Nawasalimu wakuu wote.
Leo mchana wakati nipo kwenye daladala, nikawa nawaza kimya kimya.
Kwanini utasikia Mwanamke ameenda kwa Mganga ili kumuwekea mume au mpenzi wake manjonjo asitoke kando?
Naomba nikiri, sijawahi kusikia tangu nimezaliwa, mwanaume ameenda kwa Mganga ili kumuwekea mke limbwata au mapenzi yakolee, Kuna nini hapa?
Inasemekana hata hawa vijana wa kiume wadangaji ( kina saydavto, noel gio etc) ni waumini wa waganga ili kulinda madanga yao, kwanini madanga hawaendi?
Nisiwachoshe tu ningependa kufahamu kuna connection gani hapa. Ni hilo tu kwa leo.
Ushindani wa wao kwa wao kila mwanamke anataka mume na wanaume hawana time, ili kulinda asipokonywe, ni Ndumba tu ukitaka utajiri wa ghafla ni kuwa mganga ktk nyanja hizi, yeye anapewa mshahara kwa yote;
Mwanamke anasomeshewa watoto, bure, analipwa uwepo wake pale,
Anapewa machejo bure,
Nyumba bure, Akifa mume ni yake hiyo.
Ana uwezo wa kuua mme bure, hkn wa kumuuliza.
anaweza kukupa chochote kama limbwata bure, na ukawa vyovyote zezeta bila maswali.
anaweza kukuzuia usiende kazini bure!
anapika, kula na kunywa atakavyo bure,
ukienda kazini au safari anaweza tumia mchepuko wake ndani kwako buree
anacheza mchezo kwa hela ya bureeee!
anasomeshwa bure mpaka chuo kikuu halafu anakuacha hapo bure.
Analia bure, bila mume hana pa kulilia.
Nguo chakula, joto, furaha, Ulinzi,watoto, makofi, mateke, kusali, Bure MPAKA KIFO
Wanaume hawaaminiki muda wowote upepo wa kisulisuli unambeba anakwenda kwa mwingine anakuachaia koti tu hapo.
hayo yoote lazima atafute limbwata tu, hata km ni mimi lazima nikukomeshe, nikuvune mpaka ukome.