Hizo nafasi nyingine wanazotoa za mafungu mafungu ,haina maana ya kuwa wanasumbua watu kwenda kuwaita huko Dodoma nk , wawe wanachukua kanzi data Tu ,sioni haja ya kutoa ajira 2-3 halafu unakuta mamia ya watu kwenda kuminyana huko ,kama kuna watu wamefanyiwa usahili siku za nyuma na kufaulu oral interview ,wapewe hizo kazi ,
Na kingine kuhusu lile suala la kuziacha taasisi kufanya recruitment , sidhani kama ni busara , tunajua Magumashi na corruption na nepotism iliyopo nchi hii ,hasa public institutions , wakifanya hivyo watu wengi wasio na links za rushwa na upendeleo humo serikalini kazi watazisikilizia kwenye bomba .
Utumishi wana mapungufu ila umesaidia sana kuondoa yale magumashi katika mfumo wa kuajiri public sector , kuna mapungufu bado yapo cha muhimu wawe flexible Tu kuweka mabadiliko yanayowezesha fairness kwa wote katika mchakato wa ajira ,