo wa kushindania ajira za kimataifa, ni muoga, hajiamini hata kujieleza tu anashindwa

Mimi najichanga pensheni yangu nimsomeshe mwanagu ng'ambo kwa kweli
Hutojuta mama Kama kijana akiwa anajielewa
 
Back
Top Bottom