HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Safari Yangu ya Kupata Ajira Serikalini

kwanza nianze kwa kusema nilikuwa mwajiriwa kwenye asasi ya kiraia baada ya kumaliza chuo tuu ambapo nilikuwa nalipwa mshahara ambao ulikuwa unatosha kukidhi mahitaji yangu, kufanya uwekezaji na kiasi kingingine nilikuwa na tunza kama akiba

Sababu kubwa iliyo nifanya nikaomba ajira serikalini ni kupata makazi ya kudumu maana uko nyuma unaweza fanya kazi miaka miwili kwenywe mkoa flani kisha mradi ukiisha unapelekwa mkoa mwingine ichi kitu nilikuwa nakichukia sana maana kilikuwa kinanifanya naanza upya kuanzia mipango yangu mpaka mwenendo wa maisha mbaya zaidi uwekezaji nilio ufanya kwa kipindi cha miaka miwili inaonekana sio kitu maana usimamizi ni duni ivyo nikaona suruhu ya kudumu ni kutafuta kazi serikalini angalua naweza pata makazi ya kudumu ivyo nikaanza lasmi mchakato wa kuomba kazi serikalini.

Mwezi wa nane 2024 lilitolewa tangazo la nafasi 100+ za kada yetu ambapo mwajiri alikuwa MDAs & LGAs ivyo lasmi nikafungua accont ya ajira portal na kutuma maombi kwa umakini mkubwa sana kwa kuzingatia kanuni zote za kuomba ajira

Pia mwezi wa tisa 2024 lilitolewa tena tangazo la nafasi za kazi kupitia Wakala wa huduma za Misitu(TFS) ambapo kwenye kada yangu walikuwa wanahitaji mtu mmoja tuu ivyo nikatuma maombi kwa umakini mkubwa sana na kuzingatia taratibu zote za maombi ya ajira

Baada ya apo mwezi wa kumi 2024 nilianza maandalizi maana nilitegemea miezi miwili mbele ningeitwa kwenye interview ivyo nilitenga masaa mawili asubui (5:00-7:00 Am) na masaa mawili usiku ( 9:00-11:00pm)

Kuhusu dhana za kusomea nilikuwa natumia daftari la quare 2 na Laptop, na kwaupande wa notice nilikuwa nazo kwanzia semester ya kwanza mpaka ya mwisho ivo mambo yalikuwa poa ( naomba niongelee kuhusu notice baada ya kumaliza chuo nilitumia Google Drive kuhifadhi notice zote nilizo zitumia wakati nipo chuoni ivyo muda wowote naweza kuzipata kwa kupitia email yangua, apa ndipo watu wengi tunakosea maana unataka kusoma lakini cha kusoma huna kwasababu ya kukosa notice maana ata ukiomba kwenye group la WhatsApp la chuo au kwa mtu awezi kukutumia notice za miaka mitatu au mitano yote ivyo utajikuta unakwama ivyo naomba vijana wenzangu tutumie Goolge Drive kutunza vitu vyetu maana ni rahisi pia muda wowote unaweza zipata ata ukipoteza simu au laptop )

Ivyo maandalizi yaliendelea bila kusahau kuomba na kutoa sadaka kila nikienda kwenye nyumba ya ibada, kukata tamaa kulikuwepo maana hadi mwezi wa kumi na moja majina ya walio itwa kwenye usahili yalikuwa ayajatoka lakini nikikumbuka nini nataka ivyo nilikuwa najipa moyo na kuendelea na maandalizi

Mwezi wa kumi na moja 2024 walitoa nafasi za ajira za uwalimu ngazi ya Secondary kwenye kada yangu zilikuwa kama 20+ ivyo nilituma maombi huku nikiendelea na maandalizi bila kusahau kuomba na kutoa sadaka

Mwezi wa kumi na mbili mwishoni 2024 majina ya walio itwa kwenye usahili za uwalimu yalitoka lakini sikwenda maana niliweka nadhili kwa Mungu kwamba nitapata ajira kwenye wizara, idara, au wakala na sio Tamisemi ivyo sikwenda kwenye huo usahili ingawa jina langu lilikuwepo

Mwezi wa pili mwishoni 2025 Wakala wa Huduma za Misitu(TFS) walitoa majina ya watu walio itwa kwenye usahili na jina langu lilikuwepo lakini tulio itwa tulikwa 80+ na wanataka mtu mmoja tuu

Ivyo maandalizi yaliendelea uku nikimshukuru Mungu kwa kua jina langu lilikiwepo ivyo kwa wastani nilitumia miezi mitano kujiandaa na usahili

Mwezi wa tatu 2025 nilifanya usahili wa kuandika kupitia mtandao na kufanikiwa kwenda hatua ya vitendo hapa tulichaguliwa watu kama 60+ maana walichukuwa watu walio pata maswali yote yani alama 100 (hapa naomba nitoe ufafanuzi kidogo siku niliyo enda kufanya usahili sikumwambia mtu yoyote yule ata mtu ambaye nipo naye kwenye mahusiano maana kazini nilisema naumwa, nilivyo enda kwenye usahili nilifikia Lodge ingawa kulikuwa na ndugu au jamaa ambao wapo karibu na kituo cha usahili lakini sikwenda kwao maana niliona nitakosa uhuru wa kujiandaa pia itakua vigumu kuwa siri yangu mimi na Mungu wangu ivyo wengine watajua, nilifanya ayo yote kwa sababu mimi huwa naamini kwamba jambo lolote ambalo ukilifanya kwa usiri huwa linafanikiwa sana kuliko lile unalo litangaza hii ni imani yangu binafsi ) pia nilijitaidi kuvaa kama naenda kusimamia ubatizo upande wa wakwe maana nilivunja kabati hadi watu walijua mimi ni msimamizi kumbe na mimi nimekuja kufanya sahili

Baada ya apo maandalizi ya usahili wa vitendo ulikamilika kwa kusafisha mwili wangu kwa umakini kabisa maana nilijua lazima nitavua nguo zote nikiwa kwenye huo usahili, ambapo ilikuwa ni kupima afya ( ukimwi, kisukari, BP, makovu makubwa, macho,usikivu, tatto, uzito na urefu) ivyo niliingia kwa Dr na kupima ivyo vitu lakini wakati ananipima BP nilikuwa na kitete na hofu ivyo mapigo ya moyo yalikuwa juu sana ivyo BP ikawa juu sana lakini Dr akaniambi hii sio BP yako endapo nikiandika aya majibu uwezi kupita ata kidigo ivyo akaniambia naomba utulie kisha vuta punzi na kuitoa njee zaidi ya mara nne baada ya apo akanipima tena na kupata vipimo sahihi kabisa. Apa pia nilivaa kama naenda kwenye harusi maana hadi wasimamizi wa usahili walisema kijana unajua kupangilia mavazi yako hongera kwa ilo

Baadea usiku matokeo ya vitendo yalitoka na kufanikiwa kupita kwenda kwenye hatua ya mahojiano apa tulibaki kama watu 58 ivi. Niliendelea kumshukuru Mungu kwa kila hatua niliyo pita

Siku ya usahili wa mahojiano kwanza apa nilivaa vizuri kama kawaida yangu ( suruali ya kitambaa dark blue, mkanda mweusi, shart la sky blue, tie nyeusi, fokona nyeusi ya kung'a na nyewele low cut alafu sina ndevu) ivyo niliwai mapema kwenye kutuo cha usahili kisha ni kafuata taratibu zote ivyo usahili ulikuwa unachukua dakika 20 kwa kila Msahiliwa ivyo mimi nilikuwa kama mtu wa 43 ivi ivyo tulikaa njee na kusubiria mpaka zamu yako ifike lakini mimi sikukaa na watu wakada yangu maana nilijua wataanza kuongelea maswali na majibu kuhusu usahili ivyo ingenitoa mchezoni basi nilitafuta watu wakada nyingine nikaa nao ivyo maongezi yao yalikuwa ayana faida kwangu maana siju nini wanaongelea, ivyo niliona watu wakiingia kwenye chumba cha usahili wanakaa kuanzia dakia 10 hadi 15 lakini ilivyo fika zamu yangu kabla sijaingia nilikumbuka ile mbinu ya Dr kuvuta punzi na kuitoa zaidi ya mara tano ili kuondao wasiwasi ivyo wakati naelekea kwenye chumba cha usahili nilifanya ivyo zaidi ya mara sita basi nikawa sina tena wasiwasi wala kitete

Nikagonga hodi kisha wakaniruhusu niingie, lakini nilivyo ingia sikukaa kwenye kiti maana nilisubiria mpaka waniambie ilichukua kama sekunde 30 ndipo wakaniambia nikae kisha usahili ukanza maswali yalikuwa matano tuu ivyo nilijibu kutokana ninavyo elewa aikuchukua hata dakika tano nikawa nimemaliza kujibu maswali yote matano lakini wakati najibu swali la mwisho ambalo lilinitaka nitaje point tano tuu nilivyo jibu, moja ya wale watu wa sahili aliniambia niongezee point ingawa nilikuwa najua point nyingine lakini nilikataa kutaja nikasema nazijua izo tuu mwisho akaniambia sawa unaweza kwenda ivyo ndani ya dakika tano nilikuwa njee ya chumba cha usahili, hapa kwa kweli nilipata hofu sana maana walisema muda ni dakika 20 alafu mimi nimetumia 5 tuu nadhani hata wenzangu walishangaa pia lakini nilikuwa sina namna ivyo ilibidi nipande boda na kurudi Lodge uku nikimuomba Mungu anipe Neema nne tuu
1. Neema ya kukubalika
2. Neema ya Kuaminika
3. Neema ya upendeleo
4. Neema ya Kibali

Baada ya apo niliendelea na maandalizi ya sahili ya MDAs and LGAs ambapo mwezi wanne 2025 walitoa majina na jina langu lilikiwepo ivyo nilienda kufanya usahili wa kuandika na nilipata kibali na kufauru vizuri ivyo nilitegemea mwezi wa tano nikafanye usahili wa mahojiano

Lakini tarehe 30 mwezi wa nne 2025 jina langu lilikuwa moja wapo wa jina moja tuuu kwenye kada yangu walio itwa kazini na Mwajiri akiwa ni Wakala wa Huduma za Misitu (TFS)

Mwisho kabisa vitu nilivyo jifunza kwenye mchakato wa kupata ajira serikalini kupitia utumishi wa uma ni kama ifuatavyo

1. Katika mchakato wa ajira kupitia Utumishi wa uma akuna upendeleo au connection ata siku moja wala awana watu wao ivyo kila mtu ni mtu wao ilimradi ufanye vizuri tuu
2. Sadaka na Maombi ndio nguzo sahihi ya kupata mahitaji ya mioyo yetu
3. Usiache kuomba kazi ata kama nafasi ni moja kila mtu ana uwiano sawa wa kupata iyo kazi ivyo usiogope
4. Maandalizi sahihi kwa muda sahihi ndio kitu kinaweza kukufanya kuwa na kujiamini kwa kila hatua unayo pitia kwenye sahili
5. Usifute notice za chuo baada ya kumaliza chuo kama ulifuta zitafute upya
6. Hifadhi notice zako zote kwenye Google Drive hapa uwezi jutia hata siku moja
7. Unapo fanya maombi ya ajira kuwa makini na kuzingatia kila sheria ya utumishi inauma sana kutokuitwa kwenye sahili kisa ujaweka sahihi kwenywe barua au ujaweka vyeti vya taaluma yako kwa kweli ichi kitu kinaumiza sana
8. Usiingie kwenye usahili na kusema ata nikibaki kwenye kanzi data ni sawa tuu maana ujui nini kinafanyika kwenye kanzi data ivyo pambana mpaka uwe kwenye nafasi ya kuitwa kazini katika awamu ya kwanza
9. Usitangaze kwa mtu yoyote yule kwamba umeomba hajira au unaenda kufanya usahili
10. Usifikie kwa mtu au ndugu pindi unuapoenda kufanya usahili maana kuna Lodge hadi za 15,000 au 20,0000 ongea na mtu wa boda atakupeleka
11 . Usiende na simu au saa kwenye usahili viache Lodge kwenye mapokezi maana vitakuletea usumbufu tuu wakati wa usahili
12. Vaa vuzuri kama autakuja kuvaa tena maana jukumu la kuvaa lipo mikonini mwako ivyo kazi kwako ( Apa Boys uwa tunazingua sana yani mtu anavaa jeans au suruali ya kitambaa bila mkanda au viatu vyaa wazi au jezy ya mpira kweli sio sahihi hii ni siku muhimu ivyo kuvunja kabati akuna budi kufanya ivyo)
13. Usikae na watu wa kada yako wakati mnajiandaa kuingia kwenye chumba cha usahili maana utachanganyikiwa tuu na maswali wakati mnaulizana ivyo jitaidi kuwakwepa kwa namna yoyote ile
14. Jitaidi kusoma na kuelewa majukumu ya kazi husika uliyo omba maana apo ndipo mtiani ulipo
15. Mtian wa mahojiano unakuwa na maswali matano lakini swali la kwanza lipo kwenye ufahamu wako ata kabla ujaulizwa ambalo huwa ni (tuambie wewe ni nani? apa jitaidi kujiandaa vizuri maana ndio dira au ufunguo au taa ya kijani (Green light) wa usahili wako ukizingua apa basi umearibu kila kitu)
16. Jitaidi kusoma maswali vizuri kabla ya kujibu pia usiwe na haraka ya kujibu chukua ata sekunde 20 ndio ujibu baada ya kufikiria
17. Baada ya usahili ukiambiwa nenda nyumbani fanya ivyo hata kama kuna best yako bado ajafanya usahili nenda kamsubirie stand au uko njee getini nasio eneo la usahili
18. Kwenye mtihani wa mahojiano / oral kama umeulizwa swali na wanataka point tano na wewe unajua point 2 kati ya tano usijibu ilo swali kisha wambie next ivyo ilo swali wataliacha kisha utaulizwa mwishoni wakati umekumbuka zile point nyingine tatu na kufanya kuwa point tano maana ukijibu swali lenye point tano alafu wewe ukataja point mbili apo utakuwa umemaliza ilo swali ivyo autaulizwa tena
19. Usiache kujibu swali lolote lili utakalo ulizwa kwenye usahili wa mahojiano jibu lolote litakalo kuja kichwani wewe sema maana ni bora kusema kuliko kukaa kimya
20. Andika majina yako, mahali unapotoka, namba ya simu kwenye bahasha ambayo unaweka vyeti maana unaweza vipoteza mtu akaota ivyo atakupata kwa urahisi
21. Jitaidi kuwekeza angalua 50,000 kwa mwezi baada tu ya kutuma maombi ya ajira hii itakusaidia kwenye nauli, maladhi na chukula maana usipokuwa na pesa ni vigumu kujiandaa vizuri kwasababu utaanza kuwaza mambo mengine na kuachana na usahili ivyo ndugu zangu tujitaidi kusave kwa ajili ya sahili
22. Usikate tamaa pale majina ya kuitwa kwenye usahili yatakapo chelewa kutoka bali tumia kama fursa kwako kuendelea kujiandaa vizuri na umakini wa juu kabisa
23. Ukienda kwenye usahili usiogope au kuhofia endapo ukikutana na mtu au watu ambao walikuwa wanaongoza darasani kwenu na kufanya vizuri au ata kama GPA yako ni ndogo wewe wala usitishike pale wote mpo sawa ndio maana mmeitwa wote ivyo uwepo wa uyo mtu au watu walio kuwa wanakushinda darasani wala wasikutishe maana na yeye kimoyomoyo anahofia uwepo wako hii ni win to win situation
24. Unaweza kufanya usahili kwa mara ya kwanza na ukapata kazi sio lazima ufanye sahili zaidi ya moja ndio upate kazi
25. Usaiche kuomba kwa Mungu na kutoa sadaka kabla na baada ya usahili
26. Siku ambayo utaitwa kazini taharifa iyo utapewa na mtu ambaye hata uwezi kumzania kama anajua majina yako yoye matatu au mtu ambae mlisoma wote shule ya msingi kabisa ivyo ndugu zangu tuishi kwa upendo maana uwezi kujua ni nani atakuletea taharifa njema kama iyo siku ikifika maana iyo siku wewe utakuwa auna hata hisia kama utaitwa kazini ndivyo ilivyo tokea kwangu maana majina yalitoka saa tano usiku mimi nimelala lakini nilipigiwa simu na mtu ambeye nilisoma nae shule ya msingi na kunipasha taharifa izo
27. Baada ya kupata kazi unaweza kuambia ndugu na jamaa zako isipokuwa wafanyakazi wenzako ambao ulikiwa unafanya nao kazi pia aina haja kuwaambia umeajiriwa Tamisemi au wizarani ukisema serikalini inatosha maana uwezi jua nini wanafikiria juu yako, pia usisahau kutoa Shukrani kwa Mungu

Mwisho kabisa nitoe pongezi na Mungu awabariki na kumbariki aliye anzisha uzi huu na wachangiaji wote maana wamekuwa chachu ya mimi kufanya vizuri kwenye sahili zangu. Pia naomba ndugu zangu kama auna taharifa sahihi kuhusu mchakato wajaira pindi mtu anapo kuuliza swali naomba usijibu maana kuna watu watavunjika moyo au kuwapa tumaini la uongo kisa majibu yako yasio sahihi
Ahsante sana

Hii Post ilinifanya Nifaulu Interview Yangu Ya pili baada ya Kwanza kubuma 😀

Ubarikiwe sana, Afande. Ila vipi mlimaliza lini Course Nyie? Maana nimesikia kuna wengine wana maliza Week ijayo.
 
Hivi inawezekana mtu akapata placement ( barua ya kazi ) bila utumishi kutoa PDF yoyote ??

Yani unaamka tu unakuta barua ya kazi lakini hakuna pdf yoyote iliyotolewa na utumishi kwenye website Yao ??
 
Back
Top Bottom