Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 576
- 1,625
Wahitimu waliomaliza elimu ya juu kwa kupata mkopo kutoka bodi ya mikopo kutwa wanabanwa kurudisha mikopo hiyo wakati wengi wao wanahangaika mtaani bila ajira wala shughuli za kufanya.
Wakati ukiangalia upande mwingine kuna ubadhirifu mkubwa unafanywa serikalini, viongozi wanaiba mabilioni kwa mabilioni na huoni wakichukuliwa hatua yoyote fedha hizo kurudishwa.
Kuliko kuwabana wanafunzi waliosomeshwa kwa mkopo ambao wengi kurudisha pesa hizo tunajua haiwezekani, kwanini vongozi wote waliothibitika kuiba fedha za umma hawawajibishwi na fedha hizo kusaidia kwenye elimu ya juu wanafunzi wakasoma bure?
Mianya ya ubadhirifu na ufisadi ikizibwa serikali ina uwezo kabisa wa kufanya elimu ya msingi mpaka chuoni nchini kuwa bure. Tatizo ni nini?