Kwanini wakandarasi wa kitanzania hawakui na kufikia kushindana ktk soko la nje?

I agree with you the guy has got balls and he pushes forward his company...ila huyu bwana sio engineer. Ni fundi mchundo so siku nyingine usiidhalilishe fani.
Well, kama kuna kampuni local inayojiendesha vizuri sasa hivi na kazi zao ziko up to standards, SKOL contractors wako juu. Just making your own due dilligence mtaligundua hili. Tatizo linakuja moja tu....ataweza kumudu wazee wa cartel kama Estim and the rest ambao they can make big plans and implement them????



sawa nakubaliana na wewe ila nchi hii inaweza kuendeshwa na watu wenye Elimu kama hiyo na sivyo mnavyofikiria
 
Nimekwishafanya miradi 6 hadi sasa. Na katika miradi yote nimekuwa nikifanya na makampuni ya nje. Kitu kilichonifanya nianze kuwaza kuhusu hili jambo ni namna ambavyo asilimia kubwa ya miradi inachukuliwa na wakandarasi wa nje. Ukiangalia watendaji katika miradi hiyo yote unakuta asilimia kubwa ni watanzania, kitu ambacho kinanishawishi kuona kwamba technical capability tunayo. Watu wa nje wanakuwa kwenye ngazi ya uongozi ambayo nayo ktk uzoefu wangu, ni wachache ambao unaweza kusema wametuzidi sisi. Mambo mengi tunajadiliana hadi kufikia kuamua tufanye nini, hivyo ktk masuala ya uongozi hatuko vibaya sana.

Nilifanya na kampuni moja nikiwa upande wa client, mambo niliyokutana nayo kutoka kwa wakandarasi wetu wanapoomba kandarasi inatia aibu. Unashindwa hata kuelewa kama watu hawa wanajua kuwa ukandarasi ni biashara na pia ni kazi inayohitaji taaluma fulani. Watu hawawezi hata kutengeneza unit price ambazo ni realistic. Bei zinawekwa tu na ukiomba breakdown ya rate zake hawezi kukupa!

Kuna wenye makampuni ya kitanzania ambao wanajua kuwa akisha saini mkataba basi ile pesa aliyosaini kwenye mkataba ni yake, hivyo haoni haja ya kumobilize resources kwa ajili ya kuanza uzalishaji site. Wanachoweza kufanya ni kutumia hizo pesa kwenye mambo mengine yasiyohusiana na mradi aliopewa.

Sasa kutokana na jinsi nilivyoona ktk maisha yangu ya kazi ndipo nilipotaka kujua uzoefu wa wadau wengine katika fani hii ya ukandarasi na kama kuna mambo mengine nisiyoyajua.

Ninachokifikiri ni kwamba, labda inabidi tuwe na utaratibu au sheria itakayoweka muongozo wa namna ya kuendesha kampuni na hasa za ujenzi. Utaratibu ambao utaweka mamlaka ya kila mtendaji ktk kampuni ili kuzuia wakurugenzi wasio wataalamu kuingilia maamuzi ya kitaalamu.

Nitaendelea baadae.....
 
Mtakuwa saa ngani nanyi mnafanya kazi bila viwango engineer wangu.
kaone pale mbezi stend mpya
kibao cha kuelekeza turn left/right kimeandikwa kwa mkono
kikasimikwa kwenye pipa lililojazwa mchanga, na waziri kabariki kituo.
barabara inawekwa kiraka leo kesho bonge la shimo limeshafumuka pale pale.
hivi kweli kwa kazi kama hizo mtakuwa kweli mkuu wangu.
 
Kwanza kabla ya kusaidiwa ni bora kujisaidia wenyewe kwanza....Jiulize kampuni inakua vipi?! Moja: Organically mbili: Inorganically.
Organically: kikubwa ni through reinvestment of profits into expansion...Kupata facilities zaidi ili kuongeza capacity na pia kuleverage..kutumia deni kuongeza mtaji
Inorgarnically: kushirikiana (JV au consortium), au kuungana, au acquisition....unaweza kuona jinsi PWC walivyopatikana
Sasa wewe kwa miaka kumi uliyokuwa unaoperate kampuni yako imeshakua kiasi gani....in terms of assets,Income, projects value etc, imekua vipi? na ni nini ur expansion strategy next 5 yrs....or medium n short term?!
Sasa kila mtu kama anataka akue yeye tu peke yake ni ngumu hivyo competition will have to correct that..but as u no in Tz competition is not that free or fair n in some cases not open
 
Mimi ni mhandisi wa ujenzi (Civil Engineer), ambaye nimekuwa katika fani hii kwa miaka ipatayo kumi hivi. Katika kipindi chote hiki, sijaona kampuni ya kitanzania iliyoweza kupata mafanikio na kukua kiasi cha kuweza kushindana na makampuni yanayotoka nje ya nchi.

Nimekuwa nikifikiria sana njia ya kuweza kuzisaidia kampuni hizi ili ziweze kukua lakini sijaweza kupata kitu kilicho halisi ambacho kinaweza kuwa sababu ya kushindwa kufanikiwa na jinsi gani ya kuweza kuepuka changamoto hizo na hatimaye mafanikio.

Nimeona ni vema kuleta hapa jambo hili ili tuweze kufikiria kwa makini na kupendekeza ni njia gani tunaweza kufanikiwa kama taifa katika kuwasaidia wakandarasi wetu waweze kukua.

Nawakaribisha kwa michango yenu yenye tija, karibuni!
asante sana kwa kuongea ukweli mtupu. ili ni changamoto sana kwetu wa tz. nadhani shida yetu ni kukosa ileinyaoitwa kwa kimombo business acumen
 
Wadau nimefarijika sana na hii thread, kwani imenigusa moja kwa moja kwa kile ambacho nimeanza kukifanyia kazi leo hii tarehe 1.04.2012. Ni study/research itakayonichukua muda wa miaka 3 hivi. Kwa ufupi ni kwamba ninafanya study yangu katika eneo hili. Nina Background ktk construction na Business studies na kwasasa proposal yangu inahusu Entrepreneurship Sustainability and Trade Challenges in Tanzania's Construction Industry; focusing in growth of Local Tanzanians Firms. Bado naweka mambo sawa, halafu nitawasiliana nanyi wadau ili tuweze kuona nini hasa tatizo na nini kifanyike ili kuwasaidia Wazalendo wenzetu kufikia malengo yao na ya jamii ya Watanzania. Pia, matokeo ya study yangu nitayaweka hapa ili kuweza kusomwa na wengine wengi. Hili nitalifanya ikiwa ni pamoja na kuwapa links za International Journals zitakazoweza kuwajenga wale watakaokuwa na hitaji.

NB: Ndudu zangu wakati ukifika nitakapohitaji msaada wenu wa mawazo hasa kwenye dodoso, tafadhali naomba muwe tayari kusaidia.

Natanguliza shukrani.
RDI.
Habari kiongozi.. natumai Research yako tayari imekamilika.. tunaomba utupe feedback kidogo.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom