Kwanini wanawake hawawapendi ndugu wa mume?

Kwanini wanawake hawawapendi ndugu wa mume?

pucheon

Member
Joined
Sep 13, 2016
Posts
20
Reaction score
19
Kwa utafiti mwingi nilioufanya japo sina data za kupresent hapa lakini kuna haka katabia cha wanawake wengi walioolewa kutowapenda ndugu wa mwanaume hasa linapokuja suala la kuwasaidia kifedha na hata kimawazo.

Hua wanaonyesha waziwazi kuchukizwa endapo mwanaume ataamua kuwasaidia ila ikitokea ndugu zake ndo wanaitaji msaada iyo siku utapigiwa kelele na ata papuchi hutopewa kamwe.

Je tatizo ni nini wadau maana wengi wao wapo ivyo?
 
mkuu kiukweli hiyo mada imenigusa kwa namna moja au nyingine

coz mi nilikuaga na shemeji yangu aliolewa na kaka yangu kiukweli huyu shemeji yangu alikuwaga hanipendi kabisa hadi kwa kaka alikuwa hataki nifikee.

ila mimi nilikaza moyo nikaamua kujitenga nao saivi mi na maisha yangu nina kazi yangu
sasa tangie asikie nina kazi heshima imerudiiii kwa maana siku wakikwama huja kwangu kuniomba msaada wa chochote kile
 
kwa nn..umnyime mtu chakula alichotafuta ndugu yake?
si uchizi huooo.....!!
au unavyomnyanyasa ndugu za mume kesho damu yako wakiichukia je...

tubadilikeni wanawake
 
1.ndugu wa mume wanagubu sana
2.msimamo wa mume haukuwa wazi tangu mwanzo.
Kumbuka kaka ni baba kwa mila zetu sasa unapowaponda ndugu zako kwa mke unategemea nini?muweke wazi ajue kuwa hiyo ni part ya familia yako na unawajibika nayo.Ukikaza ataelewa tu coz mke ana talaka,lakini ndugu hana.
 
Ni wanawake wapumbavu tu wasio jielewa kwa kweli, wenye roho mbaya ila kwa mwanamke anayejitambua hawezi Fanya huo ujinga. Hii kitu ipo tu kwa kweli almost kwa kila family, huwa namwomba Mungu anipe roho wa upendo na aniepusha na huo ujinga wakuchukia ndugu wa mume.
 
kwa nn..umnyime mtu chakula alichotafuta ndugu yake?
si uchizi huooo.....!!
au unavyomnyanyasa ndugu za mume kesho damu yako wakiichukia je...

tubadilikeni wanawake
Tena kwenye msosi ndo usiseme cjui huwa wanafikiria nini, kuna mama ndo ilikuwa zake za uchoyo na ubinafsi jinsi siku zilivoenda watu tukakua sasa aliokuwa anawachukia wako vzuri wanasaidia wanawe hyo aibu anayoipata, wanawake wenzangu roho mbaya na choyo si nzuri dunia duara Leo kwako, kesho kwangu.
 
Ni wanawake wapumbavu tu wasio jielewa kwa kweli, wenye roho mbaya ila kwa mwanamke anayejitambua hawezi Fanya huo ujinga. Hii kitu ipo tu kwa kweli almost kwa kila family, huwa namwomba Mungu anipe roho wa upendo na aniepusha na huo ujinga wakuchukia ndugu wa mume.
Diva wape vidonge vyao hao wanakera kinoma
 
Tena kwenye msosi ndo usiseme cjui huwa wanafikiria nini, kuna mama ndo ilikuwa zake za uchoyo na ubinafsi jinsi siku zilivoenda watu tukakua sasa aliokuwa anawachukia wako vzuri wanasaidia wanawe hyo aibu anayoipata, wanawake wenzangu roho mbaya na choyo si nzuri dunia duara Leo kwako, kesho kwangu.
yaanii..!!acha tu sijui baadae wakifanikiwa unaanzaje wakati uliwanyanyapaa?!!
 
Wanawake huwa hawapendani hasa ukiwa ndugu wa mume alafu jinsia ya kike then upo kwake ndo maaamaaaaa,,,,majanga ..
Kwanza watagombana kwa kuanza kutegeana kazi,au wifi yake akivaa vizur, utasikia ndani tuna lala na njaa wakat pesa mnanunulia mavazi.
UKIWA wa kiume bora uwe na kazi kama huna kazi wakati wa chakula anakupa maneno mpaka unasema hiki choo cha KIKE......
 
Ni wanawake wapumbavu tu wasio jielewa kwa kweli, wenye roho mbaya ila kwa mwanamke anayejitambua hawezi Fanya huo ujinga. Hii kitu ipo tu kwa kweli almost kwa kila family, huwa namwomba Mungu anipe roho wa upendo na aniepusha na huo ujinga wakuchukia ndugu wa mume.

najiuliza sana pale bustanini eden,eva aliposhawishiwa ale lile tunda kwanini alianza kula yeye na kulibugia na kulifaidi ndipo akaenda kumshawishi na adam ale??kwanini asingeondoka nalo kwenda kula pamoja na "mmewe" adam au hata aanze kummegea kwanza adam??pale ndipo alipotengeneza asili ya mwanamke kujifikiria yeye kwanza ndipo wafuate wengine!pengine tunalalama tu kumbe ni asili wala si akili au utashi wa mwanamke kuwa hivyo!!Mungu akubariki ukawe mfano
 
Tz tunapenda sn misada ndo tatizo, na kukaa kwenye vijumba vya watu, kuna ndugu wa kiumeni wanakera saña na wanawake wapo wanaokera sio upande mmoja wa kulaumiwa, kiumeni lazima watambue kuwa kaka yao kaoa kwa iyo mfumo umebadilika pia, kama walizoea kuingia store ss mamá mwenye nyumba yupo lzma waombe
 
Kiukweli linapokuja suala la maisha ya kila siku, mama zangu mlionizaa na dada zangu (wanawake) siwaaamini kabisa katika mambo mengi sana. Kwasababu akili yenu mnaijua wenyewe.
 
Back
Top Bottom