Bongo dar es salaam
JF-Expert Member
- May 11, 2020
- 235
- 589
Ukiwaza unaishiwa pozi ila kama jinsi tulivyopata placement ndani ya mwez mmoja na ndivyo tutakavyowai kuingiza kazini Mungu anatupiganiaAisee wasije wakatufanyia hivyo
Ukiwaza unaishiwa pozi ila kama jinsi tulivyopata placement ndani ya mwez mmoja na ndivyo tutakavyowai kuingiza kazini Mungu anatupiganiaAisee wasije wakatufanyia hivyo
Leo katibu mkuu utumishi Bw. Juma S. Mkomi kawatolea uvivu wote wanaochelewesha kuajiri kwa sababu zisizoeleweka wakati kabla ya kuomba kibali wamekua wametoa bajeti na kuandaa kwenye P.E .
Hali hiyo imetokana na malalamiko ya muda mrefu kwa vijana walioajiriwa na kupata barua zao lakini kukubaliwa na kuanza kazi kuna kuwa na vikwazo vya kumsubirisha mtumishi mpya kwa muda wa kufikia mpaka miezi 6 ili tu mwaka wa fedha ubadilike.
Aidha, Ametoa rai kwa waajili wote wawapokee watumishi kwani waliandaa bajeti ya kuajiriwa na kisha kuomba kibali kwa katibu mkuu utumishi.
Sambamba na hilo, Amesema kuna hali ya wasailiwa kuomba kazi mara kwa mara kwa kutotambua iwapo wako kwenye kanzidata ama hapana hivyo kupelekea wasailiwa kutumia fedha nyingi katika mchakato mzima wa ajira wakati tayari unaweza kuta msailiwa huyo amefaulu na yuko tayari kwenye kanzidata.
Vilevile, Waajiriwa wameaswa iwapo wana vijana wao wanaojitolea na hivyo kupelekea kukataa waajiriwa walioletwa na sekretarieti ya ajira yaani psrs inabidi waombe kwa kufuata utaratibu wa kuwaombea vijana hao ajira na sio lazima wakubaliwe maombi yao kwani ni utashi wa katibu mkuu kuridhia maombi hayo ama kukataa.
Pamoja na hali hiyo waajiri wameshauriwa kutotumia mwanya wa vijana wanaojitolea kuchelewesha ama kuendelea na kukataa waajiriwa wapya waliopambana na kupata kazi kwani hali hiyo haikubaliki. "Utajiskiaje kijana wako anafanyiwa jambo hilo wakati amefaulu usaili na amepata barua ya kuajiriwa? Bw. Mkomi amesema.
Katika kumalizia kikao hicho na washauri wa waajiri amesema kigezo cha kusingizia uhakiki wa vyeti sio kweli kwani mifumo haifanyi kazi hivyo. Pia amesema wakipata taarifa za muajiriwa mpya kucheleweshwa kuajiriwa watadili na muajiri kwa kufuata sheria kanuni na taratibu.
Link ya video hiyo
View: https://youtu.be/110Tv8nImIA?si=azEQ6uZQEfh-hck2
Samahani chief, ulifanya oral interview lini na placement ukapata lini? Lengo langu ni kukadiria PDF langu litatoka liniUkiwaza unaishiwa pozi ila kama jinsi tulivyopata placement ndani ya mwez mmoja na ndivyo tutakavyowai kuingiza kazini Mungu anatupigania
Kaongeze received ya Ile kazi Msimamizi wa Watoto sijui Mlezi wa watotoSamahani chief, ulifanya oral interview lini na placement ukapata lini? Lengo langu ni kukadiria PDF langu litatoka lini
Sija qualifyKaongeze received ya Ile kazi Msimamizi wa Watoto sijui Mlezi wa watoto
Afu mambo mengine yaendelee Mkuu
Watu toka mwezi wapili mbona we karibu sanaHizi placement zina stress, watu wamefanya oral tareh 14/5 mpaka leo holaaaa
DuhWatu toka mwezi wapili mbona we karibu sana
Restless Hustler wewe ni mmoja wa watu wanaosubiria ilo pdf la JUNE kwa hamu kubwa..Samahani chief, ulifanya oral interview lini na placement ukapata lini? Lengo langu ni kukadiria PDF langu litatoka lini
Duuh mpaka sasa bado hujaanza kazi mkuu!?Sio mchezo, ila huo utaratibu wa kusubiri mwaka wa fedha kubadilika ndio uhuni ambao katibu mkuu kaukemea. Natumaini mwezi wa saba tutaingia kazini mkuu.
Oral nimefanya tarehe 18 mwez wa 5 placement nipata tarehe 13 mwez wa sita ni wiki nne kasoloSamahani chief, ulifanya oral interview lini na placement ukapata lini? Lengo langu ni kukadiria PDF langu litatoka lini
Mkuu Mkuu upo ndugu yangu?uhakika unao? mkuu Restless Hustler wewe ni moja wa watu wanaosubiria pdf la JUNE kwa hamu kubwa.. waliachie tuu kama vipi
Nipo ndugu yanguMkuu Mkuu upo ndugu yangu?
Hakika mkuu ngoja tuendelee kuwa wavumilivu🙏Ukiwaza unaishiwa pozi ila kama jinsi tulivyopata placement ndani ya mwez mmoja na ndivyo tutakavyowai kuingiza kazini Mungu anatupigania
Nafikiria kwa mtumishi mwenyew kwenda kulalamika PSRSamesema wakipata taarifa za muajiriwa mpya kucheleweshwa kuajiriwa watadili na muajiri kwa kufuata sheria kanuni na taratibu.
Hii taarifa wanaipataje ?
Okay. AhsanteOral nimefanya tarehe 18 mwez wa 5 placement nipata tarehe 13 mwez wa sita ni wiki nne kasolo
Ili kupunguza stress ni vyema ukasubiri PDF.Hivi wakuu kuna haja ya kungoja pdf? Si nasikia sasa hivi placements unaikuta kwenye account yako masaa matatu kabla ya mkeka?