Kwanini baadhi ya vyuo vya Afya havigusiki?

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,296
3,967
Mafunzo ya Afya kwa kada ya kati nchi hii ni muhimu sana kwa vile wahitimu wa vyuo hivi ndio kwa kiasi kikubwa wanahudumia wananchi walio wengi katika suala zima la Afya ya msingi.

Hata hivyo kuna baadhi ya vyuo vilivyoaminiwa kutoa mafunzo ya kada hii vimekuwa vikifanya uhuni wa kila aina.
Unakuta chuo kimedahili wanafunzi darasa moja wanaofikia 500-600.Ukiangalia idadi ya wakufunzi unakuta ni wachache sana.
Darasa kama hilo ni vigumu sana kuliendesha kwa ukubwa huo.Mamlaka zinazosimamia zinafahamu ila ziko kimya.

Kuna chuo kimoja Dodoma kimedahili wanafunzi kwa kozi ambayo ilifutwa na wizara ya afya, lakini wamechukua ada na malipo ya mtihani wa wizara huku wizara yenyewe ikikana kutoa mitihani.Mkurugenzi ametamba kuwa yeye ana hela na wanafunzi hao hawawezi kumfanya lolote.Hii kauli yake ni kweli kabisa kwani hata mwaka uliopita,kuna vyuo vilionywa kwa kufanya uhuni katika udahili ila na chuo hicho kikiwemo,lakini wao hawakuchukuliwa hatua yoyote.Inasemekana kuna mwanasiasa ana mkono hapo na baadhi ya watu wanaofanya NACTVET.

Hata hivyo haya yanaachwa kwa vile Rais ni kama wanamchukulia poa na wanajua hawezi kuhoji vitu kama hivi vidogo.Hapa ni waziri Mkuu aingilie maana hivi vyuo vibasimamiwa na wizara mbili yaani ya afya na elimu.Kwa hiyo wapigaji wala milungura wakibanwa wanatupiana mizigo.Ila tatizo kubwa lipo NACTVET.
Tafadhali lindeni watoto wa maskini wasitapeliwe na vyuo hivi.
 
Back
Top Bottom