Habari,
Nimeona leo tuangalie hili suala la kudharauliwa wanawake wasioolewa kwa kuwa linazidi kushika kasi zaidi.
Mimi ni mwanamke wa mtu ila kuna hii tabia ya watu kuwasema vibaya wanawake wasioolewa. Imekuwa ikiniuma sana, kwakuwa naamini kuwa wao hawakupenda hivyo.
Naomba kufahamu juu ya hawa wanawake ambao hawajabahatika kupata wenza wa maisha kwanini huwa wanadharauliwa sana hasa katika jamii ya watu wanaomzunguka.
Pia nataka kujua kuwa kwa hawa wanawake ambao hawajaolewa wamependa au kuna nini kinasababisha wao wakose waume wa kuwaoa.
Kwa upande wangu naamini kuwa kuolewa ni mipango ya Mungu.
Karibuni kwa michango
Nawasilisha
Kukosa mume tu ndio sababu ya kudharauliwa na wanaowazarau ni baadhi ya watu katika jamii husika
Sio wanawake tu hata mwanaume, kama umeoa heshima yako haiko sawa na asieowa,
Mwanamke hata awe mzuri kuzidi nini yenyewe kama hajaolewa bado ataonekana si lolote mbele ya jamii
Sometimes ni hisia tu za kujistukia
watu wengine wala hawajui wala kujali umeolewa au hujaolewa
MWANAMKE ANAYEWAZA KUOLEWA HUYO NI MUOGA WA MAISHA NA MPENDA MITELEMKO
Habari,
Nimeona leo tuangalie hili suala la kudharauliwa wanawake wasioolewa kwa kuwa linazidi kushika kasi zaidi.
Mimi ni mwanamke wa mtu ila kuna hii tabia ya watu kuwasema vibaya wanawake wasioolewa. Imekuwa ikiniuma sana, kwakuwa naamini kuwa wao hawakupenda hivyo.
Naomba kufahamu juu ya hawa wanawake ambao hawajabahatika kupata wenza wa maisha kwanini huwa wanadharauliwa sana hasa katika jamii ya watu wanaomzunguka.
Pia nataka kujua kuwa kwa hawa wanawake ambao hawajaolewa wamependa au kuna nini kinasababisha wao wakose waume wa kuwaoa.
Kwa upande wangu naamini kuwa kuolewa ni mipango ya Mungu.
Karibuni kwa michango
Nawasilisha
Hahahahaaa we jamaa khaaaaa!Nakumbuka bongo flavour ya kitambo iliyopigwa na NGONI TRIBE, walipiga Wimbo mmoja unaitwa MANUNGA YEMBE"... (wanawake wazuri wazuri wameolewa, yamebaki manunga yembe yanahangaika)... Ulimdharau mwanamke asiyeolewa....