Kwanini vijana wanahimizwa kuoa/kuzaa?

Kwanini vijana wanahimizwa kuoa/kuzaa?

Khantwe

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
59,468
Reaction score
119,623
Habari ya usiku huu wakuu,

Nimekuwa nikisikia maneno haya inapotokea kijana ametangulia mbele ya haki akiwa hajaoa wala kuzaa utasikia 'Maskini bora hata angekuwa ameoa/ana mtoto'.

Hivi hii imekaaje wadau maana mimi huwa nadhani mtu akiacha watoto na mjane ni maumivu zaidi kwa hao anaowaacha wakiwa bado wanahitaji uwepo wake. Wanadai eti akiacha mtoto jina halipotei.

Naomba maoni yako ni lipi bora ni bora yule anayeaga dunia huku nyuma akiacha yatima na wajane Au yule anayeondoka peke yake na huku duniani hajaacha kumbukumbu.

Nimejisikia kuwashirikisha hili maana mara kadhaa nimeona vijana hasa wa kiume wanahimizwa kuoa na kuzaa pale umri unapofika ili wapate wa kuendeleza majina yao just in case.

Karibuni
 
mimi nadhani uoe au usioe, siku ukifariki bado maumivu yatakua ni yale yale kwa wale wachache waliokupenda.. kwa familia yako ya kwanza (baba, mama na ndugu zako) na famili yako ya pili yaani mke na watoto (kama ulikua nayo).
 
Mada nzuri hii…
Nakubaliana na mdau hapo juu kwamba uwe umeoa au hujaoa lazima utaacha maumivu tu na hio fikra ya kwamba ukifariki ukiwa umeoa utaacha jina au mjane ni majaaliwa tu hakuna anayetaka kufa kabla hajakula maisha lakini ni kitu ambacho kipo nje ya uwezo wetu...unaweza ufariki na mtoto afariki vielvile na unaweza uoe na usijaaliwe mtoto…Mtu aoe akiwa tayari kuoa na aishi kwa kujua kifo kipo na kinaweza kutokea wakati wowote,kwahio furahia maisha wakati unaporuhusu na si kwa kuwanufaisha watu!
 
Sawa mkuu lakini mimi naona wanajamii wanasikitika zaidi mtu anapokuwa hajaacha mtoto
 
we haupendi watoto?

Napenda sana mkuu nia yangu hapa ni kutaka kujua ni lipi bora....mtu kufariki akiwa ameacha jina(watoto)na mjane akiwa mbichi kabisa au kuondoka akiwa hana mtoto. Mods nao wameedit tittle yangu na kuiweka ambavyo sikutaka matokeo yake inaleta mkanganyiko
 
Ni kwel jamii inahimiza vijana kuoa / kuolewa mapema ili kuacha kumbukumbu na kuendeleza kizazi

Machungu yanakuwepo no matter ana mke or mtoto.japo akiwa na watoto na mke na ikatokea kwa bahat mbaya alikuwa hajawaandalia future inauma zaid.

Kuzaa ni muhimu ili kizazi, ukoo, undugu usipotee tunataka mwendelezo
 
  • Thanks
Reactions: HMS
Sawa mkuu lakini mimi naona wanajamii wanasikitika zaidi mtu anapokuwa hajaacha mtoto

Best wanasikika zaid kwa mfano hao wazazi walikuwa na mtoto mmoja tuu na akafa bila kuzaa
Je huoni uzao wa babake utakuwa umekwisha? Baada ya mama na babake kufa? Kuna familia ni muhimu kuzaa mapema au kuzaa watoto wengi kwa ajili ya mwendelezo wa kizazi.
 
Mada nzuri hii…
Nakubaliana na mdau hapo juu kwamba uwe umeoa au hujaoa lazima utaacha maumivu tu na hio fikra ya kwamba ukifariki ukiwa umeoa utaacha jina au mjane ni majaaliwa tu hakuna anayetaka kufa kabla hajakula maisha lakini ni kitu ambacho kipo nje ya uwezo wetu...unaweza ufariki na mtoto afariki vielvile na unaweza uoe na usijaaliwe mtoto…Mtu aoe akiwa tayari kuoa na aishi kwa kujua kifo kipo na kinaweza kutokea wakati wowote,kwahio furahia maisha wakati unaporuhusu na si kwa kuwanufaisha watu!

Maneno yako Kuntu
 
Unaweza kuzaa mtoto halafu akawa jambazi, au kahaba, au mvuta unga, sasa huoni kama anakuharibia jina tu. Mtoto mipango ya Mungu, lolote linawezekana, ndo maana tukafunzwa kumuomba, kumwachia yeye akuchagulie, kumwamini na kumshukuru.
 
Oa pale unapoona umejiandaa, kuwa na mtoto pale unapoona umejiandaa sio kuzaa hovyo kwa kisingizio cha kucha uzao.

Kuwa na mtoto ni kazi nzito sana
 
Best Khantwe hulali
Mashuti ya usiku kama CNN sio
Back to topic

Ni kwel jamii inahimiza vijana kuoa / kuolewa mapema ili kuacha kumbukumbu na kuendeleza kizazi

Machungu yanakuwepo no matter ana mke or mtoto.japo akiwa na watoto na mke na ikatokea kwa bahat mbaya alikuwa hajawaandalia future inauma zaid.

Kuzaa ni muhimu ili kizazi, ukoo, undugu usipotee tunataka mwendelezo

Hahahah....mi popo. Poa umesomeka kwa hiyo ukiwa unazaa unatakiwa uwaandalie wanao future mapemaaa
 
Last edited by a moderator:
Unaweza kuzaa mtoto halafu akawa jambazi, au kahaba, au mvuta unga, sasa huoni kama anakuharibia jina tu. Mtoto mipango ya Mungu, lolote linawezekana, ndo maana tukafunzwa kumuomba, kumwachia yeye akuchagulie, kumwamini na kumshukuru.

Amen....
 
  • Thanks
Reactions: HMS
Oa pale unapoona umejiandaa, kuwa na mtoto pale unapoona umejiandaa sio kuzaa hovyo kwa kisingizio cha kucha uzao.

Kuwa na mtoto ni kazi nzito sana

Ni kweli mkuu... Ukizaa huna mbele wala nyuma then ikatokea bahati mbaya ukaondoka ndo mwanzo wa kuzalisha machokoraa
 
Hii mada nzuri kijana akifa mapema ajaoa wala kuzaa uacha uzuni mwingi kwani hakuacha wa kujenga taifa. Suala la ujane si issue kubwa ndio maana vijana wengi kwa kuhofia kuwa kunaweza kukatokea kifo wanatafuta sana wake wenye uelewa au wanaojishughulisha wenye ujuzi wa kuwaingizia kipato.

Kuna lawama nyingi vijana wanashindwa kuoa ni kwa sababu hawataki mizigo. Kuna visichana vingi kwa kudanganywa na sifa za uzuri hawataki shule eti wanasomewa, wanaitwa magoli kipa. Dunia ya sasa sio ya kuoa golileeper.

Mimi uamuzi wa kuoa ilinichukua miaka 4 kupekua , nilijitahidi kuoa mfanyakazi ni mzuri kinoma lakini sifa ya kwanza nilioa kazi.

Ukioa wa kazi anakuwa anajiamini ili hata Ukifa mijamaa itakayoitwa baba inavusha watoto kwa kutupia vujisenti
 
Asante ndugu....well said
 
Mada nzuri hii…
Nakubaliana na mdau hapo juu kwamba uwe umeoa au hujaoa lazima utaacha maumivu tu na hio fikra ya kwamba ukifariki ukiwa umeoa utaacha jina au mjane ni majaaliwa tu hakuna anayetaka kufa kabla hajakula maisha lakini ni kitu ambacho kipo nje ya uwezo wetu...unaweza ufariki na mtoto afariki vielvile na unaweza uoe na usijaaliwe mtoto…Mtu aoe akiwa tayari kuoa na aishi kwa kujua kifo kipo na kinaweza kutokea wakati wowote,kwahio furahia maisha wakati unaporuhusu na si kwa kuwanufaisha watu!

Amen mama
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom