Kwanini wasifu wa marehemu waliohama CCM na kisha kurudi huwa hawaandiki historia ya vyama pinzani walivyohamia?

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Leo nimesikiliza wasifu wa Edward Lowassa, ni wazi kabisa wameruka historia ya yeye kujiunga Chadema na kugombea urais.

Vilevile imewai kutokea kwa Bernard Membe ambapo baada ya yeye kuamia ACT Wazalendo kwa nia ya kugombea urais, lakini siku ya msiba hawakusoma historia ya yeye kujiunga na chama hicho.

Siasa za namna hii ni siasa za kitoto sana. Uwezi kufuta historia ya mtu ambaye amefanya jambo linalojulikana Dunia nzima, na historia hiyo hipo mpaka mitandaoni.

Mwenye kujua sababu ya kufanya hivyo, yani kufuta historia mtujuze!
 
Back
Top Bottom