Kwanini Warundi wanapenda kuwa wakimbizi?

Kwanini Warundi wanapenda kuwa wakimbizi?

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,932
Reaction score
11,863
Nimefuatilia mgogoro wa Burundi jinsi ulivyo nimegundua kuna tatizo kubwa kwa hawa wenzetu warundi tofauti na hili la Nkuruziza kutaka kujiongezea muda wa kuwa madarakani.

Burundi kwa sasa hakuna civil war ni maandamano ya kawaida ya kutaka kumng'oa Nkurunziza madarakani tena tunaambiwa maandamano hayo yanafanyika mji mkuu Bujumbura sehemu zingine hali ni shwari sana.

Inakuaje wengine wafungashe kukimbilia Tanzania maandamano tu yanakufanya ukimbie nchi yako kwenda kuwa mkimbizi tena mwanaume nae anaacha kwenda kuandamana kuwaunga mkono anakimbilia kuwa mkimbizi.

Hivi huko kwenye kambi za wakimbizi kuna nini cha ziada kinachowafanya hawa watu waende kuishi huko na kuacha nchi yao, kwangu mimi binafsi mgogoro huu ni mdogo mno kutoa wakimbizi.

wakim.jpeg
 
Deals Ya UN
Kumbuka Hakuna Jambo Lolote Kule Yaani Full Usanii
 
Ukweli ni kwamba hakuna mtu anapenda kuikimbia nchi yake. Na ukimbizi hausababishwi na vita tu. Matatizo na shida za kiusalama, kiuchumi, kijamii, kiafya, ukabila, majanga ya kimazingira kama ukame, mafuriko, nk pia husababishwa ukimbizi. Na Burundi ni moja ya nchi yenye hali duni sana ya maisha hasa kwa watu wa hali ya chini. maisha ni magumu sana na Umasikini ni mkubwa mno. Na wanakimbilia tz wakiwa na imani kwamba tz kuna unafuu wa usalama, uchumi, na maisha ni cheap nk.

Usiombe yakukute ndugu yangu. ukimbizi ni balaa.
 
Bhanunu huyu jamaa Molembe hajatumia akili yake kwa ufasaha, kama angejua hao Warundi vita imeshawaathiri kwa kiwango gani, na hao anaowaona ni wanaume leo, miaka ya 1993 wakati wa mauaji ya hatari ndo kwanza walikuwa watoto, wakapotezana na familia zao, wakapoteza rasilimali zao pamoja na wazazi wao kuuawa mbele ya macho yao, asingesema.

Halafu ajue anapojimwaga JF,Twitter, FB, Airtel, sijui radio gani, kule Burundi hayo yote yamefungiwa. Hao wanaokimbia hawana full information kama alizonazo, wao wanasikia watu wanauana Bujumbura tu, sasa kwa nini wasikimbie?

Kikwete kasema ukipewa akili changanya na zako. Molembe Jiongezee akili kidogo inaonekana umeshiba, mind you sijakutukana ila nimekushauri tu, hakuna anayependa kuwa mkimbizi asilani.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo nchi ifutwe tu iwe sehemu ya tz maana kuna haja gani kuwepo wakati nusu ya raia wake tunakaa nao hapa, wanazalia hapa na kukulia hapa mpaka mtoto anafikisha umri wa mtu mzima hapa hapa tz???
 
Bhanunu huyu jamaa Molembe hajatumia akili yake kwa ufasaha, kama angejua hao Warundi vita imeshawaathiri kwa kiwango gani, na hao anaowaona ni wanaume leo, miaka ya 1993 wakati wa mauaji ya hatari ndo kwanza walikuwa watoto, wakapotezana na familia zao, wakapoteza rasilimali zao pamoja na wazazi wao kuuawa mbele ya macho yao, asingesema.

Halafu ajue anapojimwaga JF,Twitter, FB, Airtel, sijui radio gani, kule Burundi hayo yote yamefungiwa. Hao wanaokimbia hawana full information kama alizonazo, wao wanasikia watu wanauana Bujumbura tu, sasa kwa nini wasikimbie?

Kikwete kasema ukipewa akili changanya na zako. Molembe Jiongezee akili kidogo inaonekana umeshiba, mind you sijakutukana ila nimekushauri tu, hakuna anayependa kuwa mkimbizi asilani.

Na wewe tumia ubonge wako huwezi kusikia tetesi ukakimbia kwako halafu kukimbia tatizo sio kutatua tatizo ila ni kujiongezea matatizo yaani maandamano kidogo tu ya Bujumbura watu wanafungasha virago
Btw wewe na choko Bhanunu ni warundi.
 
Last edited by a moderator:
Ukiwa haujui sasa za Burundi, unaweza kuuliza hilo swali ila kwa kifupi, inavyoonekana hawa warundi hawamuungi mkono nkurunziza, kwaio hawata mpigia kura, na wasipo mpigia kura jamaa wanatafuta nani hajampigia kura jamaa maana yake wewe upo ba upinzani na ukiwa upinzani jamaa wanakuteketeza...
 
Utajaza Mkun.du we
 
Kumbe Burundi hamna upinzani.
 
Ulicho kiongea yaweza kuwa sahihi lakini kuna mengine hapo yanawasababishia hilo, waliokimbia wengi wana asili ya kuish tz, tena wanapenda tz kuliko kwao, wengi wamepata nafasi ya kurudi au kutimiza ndoto zao za kuishi tz, jua kule kuna uhaba wa ardhi na asilimia kubwa ya warundi ni wakulima, huna ardh huna umaisha kule, sasa wao wameshajikatia tamaa nakuona wenzao zaid ya 150000 Walipatiwa uraia na kufurahia maisha tz kiasikwamba wapo wanao miliki hadi ekari 10 huku, Tunapaswa kuwa makini sana midafulani wemawetu utakuja kuwa tatizo, tumeo na kina mchambawima1 wamekulia tz wamepataelim tz, wamejua kujichamba wakiwa tz leo wanaidharau tz na hata kututukana haya yasijirudietena
 
Last edited by a moderator:
Ni kushindwa kufikiri kabisa...kuamini kuna mtu anapenda kuwa mkimbizi..
 
Back
Top Bottom