Dah!!, haya mambo yanahitaji neema za Mungu. Binafsi interview za ualimu za Januari nilipigwa chini bila huruma kwenye written kwa sababu nilikosa document moja original. Juzi kati hapa nikaitwa moja kwa moja Oral pale DUCE, maswali yao ni ya kawaida lakini yanahitaji experience zaidi, kama umetoka chuoni na hujafundisha popote basi angalau uwe hujahitimu miaka mingi iliyopita, vinginevyo usipokaa sawa unapigwa knockout. Hebu fikiria maswali matano na kila swali linahitaji point zisizopungua nne uyajibu ndani ya dakika tano pekee😔. Mimi nilijibu kwa kadri ya uwezo wangu, mengine namuachia Mungu.