Kwanini vijana wanahimizwa kuoa/kuzaa?

Kwanini vijana wanahimizwa kuoa/kuzaa?

Habari ya usiku huu wakuu,

Nimekuwa nikisikia maneno haya inapotokea kijana ametangulia mbele ya haki akiwa hajaoa wala kuzaa utasikia 'Maskini bora hata angekuwa ameoa/ana mtoto'.

Hivi hii imekaaje wadau maana mimi huwa nadhani mtu akiacha watoto na mjane ni maumivu zaidi kwa hao anaowaacha wakiwa bado wanahitaji uwepo wake. Wanadai eti akiacha mtoto jina halipotei.

Naomba maoni yako ni lipi bora ni bora yule anayeaga dunia huku nyuma akiacha yatima na wajane Au yule anayeondoka peke yake na huku duniani hajaacha kumbukumbu.

Nimejisikia kuwashirikisha hili maana mara kadhaa nimeona vijana hasa wa kiume wanahimizwa kuoa na kuzaa pale umri unapofika ili wapate wa kuendeleza majina yao just in case.

Karibuni

Mimba nlokupa inaendeleaje?
 
kule kwetu anapofariki, asiye na mtoto wanasema 'obotelaga', wengine wanasemwa 'ochaga' au 'ozumalikaga'.

Kuacha watoto muhimu, kama Mungu kakupa kizazi.
 
kule kwetu anapofariki, asiye na mtoto wanasema 'obotelaga', wengine wanasemwa 'ochaga' au 'ozumalikaga'.

Kuacha watoto muhimu, kama Mungu kakupa kizazi.

Lakini mkuu...adha wanazopata watoto yatima si unaziona?
 
Kama watu wangejua wanakufa lini wangejiandaa. Nafikiri kila kitu ni mipango ukimshirikisha Mungu.
 
Sawa mkuu lakini mimi naona wanajamii wanasikitika zaidi mtu anapokuwa hajaacha mtoto

ni kweli, maybe ni kwa sababu ya kumbukumbu, unajua ukiacha mtoto hata mmoja.. mara nyingi ataheshimiwa kama ulivyoheshimiwa wewe, na kama alifanana na wewe baba yake, ndio kabisaa jamii ita-expect vitu vingi kutoka kwako baba ,vionekane na kwake pia.. wanasema kama mtoto (hasa wa kiume) amefanana na baba yake na kufanya vitu vingi anavyofanya baba yake, ikitokea baba akafariki, atakua hajafariki, atakua anaishi ndani ya mwanae.. yaani wakimwona yeye ni kama wamemwona babaye.
 
hiyo ni dhana ilozoeleka na watu ambayo haina uhalisia.
watoto ni baraka jaman japokuwa hii inaumiza wengi ambao hawajajaliwa kupata watoto mungu awe pamoja nao waweze kupata watoto
 
Na ni wangapi wameoa lakini bado uzinzi unaendelea kuwa sehemu ya maisha, michepuko na nyumba ndogo kibao si nafuu asiyeoa

Ni kweli mkuu kuoa si dawa ya kutibu uzinzi....dawa ni damu ya Yesu tu baaas
 
Na ni wangapi wameoa lakini bado uzinzi unaendelea kuwa sehemu ya maisha, michepuko na nyumba ndogo kibao si nafuu asiyeoa

Kufanya mapenzi kabla ya ndoa ni dhambi, kufanya mapenzi na mtu asie mkeo ni dhambi pia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom