Nakumbuka miaka ya nyuma kulikuwa na vodka vladimir na zed za viroba yaan za kwene vikaratasi. Mda huo unapga vladmir zako vizuri afu viwili vya mwisho unapga vized ati kufuta harufu maana vilikuwa na harufu flan ya tunda la nanasi.
Wajomba cku hiyo nimepga vizur mda wa saa tano natoka banda la video niende home kwenye kona mbwa ndio hawa wakimfukuza mwenzao na ni kona sharp yaan kukwepa mbwa wa kwanza wa pili huyu hapa miguuni kwangu watatu nae akanipga mtama wa maana mim huyo chn nakumwangukia mbwa wa nne. Yaan after hapo kila kiumbe kilibuni njia yake coz wote tulishtuka na kigiza kile cha ucku niliea nyumban na kiatu kimoja kingne hadi wa leo cjui kilienda wapi. Asubuh niliporud kuangalia yale mazingira chini pamechimbika hadi njia utadhani ni watu walikuwa wanapachimba hadi watu walikuwa wakifika hapo wanakwepa kupita wakidhan ni wachawi wamefanya mambo yao pale. Tangu cku hiyo nilipanda daraja kwa lazima ni mwendo wa pombe ya chupa ili mda naenda nyumbani nabeba kama silaha, badae nikanunua gari.