Mwifwa
JF-Expert Member
- Apr 3, 2017
- 46,924
- 122,195
Nimejaribu kutafakari kidogo tu kwa utashi wangu na kubaini jambo ambalo sijafurahishwa nalo japo ni jema.
Ni takribani miezi 3 tangu Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki(CHADEMA)-Tundu Lisu ashambuliwe na watu wasiojulikana kule mjini Dodoma.
Siku hiyo kulionekana na ushirikiano wa Wabunge wote wa Upinzani na CCM kufanya juhudi ili apelekwe Nairobi kwa Matibabu ambapo hadi leo bado yupo huko.
Toka hiyo siku aliposafirishwa majira ya saa 7 usiku kuelekea Nairobi alisindikizwa na Wabunge wote(Upinzani na CCM) kuanzia Hospital ya Mkoa wa Dodoma hadi uwanja wa Ndege hapo Dodoma, hakuonekana mbunge au kiongozi yeyote kutoka CCM kwenda kumjulia hali isipokuwa Lazaro Nyalandu(Kipindi hicho kabla hajahama CCM).
Juzi VP-Mama Samia Suluhu wakati akiwa ametoka kwenye sherehe za kuapishwa Rais Uhuru Kenyata alienda kumsalimia Lisu, jambo ambalo lilipokelewa na wengi kwa furaha na kuonekana kaonesha utu kwa binadamu mwenzio.
Leo tena kaenda Rais Mstaafu- Mzee Mwinyi, pia ni jambo zuri na lenye kuonesha utu.
Nimejiuliza swali dogo tu.
Kwanini siku zote hawakuweza kwenda kumsalimia alipokuwa na hali mbaya zaidi? Ni kipi kiliwazuia?
Tukumbuke hili tukio liliibua mijadala mingi sana na sintofahamu juu ya waliomshambulia.
Sasa hawa watu ambao walikataa kwenda kumsalimia wameanza kwenda tena kuanzia viongozi wa ngazi za juu, sijui kesho atafuatia nani!? Tunawaamini vipi hawa watu?
Tunaweza kusema tumeshinda vita na tuvute pumzi kidogo kumbe tunajiangamiza kwa kujisahau tu kitu kidogo halafu baadae tukaanza kujilaumu.