Kwanini viongozi wanavaa miwani?

Dokta Uchwara

JF-Expert Member
Apr 29, 2022
1,371
3,146
Sijui mmeshagundua? Kila kiongozi nchini lazima ajitutumue kuvaa kamiwani hata kama si mgonjwa wa macho.

Haka kastaili cha viongozi kuvaa vimiwani wamekatoa wapi? Ni fasheni? Ujiko? Au kasumba fulani ya kishamba?

Kwa nchi kama Marekani, sijawahi kuona rais ana kamiwani. Ni nadra sana kukuta kiongozi amevaa kamiwani. Ni wachache.

Hata JK wakati anaingia madarakani hakuwa na miwani. Lakini alivyojipachika tu jina la DOKTA tukaona anaanza kuvaa kamiwani.

Na samia pia, alikuwa ana kamiwani ka kuzugia toka enzi za umakamu, lakini yeye alikuwa anakavaa kwa kukaweka juu ya pua.

Na mawaziri wakuu pia toka awamu ya Mkapa, wote wana vimiwani eti!!

Kwani hauwezi kuwa kiongozi bila kuwa na kamiwani cha maigizo?

Ni kama aina fulani ya ugonjwa wa akili?
 
Kuna kazi kubwa ya kuongoza wajinga ndio maana macho yanauma kutokana na maumivu ya kichwa.kitaalamu wanasema (eye cotyledonhaeach)


Mbona hata hao akina JK nao wanaonekana ni wale wale tu akili za TIA MAJI TIA MAJI.

Bora Magufuli tunajua ana historia ya kuvaa miwani tangu akiwa mtoto.

Sasa huyu JK! Duh! Tangu ajipachike UDOKTA ni mwendo wa kamiwani Na NAPE
 
Labda Kuna ka ukweli.

Hebu mawaziri wasiovaa miwani ni Gwajima, dada Joy, Mwaimu, yule wa ardhi, wengine wote nadhani wanavaa miwani.

Waziri mkuu ambaye hakuvaa miwani akiwa waziri mkuu Ni Nyerere, kawawa, Sokoine na Msuya wengine wote walivaa.
 
Mawani yanaficha aibu za mtu alizonazo machoni (hamuwezi kumsema kwamba anaona aibu kuangalia wananchi au kamera)

Maglasi yanavaliwa/yanawasaidia wale wenye matatizo ya uoni (hasa wazee)

Miwani inachukuliwa/inavaliwa kama fasheni na mauzo (ili uonekane serious, msomi, mwenye cheo, msafi na gentle)
 
Sio kwamba wengine wanakuwa hawajapimwa afya mpaka wapate uongozi ndio wanajua wana matatizo ya macho?
Yeye mwenyewe aliyeandika hii thread akipewa free chechup ya macho lazima akutwe na tatizo la macho.

Walikuja Wamarekani Bongo kufanya clinic ya macho bure kwa wiki moja uwanjani wa Taifa, kuwahi namba ilibidi udamke SAA 10 usiku ndio update namba ya kufanya checkup kama ni Dawa utapewa kama Miwani ya aina zote IPO ya kuonea kusomea na ya jua bure.

Sikwenda kwenye hii clinic kwa sababu ni bure la hasha Bali ni imani yangu kwao.

Sasa ule umati uluokuwa unajaa pale uwanjani wa Taifa huwezi kuamini, tatizo la macho ni kubwa ni sana Tanzania na hiyo ni Dar peke yake.

Nilichogunduwa kwa vumbi la Bongo huwezi kusalimika macho, nawashauri watu waanze kuvaa Miwani ya jua kulinda macho yao tatizo ni kubwa sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom