Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,160
Imeandikwa Katika Biblia, kitabu cha Mithali 14:34 nanukuu "HAKI HUINUA TAIFA, BALI DHAMBI NI ADUI WA WATU WOTE" mwisho wa kunukuu.
Pamoja na kuwa Mimi siyo Askofu wala Sheikh, lakini nafahamu kuwa AMANI na HAKI ni pacha na huwezi kuvitenganisha vitu hivyo viwili, yaani AMANI na HAKI.
Inafahamika kupitia malalamiko mengi ya wananchi, kuwa Katika nchi yetu, watawala wetu hawatutendei Haki, lakini ni watawala wetu hao hao, hupenda kuwahimiza viongozi wetu wa dini, wahubiri amani, bila kwanza wao kututendea Haki, kama ambavyo imeandikwa Katika Biblia, kama nilivyonukuu.
Ni kwanini viongozi wetu wa dini Katika mahubiri yao, sijawasikia hata siku moja, wakiwahubiri watawala wetu, wakubali kutenda HAKI kwa kuiandika upya Katiba yetu, kwani ndiyo sheria mama, kwa kuwa Katiba tuliyo nayo hivi sasa, HAIKIDHI kabisa, mfumo wa vyama vingi, tulio nao hivi sasa na inakipendelea chama tawala cha CCM?
Hata Rais wetu, Samia Suluhu Hassan, anafahamu umuhimu wao viongozi wetu wa dini na akawasihi viongozi wetu wa dini, wahimize wananchi wadumishe amani, kwa kuwa kama alivyoeleza Rais wetu kuwa hao viongozi wetu wa dini, ndiyo wanaosikilizwa zaidi na sisi waumini wao!
Hivi hao viongozi wetu wa dini hawajui kuwa Hawa watawala wetu wa CCM, hawatendi Haki, kwa kupiga "chenga" kuiandika Katiba mpya ya nchi, huku wakiendelea kukumbatia Katiba ya zamani ya mwaka 1977, ambayo wanajua fika kuwa inaipendelea CCM na iliandikwa wakati wa mfumo wa chama kimoja, ilihali wakati huu tupo kwenye mfumo wa vyama vingi, ambapo Katiba hiyo ya zamani HAIKIDHI kabisa, mfumo huu wa vyama vingi?
Hivi viongozi wetu wa dini ni "vipofu" kiasi ambacho hawawezi kuona namna Katiba yetu ya sasa, inavyoviminya vyama vya upinzani, uwepo wake?
Hivi viongozi wetu wa dini, hawaoni namna watawala wetu wasivyovitendea vyama vya upinzani Haki, kwa kuendelea wao CCM kuendelea kufanya mikutano ya hafhara, wakati wanawatuma Polisi wao kuwapiga marufuku, vyama vya upinzani visifanye mkutano wowote wa kisiasa?
Hivi viongozi wetu wa dini, hawaoni namna Rais wetu, ambaye pia ndiyo Mwenyekiti wa Chama chake cha CCM, namna alivyopewa madaraka makubwa mno ya kikatiba, kitu kinachosababisha, aendelee kuviminya vyama vya upinzani?
Hivi viongozi wetu wa dini hawaoni madaraka makubwa aliyopewa Rais wetu ya kuteua wajumbe wote wa Tume ya uchaguzi nchini, Majaji wote wa Mahakama juu, Wakuu wote wa Mikoa, wakuu wote wa wilaya, wakurugenzi wote wa wilaya, ambao pia ndiyo wasimamizi wakuu wa chaguzi zetu?
Hivi upendeleo wote uliopewa chama cha CCM kwenye Katiba yetu, ina maana viongozi wetu wa dini, wamekuwa "vipofu" na hawawezi kabisa kuuona?
Nawasihi viongozi wetu wa dini, Kila watakapokuwa wanatusihi sisi wananchi tuendelee kudumisha amani, wafunguliwe mioyo yao na waone umuhimu mkubwa wa kuwasihi watawala wetu pia wadumishe HAKI Katika utawala wao, kwani huwezi kuitenganisha AMANI na HAKI, kwani vitu hivyo ni PACHA.
Mungu ibariki Tanzania