Kwanini wajawazito wanafanyiwa hivi?

Kwanini wajawazito wanafanyiwa hivi?

kidadike

Member
Joined
Feb 19, 2013
Posts
33
Reaction score
28
Kuna jambo moja linafanywa kwenye hospitali na zahanati za Serikali mimi binafsi naona kama haliko sawa Naomba ndugu zangu mnisaidie kunipa muongozo katika jambo hili.

Kuna binti mmoja amepata ujauzito lakini bahati mbaya kijana aliyehusika amekataa sasa binti huyu amepata changamoto ambayo mimi naiona ni kubwa alipoenda kwenye hospitali fulani ya wazazi ili aanze kliniki. Bahati mbaya amekataliwa kuanza kwa sababu utaratibu wa hospitali unamtaka aende na aliyempa ujauzito na kama amezaa na mume wa mtu basi aende na barua kutoka uongozi wa mtaa.

Akaamua kwenda katika zahanati akakutana na changamoto hiyohiyo, mpaka hivi sasa haeweli afanye nini na ukizinga hospitali za binafsi zina gharama kubwa.

Japokuwa kuna umuhimu mkubwa sana kwa mwanaume na mwanamke kwa pamoja kushiriki Kliniki kwa ajili ya malezi ya mtoto lakini jambo hili naona kama linawanyima wanawake haki hasa ukizingatia kipindi cha ujauzito ni kigumu.

Je, pia ni sahihi wanapowajibu kwamba kama hajaenda na aliyempa ujauzito ni Malaya?
 
Kwanini usikubali kwenda nae tu?! Hata kama mume wa mtu ukifika huko kataa ww siyo mume wa mtu. Na hata hvyo anaogopa bure tu kwenda kuandikiwa barua maana haunyimwi na wala huulizwi maswali ya kijinga.
 
Barua na "Kijacho" huyo, ina uhusiano gani?? Je, kama hamtaanzisha hiyo klinik ndo tuseme mtoto huyo hatazaliwa?? Mambo ingine naona ni ufiraun tu umewajaa watu.
Mimba ishanasa, sasa fikirini namna ya kumpokea mgeni hayo ya babake nnani tutayajua baadaye. Obama angepatapi urais wa Marekani hao wapuuzi wangekuwa huko kwao?? Tafuteni njia nyingine ya kuongeza vifo vya utotoni sio hii. Ndo maana kila mission mnayoifanya ina buma. Na Kijobisimba amenyamaza tuuu kazi kutetea wapinzani. Yaani nachukiaaaaaa
 
Ni kweli haunyimwi lakin usumbufu unakuwa Mkubwa wengine wanaamua kumuomba mtu yeyote ili aende nae akamsaidie lakini sio jambo zuri
 
Barua na "Kijacho" huyo, ina uhusiano gani?? Je, kama hamtaanzisha hiyo klinik ndo tuseme mtoto huyo hatazaliwa?? Mambo ingine naona ni ufiraun tu umewajaa watu.
Mimba ishanasa, sasa fikirini namna ya kumpokea mgeni hayo ya babake nnani tutayajua baadaye. Obama angepatapi urais wa Marekani hao wapuuzi wangekuwa huko kwao?? Tafuteni njia nyingine ya kuongeza vifo vya utotoni sio hii. Ndo maana kila mission mnayoifanya ina buma. Na Kijobisimba amenyamaza tuuu kazi kutetea wapinzani. Yaani nachukiaaaaaa
Sawa mkuu.. Naona una hasira sana
 
Nini faida za mwanaume kwenda kliniki???
Labda tuanzie hapo
 
Bahati mbaya amekataliwa kuanza kwa sababu utaratibu wa hospitali unamtaka aende na aliyempa ujauzito na kama amezaa na mume wa mtu basi aende na barua kutoka uongozi wa mtaa

Umenitoa kwenye reli
Ujauzito......, na kama amezaa na mme wa mtu..., mawili yote yanawezekanaje at the same time?
 
Japo dogo sana hilo kama shida yao ni aliempamimba aende nae si amtafute tuu mtu yeyote anaemuamini kuwa ni mzima akapimwe nae tuu au haiwezekani
 
Back
Top Bottom