Kwanini Wanajeshi hamtaki kuingiza ndugu zenu Jeshini?

Kwanini Wanajeshi hamtaki kuingiza ndugu zenu Jeshini?

hata mimi

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2017
Posts
1,356
Reaction score
1,449
Ukifuatilia wanajeshi wengi utakuta hawapo tayari watu wanaowapenda wafuate nyayo zao. Wanajeshi wengi utakuta mtu analalamikiwa na wanafamilia wake kwamba hatumii nafasi aliyopata kuwezesha wengine kuingia jeshini.

Utaona wanajeshi wengi wanalalamikiwa kutotumia nafasi walizonazo kusaidia watu wao wa karibu kujiunga jeshi... badala yake utakuta mtu kajaza mashemeji na ndugu wengine wengine wa upande wa mkewe tu

Wapo ambao wanaweka wazi kabisa kuwa hayupo tayari kuingiza ndugu yake Jeshini lakini wengi wao ni kimya kimya tu anakukaushia na hata kama ukitaka basi hakuzuii ila anakuacha upambane mwenyewe kuipata nafasi hiyo

Enzi za operesheni ya kwa Amin Serikali ilikuwa ikichukua mtu mmoja tu katika familia hata kama familia ina askari sita na sababu ilikuwa ni kwamba waliangalia endapo ikitokea swala la kifo basi familia zisije kukosa wapendwa wao kwa mpigo... sasa

Je na wanajeshi hiki ndicho wanachozingatia au kuna sababu nyingine?
 
Mimi Father amekataa katakata nisiende mpaka wenzie wamemshawishi lakini amekataa lakini kamsaidia Kaka, Mtoto wa mdogo wake kaingia na sasa ni Luteni Kanali.

Mpaka leo sijajua sababu namuonaje sijui.
 
Mwingine ni Major, Mtoto wake kabisa amekataa asiende... Mamayake akampeleka Kinguvu akaingia lakini baada ya Mafunzo ya Awali wamemrudisha yuko home saahizi tunaangalia nae Azamtv.
Nadhani inategemea na familia unayotoka wenzetu mkoa wa Mara wako poa sana kuhusu Connection
 
Walaa... Nikumuuliza ananiambia siku moja utajua kwanini!? Miaka 12 sasa sijaona chochote zaidi ya Msoto tu.
Na unahisi kuna huo unaouwaza?
Endelea kuteseka na umasikini
 
Then Ikitokea vita ndo unalazinishwa kuwa mwanajeshi, Wanajeshi pambaneni na hali zenu incase of anyvita
 
Kazi za majeshi wee, lazima ugangamale[emoji23][emoji23].
 
Mwingine ni Major, Mtoto wake kabisa amekataa asiende... Mamayake akampeleka Kinguvu akaingia lakini baada ya Mafunzo ya Awali wamemrudisha yuko home saahizi tunaangalia nae Azamtv.
Nimecheka sana eti tunaangalia nae Azamtv
 
Aaargh!! Wapi!! Mzee anazeeka vibaya. Hana jipya.
Sio wewe tu. Wazee wengi waliojiunga na jeshi miaka ya 70 wamepitia kipindi ambacho wanajeshi wengi walikuwa walevi, Malaya na wengi walishindwa hata kusimamia mali za urithi vizuri.

Wanakuja kustaafu wakiwa wamechoka, wanalewa tu hawana chochote mpaka wanakufa.
 
Back
Top Bottom