Sasa Boss hiyo poverty mentality iko kwa huyu mwanamke mwenye gari au kwa mwanume asiye nalo? We unaona gari ni kama viatu lakini wenzio wakiona gari hata kama ni la serikali akili zinawaruka. It is a status symbol. Hata viatu havifanani. Vaa basi yebo yebo au R.I.O na mwenzio avae viatu vizuri (bahati mbaya sijui designers wa vitu vya kiume ukiacha kelvin clain) muwe na sifa zinazofanana halafu mpeane muda sawa wa kutongoza uone nani atawahi kufanikiwa).
Wanaume ndo waliokuwa wamezoeleka kuwa na magari ya kuwazuzulia wanawake. Sasa wanawake nao wana magari, nao wana shahada, vyeo, biashara, mali n.k. Haya mabadiliko unafikiri yamerahisisha maisha? Wanaume wamepoteza identities na wanawake pia. Nadhani umeshasikia neno "mwanaume suruali", "iron ladies" n.k. Ni vigumu mwanamke aliyejitanabaisha na "vitu vya wanaume" kuendelea kuonekana ni mwanamke yule yule. Wanawake wenye magari nao wanawazuzua vijana wasio nayo. Wanaume waoga wapo, wanajishuku kuwa wataonekana kapuku kama hawana magari na nyumba kama wanawake zao kwani uanaume wao wameuambatisha kwenye hivyo vitu. Wanawake wenye hela pia wana matatizo kama ya wanaume wenye hela. Wanafatwa na wengi kiasi kwamba hawajui nani kafata mapendo, nani kafata kulelewa. kazi yake inakuwa ngumu kuliko yule asiye navyo. Ni wanaume wanaojitambua tu wanaweza kuanzisha mahusiano mazuri na ya kudumu na wanawake wa aina hii wanaojitambua pia.