HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Ndugu zangu kuna maza hapa kitaa wakati anapasi nguo zake asubui ili aende kanisani pasi yake ilimgomea kuwaka.Basi akaniletea engineer EL -Marabish nimrekebishie (mwanae alimwambia nina degree ya umeme ndo alieniponza), nikamwambia mbona hilo ni tatizo dogo sana kwangu. Basi akaniachia ile pasi, namshukuru mungu niliirekebisha vizuri tu ikawa inawaka taa ila baada ya kuichunguza nikaona kama haipati joto vilee, si nikaamua niguse lile bati bana kuona kama inachemka, halooo..!!! narudia tena haloo...!!!🙌🙌 sitakuja kusahau shoti niliyokutana nayo yaani nilivutwa mkono nikahisi mkono umenyofolewa halafu kulikua na watu sasa nikawaangalia bahati nzuri hawakuusoma mchezo nikatoka nje taratibu kwenda kupigwa upepo.hapa nimeifunga vizuri kesho asubuhi nataka niwapelekee mafundi (wenye kazi zao) ikipona nitamwambia mie ndo nimeitengeneza....
Mambo yako yananifurahisha ga sana we jamaa 😂😂
 
Kwa maneno haya ya katibu kutakuwa na shida kubwa sana kwenye taasisi hivi kwanini wasiwe Kama halmashauri ukifaulu wiki tu uko kazini
Kuna vita kubwa sana mkuu unapo report wanahisi u deserve ukikuta na mtu anayejitolea ana drive anakuangalia kwa chuki utafikiri anataka kukuua

Apo unaambiwa nenda utapigiwa sahau miezi mitano sita nane ndio wanaweza kukufikilia
 
Jamani hivi kuitwa kazini kama ulifanya oral kupitia taasisi means na kaz utapat za taasisi pekee

Sikufanikiwa kwenda oral ajira za MDA & LGA za mwezi september 2024 kada afya

Nikaja kupita kwenda oral ajira ya taasisi ,ambapo walitak mtu mmoja na washampata

Sasa kila pdf nalolizoom naona wanaoitwa kazini ni wale waliofanya oral ya LGA & MDA ni kwamba sisi wa oral ya taasisi japo kada moja tupo sawa tu na wadau wa not selected majina yetu yanawekwa kapuni au inakuaje

Nimechok kupitia pdf kwa kweli
Hapana mkuu. PSRS wana uwezo wa kukupanga popote pale nafasi ikipatikana kama ulifaulu usaili na kukaa kwenye database.

USHUHUDA: Classmate wangu alifanya usaili wa ICT officer TBC, Amepangiwa kazi Halmashauri. Alitaka kukataa kwenda kuripoti ndio akashauriwa lazima aripoti kwa maana hatopangiwa kazi kama hiyo tena kwa mujibu wa kanuni za PSRS.
 
Kuna vita kubwa sana mkuu unapo report wanahisi u deserve ukikuta na mtu anayejitolea ana drive anakuangalia kwa chuki utafikiri anataka kukuua

Apo unaambiwa nenda utapigiwa sahau miezi mitano sita nane ndio wanaweza kukufikilia
Yani hii yako MIEZ 7 aise yataka moyo sana sisi tuliopata mwez huu tunaishia kusema sisi tuko karib na mwaka wa fedha tutaitwa faster tunaomba tusifike level yenu hiyo
 
Ukipata placement hautasumbuka maana hayo ni maelekezo ya katibu mkuu utumishi, hivyo jobless wote tumepata matumaini ya mchakato wa kuanza kazi kuwahishwa na pia ukishapangiwa mwajiri hana uwezo wa kukukataa.
Hii safi sana ukiomba watu ukaletewa inabidi ndani ya mwezi wawe kwenye mfumo tayari hapa kaupiga mwingi katibu
 
Yaani katufurahisha sana. Ukiwaangalia hao HRs hapo wameridhika sana na wanafurahi kutusubirisha jobless bila kuwa na sababu za msingi. Katibu mitano tena.
Kuna jamaa karipoti mwezi wa 5 mwanzon mpaka Leo hajaanza kazi walimwambia mpaka mwaka wa fedha upinduke alafu hiyo hiyo taasisi na Mimi ndo nimepelekwa nawaza Ina maana Nina muda mwengine Tena wa kula msoto kama nilivyokuwa nasubiri placement daah!!
 
Hapana mkuu. PSRS wana uwezo wa kukupanga popote pale nafasi ikipatikana kama ulifaulu usaili na kukaa kwenye database.

USHUHUDA: Classmate wangu alifanya usaili wa ICT officer TBC, Amepangiwa kazi Halmashauri. Alitaka kukataa kwenda kuripoti ndio akashauriwa lazima aripoti kwa maana hatopangiwa kazi kama hiyo tena kwa mujibu wa kanuni za PSRS.
Asante sana mkuu wangu umefufua upya matumaini yangu
 
Leo katibu mkuu utumishi Bw. Juma S. Mkomi kawatolea uvivu wote wanaochelewesha kuajiri kwa sababu zisizoeleweka wakati kabla ya kuomba kibali wamekua wametoa bajeti na kuandaa kwenye P.E .

Hali hiyo imetokana na malalamiko ya muda mrefu kwa vijana walioajiriwa na kupata barua zao lakini kukubaliwa na kuanza kazi kuna kuwa na vikwazo vya kumsubirisha mtumishi mpya kwa muda wa kufikia mpaka miezi 6 ili tu mwaka wa fedha ubadilike.

Aidha, Ametoa rai kwa waajili wote wawapokee watumishi kwani waliandaa bajeti ya kuajiriwa na kisha kuomba kibali kwa katibu mkuu utumishi.

Sambamba na hilo, Amesema kuna hali ya wasailiwa kuomba kazi mara kwa mara kwa kutotambua iwapo wako kwenye kanzidata ama hapana hivyo kupelekea wasailiwa kutumia fedha nyingi katika mchakato mzima wa ajira wakati tayari unaweza kuta msailiwa huyo amefaulu na yuko tayari kwenye kanzidata.

Vilevile, Waajiriwa wameaswa iwapo wana vijana wao wanaojitolea na hivyo kupelekea kukataa waajiriwa walioletwa na sekretarieti ya ajira yaani psrs inabidi waombe kwa kufuata utaratibu wa kuwaombea vijana hao ajira na sio lazima wakubaliwe maombi yao kwani ni utashi wa katibu mkuu kuridhia maombi hayo ama kukataa.
Pamoja na hali hiyo waajiri wameshauriwa kutotumia mwanya wa vijana wanaojitolea kuchelewesha ama kuendelea na kukataa waajiriwa wapya waliopambana na kupata kazi kwani hali hiyo haikubaliki. "Utajiskiaje kijana wako anafanyiwa jambo hilo wakati amefaulu usaili na amepata barua ya kuajiriwa? Bw. Mkomi amesema.

Katika kumalizia kikao hicho na washauri wa waajiri amesema kigezo cha kusingizia uhakiki wa vyeti sio kweli kwani mifumo haifanyi kazi hivyo. Pia amesema wakipata taarifa za muajiriwa mpya kucheleweshwa kuajiriwa watadili na muajiri kwa kufuata sheria kanuni na taratibu.

Link ya video hiyo

View: https://youtu.be/110Tv8nImIA?si=azEQ6uZQEfh-hck2

Tunamuomba Mwenyezi Mungu ,kauli ya Katibu ifanyiwe kazi mapema iwezekanavyo. Asante
 
Dah. Afadhali, maana miezi miwili inakata, kila ukimcheck anakuambia usiwe na haraka Afisa. Yaani unapewa cheo kikubwa wakati nipo mtaani naendelea kuchakaa. Dah!
Inawezekana jamaa huwa wanazipiga hizo hela za mishahara au vipi ndio maana wana target mwaka mpya wa fedha ?
 
Kuna jamaa karipoti mwezi wa 5 mwanzon mpaka Leo hajaanza kazi walimwambia mpaka mwaka wa fedha upinduke alafu hiyo hiyo taasisi na Mimi ndo nimepelekwa nawaza Ina maana Nina muda mwengine Tena wa kula msoto kama nilivyokuwa nasubiri placement daah!!
Sio mchezo, ila huo utaratibu wa kusubiri mwaka wa fedha kubadilika ndio uhuni ambao katibu mkuu kaukemea. Natumaini mwezi wa saba tutaingia kazini mkuu.
 
Back
Top Bottom