Kwanini wafanyakazi wa Zanzibar wawekewe nauli za usafiri kwenda kazini na kurudi wa Tanzania bara wasipewe?

Watanzania mjue jambo moja tu.

Tanzania Zanzibar hawakuanza kupewa nauli leo.

Wafanyakaz Zanzibar walianza kupewa nauli zamani kidogo.

Raisi Samia angalia hili
siku mkiacha kutaja neno Tanzania bara mkajiita Watanganyika mtaongezewa,zanzibar ni taifa linalojitambua na kuendesha mambo yake bila kubughudhiwa na yeyote
 
Ndugu yangu sisi watanganyika tupo wengi tu wenye akili tatizo ni viongoz wa ccm wenye mamlaka,tunafanyaje?hadi tutakapowaondoa madarakani
Sio kweli wengi wenu watanganyika ni mbumbumbu katika kuufahamu muungano hebu angalia hata huyo mleta mada na hao wachangiaji
 
Subiri kwanza bado wadudu wanapiga show hapo Chuga wafanyakazi wameletewa burudani.
 
Una uhakika?

pia ukumbuke na population ya Tanzania, ukilinganisha na nchi ya Zanzibar.
Kwahiyo kwa akili zako ukipewa essay juu ya ufukara Tanganyika point #1 ni eneo kubwa la kijiografia na point #2 ni idadi kubwa ya wananchi!!!
Maskini hii nchi ina vilaza wengi , tena wengine wana degree kabisa.
China ina idadi kubwa inafanana na idadi ya Waafrika wote lakini vipi wanaishi kifukara?
 
Jibu ni rahisi, wao wana serikali na ndiyo iliyoamua hivyo. Watanganyika hawana serikali, nani atawasemea? Tukiunga mkono madai ya Mtikila (RIP) tutafanikiwa.
 
Tunarudi pale pale.
Tunajinasibu Muungano! Ni uchawa tuu!
Hizi inaeleweka ni NCHI 2 tofauti! Rais wao, Kaatiba yao! Mamlaka polisi jeshi lao.
Watu wanaposema Katiba mpya ni Sasa hakieleweki tu! Wapinzani wakisema mnaleta ngonjera za kulindana! Ndio maana tumerudi nyuma sana.

Umesikia Rais akisema nyongeza ya mshahara wamepokea na wataifanyia kazi uchuminwa nchi ukikua kidogo!!

Huko bungeni na waziri wa Fedha mzee wa Tai bendera anajinasibu mama kakuza uchumi!!
Yaani yanayosemwa ni tofauti na uhalisia!!
WaTanzania tuamkeni Katiba Katiba.
 
Si muende mkafanye kazi huko, kwanini mnatupigia kelele, tuna mambo mengi ya kushuhulikia ikiwa ni pamoja na kupambana na athari za mafuriko.
Acha uzumbukuku wewe!Tangu lini mwandiko uliwahi kumpigia mtu kelele?Tunajadili mambo ya kiutu uzima.Wewe katoto ukacheze na wenzio.
 
Hii inafanana na ile ya kulalamika kwa nini dialysis Zanzibar ni bure!!

Mambo yao waachiwe wenyewe, tupambane na yetu!

Kikokotoo kimetushinda..
 
Back
Top Bottom