Kwanini vyuo vya Tanzania havina endowment funds?

Midevu

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
274
437
Endowment fund ni nini?
Kwa kifupi, ni mfuko ambao fedha za za michango na misaada kwa chuo huwekwa na kuwekezwa sehemu mbali mbali ili zizalishe faida. Hiyo faida inatumika kutunza thamani ya huo mfuko na kufadhili shughuli za chuo kama tafiti na ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wenye vipaji au wanaotokea kwenye mazingira magumu.


Ukiangalia vizuri list ya vyuo vinavyoongoza kwa ubora duniani utagundua kuwa list ya yuo bora haitofautiani sana na list ya ukubwa wa endowmnet funds za vyuo.

Hili suala lipo hivyohivyo ukiangalia list ya vyuo vyenye endowments kubwa Africa ndio hivyo hivyo vilivyo juu kitaaluma.

Hili halishangazi kwa upande mmoja kwa sababu ukiwa na pesa unaweza kuleta wanafunzi bora chuoni kwako na watafiti/ walimu bora pia watataka kufanya kazi kwako na mambo mengine mengi yanaweza kufanyika kuboresha chuo.

Kinachoshangaza ni kwa nini vyuo vyetu havina hii mifuko? Chuo kama UDSM kina alumni wengi sana, wakichangia hata buku 10 tu inatosha kuanzisha mfuko mkubwa tu.

Angalia namna endowment funds zinavyoviweka vyuo vya South Africa kwenye chati kwa Africa. Kuna vyuo vina endowments za zaidi ya trilioni moja tshs. Kwa hiyo chuo kinaweza kupata hadi bilioni 50 tshs kutoka kwenye hiyo fund. Hapo ni kabla ya tuition fees na fedha za consultancy, research commercialization n.k.


View: https://www.youtube.com/watch?v=MHQvSA8rOpQ&t=610s

Same story kwa USA;


View: https://www.youtube.com/watch?v=SRAfRu4ez_s
 
Back
Top Bottom