Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 39,467
- 60,796
KIjana x alikuwa anasoma chuo kimoja kwa fani ya udaktari, kutokana na juhudi na kipaji alichokuwa nacho, alikuwa ni mwepesi sana wa kuelewa jambo pamoja na kulifanyia udadisi.
Alipofikia mwaka wa mwisho wa kuhitimu masomo yake, alishindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto za kushindwa kulipa ada.
Kijana x ilibidi aache masomo na kuanza kufanya vibarua mbali mbali, ingawa ndoto yake kubwa ilikuwa ni kutaka kuwa daktari bingwa wa upasuaji wa moyo.
Kutokana na changamoto ya kuacha masomo, aliamua kujisomea vitabu mbalimbali vya tiba ili aendelee kujiongezea maarifa.
Katika kijiji alipokuwa akiishi, walimuomba kijana x aweze kuwasaidia kuwapatia huduma ndogo ndogo za kiafya katika zahanati.
Kupitia uzoefu wa kujitolea kwenye vituo vingi vya afya, akajikuta naye anaweza kufanyia watu upasuaji.
Kutokana na hamasa ya kutaka kuwa bingwa wa upasuaji kwa magonjwa ya moyo, kupitia uzoefu wa kazi na jitihada binafsi ya kupitia vitabu na tafiti mbalimbali, akajikuta amekuwa mbobezi wa upasuaji wa moyo.
Siku moja bwana A, akakumbwa na tatizo kubwa la moyo na akajaribu kutafuta matibabu ya hapa na pale kwa miaka mingi, bila kupata suluhisho la kudumu.
Kutokana na tatizo kuwa kubwa, bwana A alizimia akawa hajitambui na ndugu zake wakapoteza matumaini ya ndugu yao kama atapona tena.
Ndipo mzee mmoja akashauri ile familia ya bwana A, wampeleke mgonjwa katika hospitali Z ambapo kuna daktari bingwa (kijana x) ambaye hana vyeti.
Wanafamilia wakakubali ushauri na kumpeleka mgonjwa hospitali z.
Kijana x (daktari) alipomuona mgonjwa (bwana A) na hali aliyokuwa nayo, kwa viashiria vya kimatibabu, daktari akashauri leo jioni itabidi bwana A afanyiwe upasuaji wa moyo.
Baada ya siku tatu, bwana A akawa amepata matibabu sahihi na tatizo lake la moyo likawa limeisha.
Bwana A kutokana na furaha aliyokuwa nayo, akaamua kumzawadia nyumba kijana x kwa kuokoa maisha yake.
Baada ya miaka miwili kupita kukawepo na sera, daktari yeyote yule anayetoa huduma za matibabu ya moyo lazima awe amesoma kwa kiwangi cha PhD na awe na leseni inayotambulika na wizara, kama hutokuwa na sifa hizo na unafanya hizo kazi, itakulazima kupewa kifungo kwa kuwa unacheza na maisha ya watu.
Kwa bahati mbaya, bwana A ndiye kiongozi wa msako na mhakiki wa leseni za madaktari wote.
Alipofika kumhakiki kijana x na , bwana A hakuendelea na kumhakiki, bali alipiga magoti na kunyooosha mikono juu na kuanza kulia.
Sijui alikuwa analilia nini? Leta jibu.