Kwanini wakandarasi wa kitanzania hawakui na kufikia kushindana ktk soko la nje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini wakandarasi wa kitanzania hawakui na kufikia kushindana ktk soko la nje?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Nkamu, Apr 1, 2012.

 1. Nkamu

  Nkamu JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 206
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mimi ni mhandisi wa ujenzi (Civil Engineer), ambaye nimekuwa katika fani hii kwa miaka ipatayo kumi hivi. Katika kipindi chote hiki, sijaona kampuni ya kitanzania iliyoweza kupata mafanikio na kukua kiasi cha kuweza kushindana na makampuni yanayotoka nje ya nchi.

  Nimekuwa nikifikiria sana njia ya kuweza kuzisaidia kampuni hizi ili ziweze kukua lakini sijaweza kupata kitu kilicho halisi ambacho kinaweza kuwa sababu ya kushindwa kufanikiwa na jinsi gani ya kuweza kuepuka changamoto hizo na hatimaye mafanikio.

  Nimeona ni vema kuleta hapa jambo hili ili tuweze kufikiria kwa makini na kupendekeza ni njia gani tunaweza kufanikiwa kama taifa katika kuwasaidia wakandarasi wetu waweze kukua.

  Nawakaribisha kwa michango yenu yenye tija, karibuni!
   
 2. bg_dg_dy

  bg_dg_dy JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2012
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  Basi wewe yawezekana sio engineer aliyebobea ktk fani yako, ungekuwa umebobea miaka hiyo yote kumi ungeweza kujua changamoto zinazowakabili makandarasi wazawa. Huenda unasindikiza watu ktk fani "you ain't proactive"
   
 3. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Jaribu kuangalia mitaji waliyonayo inayoweza kuwafanya wafanye kazi zinazohitaji pesa nyingi.
  Pili angalia teknolojia waliyonayo katika kazi wanazofanya uone na kama wameweza kuitumia mahali popote na kuwafanya wawe na sifa ya kuaminika.

  Angalia uongozi wa kampuni hizo uone kama kweli ni uongozi firm wenye uwezo wa kuendesha na kuipatia mafanikio kampunii

  Angalia kama kweli they wako kwenye business au wapo tu kuganga njaa, wakipata vijisent basi wanaacha kazi.

  Ukiwa na majibu ya maswali haya rahisi basi unaweza kujua pa kuanza kuwasaidia.
   
 4. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu unatutia aibu:wink2:
   
 5. Nkamu

  Nkamu JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 206
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nashukuru kwa jibu lako! Lakini ninalo neno kwako; kama hujui tatizo ni nini, ni vema ukakaa kimya kuliko kuonesha ni jinsi gani sio mstaarabu! Hapa nataka tujadili mada na sio kujadili watu!

  Nimepost hapa kwa ajili ya majadiliano na kupata mustakabali wa tatizo kwa mapana na marefu na si fikra za mtu mmoja tu! Kama hujui kaa kimya, waachie wenye uwezo wa kujadili.
   
 6. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Hawakui kwa sababu wakishalipwa baada ya kumaliza kazi wanatumia sehemu kubwa ya faida zao kununua ma V8, kujenga nyumba za kifahari za kuishi pamoja na kukesha bar na vimwana. Hawaelewi kuwa kuna ku invest faida wanayopata katika kukuza kampuni zao. Engineers wenye akili ni wachache sana, wakiongozwa na George Rupia wa Del Monte ambapo growth ya kampuni unaiona dhahiri, wengine mhmhmh
   
 7. Nkamu

  Nkamu JF-Expert Member

  #7
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 206
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nashukuru kwa mchango wako mzuri sana.

  Katika hayo uliyoyataja nimekwisha yafanyia kazi. Kuna wale wenye mitaji ya kutosha lakini wakipewa kazi ni shida kubwa sana kuweza kuifanya kwa wakati na kwa kiwango kinacho kubalika.

  Kuna wale wenye uongozi mzuri lakini hawapewi kazi za kufanya na kuishia kudumaa na hatimaye kufa.
   
 8. Nkamu

  Nkamu JF-Expert Member

  #8
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 206
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Fikiria kwanza kabla hujaandika hapa. Kama kuna unachojua andika hapa, acha kulaumu. Nchi hii hatuendelei kwa mambo kama haya!
   
 9. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #9
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  kinachotudidimiza waTZ ni culture of ignorance. Au kinyume chake hatuna culture of excellence. Kwa asili tunasikia kichefuchefu mtu akitaja maneno kama Accuracy, Precise, Perfect, Excellence, Integrity, In Time, Superb. matokeo yake kazi nyingi za watu wetu ni kwa mtindo wa ILIMRADI INAFANYA KAZI ILIYOKUSUDIWA. Duniani hakuna mambo hii.
   
 10. bg_dg_dy

  bg_dg_dy JF-Expert Member

  #10
  Apr 1, 2012
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  TUTOLEE ***** HAPA, bora ungetuelezea moja kwa moja kuliko kumwaga uparatu humu jamvini. Ninaelewa sana hili game na sababu ninazo, sababu ambazo umezitoa kwenye post yako ndani ya thread hizi ni sababu mfu. Nitafute nikueleze kinagaubaga
   
 11. bg_dg_dy

  bg_dg_dy JF-Expert Member

  #11
  Apr 1, 2012
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  Issue hapa sio ulichokielezea hapa, the real problem hapa ni "lack of corporate governance" na "bridge finance"
   
 12. Nkamu

  Nkamu JF-Expert Member

  #12
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 206
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Sasa tumeanza kwenda sawa ili tuweze kuisaidia nchi yetu kabla muda wetu haujaisha!

  Naam, hebu amplify kidogo unapozungumzia suala la lack of corporate governance na bridge of finance!
   
 13. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #13
  Apr 1, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Mkuu Nkanu,
  Umeshajaibu kuangalia uwezo wa CASPIAN ama KASSCO? Hizi kampuni zinafanya vizuri sana kwenye sector ya Mining hizo ni engeering Company,
  Hao Kassco wanafanya kazi mpaka Zambia
   
 14. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #14
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Sahihi kabisa. Na hii siyo kwa mainjinia tu bali kwa profession nyingi sana (labda madaktari kidogo wamejipanga).

  Nitakupa mfano kwenye contracts ambazo ni competitive, unakuta yeye hajajipanga vizuri na anategemea kupata favours kutoka kwa yule anayeaward contracts. Mimi siyo engineer lakini nilikuwa kwenye kitengo ambacho kilikuwa kinahusika na procurement of consultants. Unajaribu kutoa favours kwa local experts na unamwelekeza kujaza zile RFPs lakini bado analeta zina makosa tele tele. Matokeo yake wengi wanakuwa disqualified hata kabla kufikia stage ya evaluation.

  Mainjinia wetu kama wanataka kuendelea na kuwa competitive lazima wajifunze vitu vingi, vikiwemo mbinu za kufanikiwa kupata contracts. Na wasione shida kujiendeleza kwa masomo ya aina hiyo hata kama yako nje ya profession yao.
   
 15. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #15
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Wadau nimefarijika sana na hii thread, kwani imenigusa moja kwa moja kwa kile ambacho nimeanza kukifanyia kazi leo hii tarehe 1.04.2012. Ni study/research itakayonichukua muda wa miaka 3 hivi. Kwa ufupi ni kwamba ninafanya study yangu katika eneo hili. Nina Background ktk construction na Business studies na kwasasa proposal yangu inahusu Entrepreneurship Sustainability and Trade Challenges in Tanzania's Construction Industry; focusing in growth of Local Tanzanians Firms. Bado naweka mambo sawa, halafu nitawasiliana nanyi wadau ili tuweze kuona nini hasa tatizo na nini kifanyike ili kuwasaidia Wazalendo wenzetu kufikia malengo yao na ya jamii ya Watanzania. Pia, matokeo ya study yangu nitayaweka hapa ili kuweza kusomwa na wengine wengi. Hili nitalifanya ikiwa ni pamoja na kuwapa links za International Journals zitakazoweza kuwajenga wale watakaokuwa na hitaji.

  NB: Ndudu zangu wakati ukifika nitakapohitaji msaada wenu wa mawazo hasa kwenye dodoso, tafadhali naomba muwe tayari kusaidia.

  Natanguliza shukrani.
  RDI.
   
 16. mundo

  mundo JF-Expert Member

  #16
  Apr 1, 2012
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wote mnajua ukweli lakini mnapindisha......ppra.....crb.....tender board za mashirika na taasisi......wasimamizi wa site na wakaguzi wa site.........changanya na zako?
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Apr 1, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe kabisa. Angelikuwa serious, angeanza kwanza kujua sababu za wakandarasi kutofanya vizuri. Kwangu mimi suala la mitaji ya kufanyia kazi, uwezo mdogo wa kitaalamu wa kuzifanya kazi hizo na kukosekana kwa malengo ya muda mrefu miongoni mwa wakandarasi zinaweza kuwa ndio sababu. Kampuni nyingi za kikandarasi zimekaa kusubiri mambo ya "bongo tambarale"...kuna fedha za mjomba mjomba za kuchukua bila kufanyia kazi. Leo hii eneo lenye ubadhilifu mkubwa kwenye halmashauri zetu ni miradi inayoendeshwa na makandarasi tena hawa locals. Wanashirikiana sana na halmashauri zetu kula hela za walipa kodi tena mara nyingine bila hata kufanya kazi yoyote. Kampuni za aina hiyo zitakuwa vipi? Huo si wizi tu kama wizi mwingine???
   
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  Apr 1, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  I agree with you the guy has got balls and he pushes forward his company...ila huyu bwana sio engineer. Ni fundi mchundo so siku nyingine usiidhalilishe fani.
  Well, kama kuna kampuni local inayojiendesha vizuri sasa hivi na kazi zao ziko up to standards, SKOL contractors wako juu. Just making your own due dilligence mtaligundua hili. Tatizo linakuja moja tu....ataweza kumudu wazee wa cartel kama Estim and the rest ambao they can make big plans and implement them????
   
 19. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #19
  Apr 1, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  wakandarasi? mbona unaenda mbali? huulizi fani rahisi kama muziki, michezo ambazo pia tunashindwa!
   
 20. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #20
  Apr 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Tunaomba utueleze umeshafanya miradi mingapi na vikwazo vilikuwa nini...you have a first hand experience don't you?

  Zaidi ya hapo nadhani ni kutokuwa na uzoefu wa biashara maana miradi mingi nchi hii imewapa lakini mmeshindwa kutu-impress...:nono:
   
Loading...