Kwanini Wasabato hawana Baraza la Kuidhinisha "Halal foods"

masare

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
421
500
Kwa ndugu zetu Waislamu wanalo baraza la kuidhinisha "Halal foods" yaani vyakula ambavyo havijachanganywa na hata chembe ya product/ ingredients yoyote itokanayo na nguruwe pamoja na wanyama wengine waliokatazwa kwa kadiri ya imani ya Waislamu, Wasabato na Wayahudi.

Ukiangalia bidhaa za Azam Bakhresa kumewekwa mhuri kabisa kwenye makasha ya bidhaa zao kama juisi, biskuti, mikate n.k kuonesha kuwa vyakula hivyo ni "Halali".

Kwanini sasa nduguzetu Wasabato nao wasingekua na baraza la kwao la kuidhinisha "Halali" kwa bidhaa za vyakula vinavyotumika kila siku majumbani ili wasabato wasije wakatumia vyakula "haramu" yaani ambavyo vimechanganywa na chembechembe za products za kitimoto.

Nawasilisha
 

kikokotoo kipya

JF-Expert Member
Dec 18, 2018
389
500
Umetoa mfano wa brand moja tu iliyo na alama, na hivyo viwanda vinamilikiwa na Mwislam. Je, Waislam wanauona huo muhuri unauona kwenye bidhaa zitokazo China, Ulaya, Marekani ,Kenya na nchi nyingine nyingi?

Mtu aliyetengeneza juice na kuamua kutia nguruwe bila mlaji kujua hilo siyo tatizo. Tatizo ni mtu anayekula au kunywa huku akielewa humu kumetiwa kitu ambacho hakiendani na imani yangu.

Ukinunua nyama ya kopo, iliyoandikwa nyama ya ng'ombe kumbe ndani ni nyama ya punda, je hapo kosa ni la mnunuaji?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom